March 2015
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Na Afisa habari RS-  Mwanza

MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA MH. ZAINAB  TERACK,  AKIHUTUBIA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAJI  KIMKOA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MWANZA WILAYANI SENGEREMA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amewataka wahandisi wa miradi ya Maji katika  Mkoa na wale wa  Halmashauri na miji midogo mkoani hapa kusimamia vizuri miradi ya maji na kwamba fedha zitakazotumika kwenye miradi hiyo zitumike vizuri ilikusaidia kukamilika  katika  viwango vinavyotakiwa.

Akizungumza kwa kwenye kilele cha maji  mkoani hapa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Zaibabu Terack kwenye  sherehe za kilele cha maji zilizofanyika Wilaya ya Sengerema, Mulongo alisema kuwa miradi ya maji Mwanza inaweza kukamilika kwa wakati kama fedha za miradi hiyo zitatumika vizuri.

Alisema kazi ya kusimamia miradi hiyo inapaswa kufanywa na wakandarasi wa Halmashauri na miji midogo ambayo inapitiwa na miradi hiyo na kwamba kama fedha za miradi zitatumika kinyume Mwanza itaendelea kuwa na tatizo la maji.

Katibu Tawala msaidizi maji, Wariba Sanya
akitoa taarifa ya hali ya maji na miradi itakayo
Tekelezwa Mkoani Mwanza.
“Naomba niwaombe Wakandarasi wa maji kutoka Halmashauri zote za Mwanza pamoja na miji midogo ambayo inapitiwa na miradi ya maji isimamie vizuri miradi hiyo.Nataka kuona fedha za miradi zinatumika vizuri na miradi yote inatekelezwa kwa wakati,”alisema Mulongo na kuongeza:

“Kama tutakwenda kinyume na matumizi ya fedha za miradi ya maji tutaendelea kuwa na tatizo la maji na kero za maji ambazo zinawakabili wananchi zitaendelea, hivyo sitakubali kuona wananchi wanateseka kwa kukosa maji wakati Serikali yao inawajali kwa kuwaletea miradi ya maji.”

Akisoma taarifa ya miradi ya maji, Katibu tawala msaidizi maji Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Warioba Sanya, alisema Serikali imewekeza Sh.84.46 bilioni  kwa ajili ya miradi ya Maji  ya mkoa wa Mwanza  kupitia mapango wa maji wa (WSDP).

“Mwanza tunaishukuru Serikali, kwani licha ya kutupa miradi mbalimbali ya maji Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maji vijijini 217 kati ya hiyo miradi 140 imekamilika sawa na asilimia 65 na kwamba miradi iliyobaki itakamilika ifikapo mwezi juni mwaka huu,”alisema Sanya.

Mkoa wa mwanza kwa hivi sasa unawapatia maji wananchi kwa asilimia 61.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


 

Ndugu Mheshiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa,

Ngugu Katibu Tawala Mkoa

Ngudu  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,

Ndugu  Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya ,

Ndugu  Waheshimiwa Wabunge,

Ndugu Wakurugenzi wa Halmashauri,

Ndugu Waheshimiwa Madiwani,

Ndugu Viongozi wa Dini,

Ndugu  Viongozi wa Vyama vya Siasa,

Ndugu Wahandisi wa Maji wa Wilaya na Mamlaka za Maji,

Ndugu Viongozi wa Chama na Serikali,

 
MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA BIBI ZAINAB TERACK ALIYESOMA HOTUBA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MWANZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA KILELE CHA SIKU YA MAJI. 

Awali ya yote, ninayo heshima kubwa kuwapongezeni katika kushiriki siku hii ya kilele cha wiki ya maji Mkoa wa Mwanza, siku ambayo huadhimishwa siku kama ya leo ya tarehe 22/03 kila mwaka Duniani kote.  Ninayofuraha kunialika hapa kuwa Mgeni rasmi siku ya leo.

Ndugu wananchi,  

Wiki ya Maji huadhimishwa kila mwaka Duniani, kauli mbiu ya mwaka huu kama mlivyokwisha elezwa ni MAJI KWA MWENDELEO ENDELEVU ( WATER FOR SUSTAINABLE DEVELOPMENT).  Natumaini wiki hii imewajengea elimu na uzoefu wa kutosha kutoka kwa wageni mbalimbali walioshiriki  wiki ya Maji.

Ndugu wananchi,

Nimeambiwa kwamba wastani wa utaoji wa huduma ya Maji safi Mkoa wa Mwanza ni asilimia 61, ikiwa maelengo tuliyojiwekea katika MKUKUTA I ni asilimia 65 kufikia June 2015.  Hivyo bado tuna changamoto ya asilimia 4 ili tuweze kukamilisha kiasi kilichobaki kwa muda uliobaki. Aidha, nimeambiwa  kuwa kuna jitihada kubwa za Serikali zinazoendelea katika kuboresha huduma ya maji mijini na vijijini ikiwa ni pamoja na; kujenga miradi mipya katika Mkoa  ikiwemo  Mradi wa maji uliokamilika wa Ngudu Mjini, Ujenzi wa Mradi wa Maji unaoendelea Mjini Nansio na Sengerema, ujenzi wa miradi ya maji maeneo ya milimani Mjini Mwanza( Igogo, Ibanda, Bugarika, Mjimwema nk) na  ujenzi wa miradi ya maji vijiji vipatayo 217.

Aidha, Nimeambiwa pia kuhusu mipango mizuri iliyopo ya kuboresha miundombinu ya Maji katika Mji wa Misungwi na Magu, mradi ambao unatarajiwa kuanza mwenzi Septemba mwaka huu.

Hivyo, niwatake wahandisi wa maji wanaohusika na shughuli za miradi hii ikiwemo MWAUWASA( wanaosimamia ujenzi wa miradi ya Maji mijini), Secretariati ya Mkoa na Wahandisi wa Wilaya na Mameneja wa Mamlaka za miji midogo,  wafuatilie kwa karibu Wakandarasi wa miradi hii na kuhakikisha inakamilika kwa wakati, ubora na thamani ya fedha ionekane katika kazi hizi. Fedha nyingi Serikali imewekeza katika kuboresha huduma ya maji Mkoani Mwanza, hivyo nataka nione matokeo yanayofanana na uwekezaji huo.

Ndugu wanachi,

Niwakumbushe tu kwamba wataalamu wanasema asilimia 80 ya magonjwa yanayotupata yanahusiana na maji (yawezekana kwa kunywa au kuoga maji machafu au kukosekana kwa maji safi). Pia, maji hutumika katika uzalishaji wa vitu viwandani na shughuli zetu za kila siku za kiuchumi hususani uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.

Hivyo, nami nakubaliana kabisa na kauli mbiu hii kuwa Maji ni muhimu katika maendeleo endelevu. Kwa pamoja tunaweza.

Ndugu wananchi,

Jukumu la kutunza na kulinda vyanzo vya maji visichafuliwe ni la kwetu sote,  Sera yetu ya maji inatutaka tusimamie miradi yetu ya maji inayokamilika kujengwa  kwa kutumia vyombo vya watumia maji kama vile bodi za maji na jumuiya za watumia maji. Kwa sasa katika Mkoa nimeambiwa tunazo jumuiya zipatazo 157 na bodi za maji 5. Vyombo hivi bado havitoshi kusimamia miundombinu yetu ya maji tuliyonayo. Sehemu nyingi bado tunatumia kamati za maji zilizochini ya serikali ya kijiji, miradi mingi iliyojengwa miaka ya 1970 ilikufa kwa sababu ya kukosekana usimamizi bora wa wananchi.  Hivyo, niwaombe Halmashauri za wilaya kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha kwamba katika kila mradi wa maji ya bomba unaojengwa, jumuiya hizi zinaundwa na kusajiliwa  kwa mujibu wa sera na sharia ya maji mapema iwezekanavyo ili ziendeshe na kusimamia miradi hii.

Ndugu wananchi.

Mtakumbuka kuwa utunzaji wa mazingira, Upimaji wa viwanja na ujenzi wa makazi bora ni vitu muhimu katika upatikanaji wa maji na uzuiaji wa majanga yanayotokana na mvua nyingi au vimbunga. Mfano mzuri ni janga la uezuaji wa paa za nyumba uliokumba wilaya yetu ya Kwimba mwezi ulioisha, nachukua fursa hii kuwapa pole wanachi wenzetu wa Wilaya ya Kwimba kwa Mkasa huo.

Niwape moyo tu kwamba Serikali ya Mkoa iko pamoja nanyi katika wakati huu mgumu.

Ndugu wanachi,

Ni matumaini yangu kuwa tutakuwa makini kushiriki shughuli za maji na usafi wa mazingira ili kuboresha afya ya jamii yetu kwa ujumla.  Pia, natumaini nyote mumefurahi na kutendea haki kilele hiki cha wiki ya Maji Mkoa. Nawatakieni safari njema mara mrudipo maeneo yenu ya kazi.

 

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA.

BAADHI YA WAGENI  WALIOHUDHURIA KATIKA MAADHIMISHO HAYO. 

KIKUNDI CHA AKINA MAMA NGUVU KAZI KIKITUMBUIZA KATIKA SHREHE HIZO.

KATIBU TAWALA SEKSHENI YA MAJI WARIOBA SANYA AKITOA TAARIFA YA HALI YA MAJI KATIKA MKOA WA MWANZA

MTAALAM MSHURI KUTOKA MAMLAKA YA MAJI MWANZA, MWAUWASA AKITOA MAELEZO KUHUSU HALI YA MIRADI YA MAJI WANAYO ISIMAMIA KATIKA MKOA WA MWANZA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kufanya makubwa zaidi  2015.
Na : Afisa Habari RS Mwanza.
MAAFISA WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA WAKIWA KATIKA MOJA YA ZIARA WILAYANI KUKAGUA MAENDELEO YA SHUGHULI MBALI MBALI ZA SERIKALI.
Mkoa wa Mwanza umeshika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne yaliyo tangazwa hivi karibuni kwa kupata ufaulu wa GPA 2.67, huku ukitanguliwa na Mkoa wa Pwani (GPA 2.79) na Shinyanga (GPA 2.69) haya  yamebainishwa na Afisa Elimu Taaluma katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza Mwl. Gervas Sezulu wakati wa mahojiano baina yake na Mtandao huu wa Mkoa.
Sezulu amesema, ufaulu huo unaifanya Mwanza kuwa moja ya Mikoa inayofikia malengo ya Mpango wa matokeo makubwa sasa yaani Big Results Now (BRN). “Mwishoni mwa mwaka jana (2014), mitihani ya kidato cha nne ilifanyika nchini kote na Mkoa huu wa Mwanza ukiwa ni mmoja wapo shule zetu zote ” alisema Sezulu na kuongeza kuwa, kwa Mkoa wa Mwanza jumla ya wanafunzi 19,783 waliandikishwa kufanya mtihani huo, walifanya mtihani huo.
Amesema, kwa matokeo ya mwaka 2013 ya mtihani huo wa kidato cha nne, Mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya 12 kwa kupata ufaulu wa asilimia 39.29 hali hiyo ulifanya Mkoa kujipanga vizuri zaidi na huku ukijiwekea mikakati kabambe itakayo wawezesha kufanya vizuri zaidi kwa mwaka 2015.
Akibainisha mikakati hiyo, Sezulu alisema ni pamoja na kuendelea kuwathamini walimu, kuendesha na kutoa semina kwa walimu wote Mkoani hapo, kufanya mikutano na viongozi wa Elimu wilaya, kuwa na mpango kazi wa ufatiliaji wa karibu katika ngazi zote, kutoa majaribio yakutosha kwa watahiniwa wote, pamoja na kuwashirikisha wadau wa elimu kuhusu mafanikio yanayo patikana katika Mkoa wa Mwanza.
Mkoa wa Mwanza ambao unatekeleza mpango wa BRN uliowekewa wastani wa ufaulu wa kufikia silimia 70 ya kitaifa hali ambayo imeufanya Mkoa huo kubuni mbinu mbali mbali za kuuwezesha kushika nafasi za juu kitaifa miongoni mwa mikoa 27 ya Tanzania, ambapo 25 kwa Tanzania bara na miwili Tanzania visiwani.
Mbali na matokeo ya kidato cha nne, Sezulu alisema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri ulipo baina ya Walimu, wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe ambao kwa namna moja wameonekana kujituma zaidi katika masomo yao.
Mbali ya matokeo ya kidato cha nne, Mkoa wa Mwanza umeonekana kufanya vizuri katika elimu ya msingi  kwa mwaka wa 2014, kwakuwa katika mtihani wa kumaliza darasa la saba Mkoa ulishika nafasi ya tatu kitaifa kwa kupata ufaulu wa asilimia 69.07 huku ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es Salaam ambao katika matokeo ya darasa la saba ulipata ufaulu wa asilimia 77.94 na Kilimanjaro asilimia 69.08.
Hata hivyo Sezulu amesema wamejizatiti kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika mitihani ya mwaka huu wa 2015 kwa ya Shule ya msingi lakini pia Sekondari
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
WAKUU WAPYA WAWILAYA ZA MKOA WA MWANZA WALIOSIMAMA KWA NYUMA, WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, amewaapisha Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais kwenye viwanja vilivyopo kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
 
Walio apishwa na kupewa majukumu ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Zainab Terack, mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mwajuma Nyiruka na mkuu wa wilaya ya Kwimba Pili Moshi.
 
Akiwaaasa mara baada ya kuapishwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, aliwaambia viongozi hao wapya katika nafasi ya ukuu wa wilaya, waende wakawatumikie wananchi na kwamba huko kwenye wilaya zao kuna viongozi wengine walioko huko waende kujifunza kutoka kwao ili waweze kuwahudumia wananchi. " mimi niowaombe ndugu zangu wakuu wa wilaya wala msiogope huko muendako kuna viongozi wenzenu chukueni muda mjifunze kwao" alisema Mulongo na kuongeza kuwa zipo changamoto kadhaa kwenye wilaya ambazo wamepangiwa ikiwapo ya suala la ulinzi na usalama wameaswa kulipa kipaumbele katika shughuli zao za kila siku lakini wahakikishe pia wanasimamia shughuli za maendeleo .
 
FATILIA HAPA CHINI MATUKIO KATIKA PICHA. 
 
 
SHEHE HASSAN KABEKE AKITOA MAOMBI WAKATI WA SHUGULI YAKUWAAPISHA WAKUU WA WILAYA.


WAKUU WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA, KUTOKA KUSHOTO NI CAREEM YUNUS (MAGU), MANJU SALUM MSAMBYA(ILEMEL), MWAJUMA NYIRUKA(MISUNGWI), BARAKA KONISAGA (NYAMAGANA), PILI MOSHI(KWIMBA), JOSEPH MKIRIKITI (UKEREWE) NA ZAINAB TERACK (SENGEREMA)


MKUU WA WILAYA YA KWIMBA PILI MOSHI AKIPOKEA ZANA ZA KUFANYIA KAZI MARA BAADA YA KUAPISHWA.

MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA ZAINA TELACK AKILA KIAPO MBELE YA MKUU WA MKOA HAYUPO PICHANI SIKU YA TAREHE 25.2.2015 KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA.

BAADHI YA WAGENI WAALIKWA WAKIFATILIA ZOEZI LA KUAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA.


WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA WAKIMPONGEZA MKUU WA WILAYA HIYO BARAKA KONISAGA, BAADA YAKUBAKIZWA KWENYE KITUO HICHO, HAPA NIKATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MKUU MKOA WA MWANZA.

KATIBU WA ALBINO MKOA WA MWANZA NAYE ALIPATA FURSA YAKUTOA NENO KWENYE HAFLA HIYO

BAADHI YA WAGENI WAALIKWA WAKIFATILIA ZOEZI LA KUAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA.