June 2016
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA, AKIFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA CHUO CHA MALIASILI CHA PASIANSI KILICHOPO MKOANI MWANZA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
kuni mkubwa
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akipokea maelezo kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa Madawati kwa mkoa wa Mwanza hususan Jiji la Mwanza.
kuni mkubwa
Mmmoja wa maafisa wa Jiji la Mwanza aliyekutwa eneo la Utengeneza akisimamia zoezi hilo.



kuni mkubwa
Twende nikajionee mwenyewe hatua mliyopiga hadi hivi sasa.


Gari lililokutwa eneo la Buhongwa chuoni likiwa linapakia madawati yaliyo kamilika kwaajili yakupeleka mashuleni.

Na.  Atley Kuni. RS Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amefanya ziara ya kushtukiza katika chuo cha Ufundi Buhongwa kwa lengo la kujionea utengenezaji wa madawati ambapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepiga kambi katika eneo hilo kwa ajili ya madawati ya Wilaya ya Nyamagana.

Ziara hiyo imekuja ikiwa zimesalia siku ishirini na mbili kabla ya tarehe ya mwisho kwa mikoa kukabidhi takwimu za madawati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, ambaye alitoa muda kwamba hadi kufikia tarehe 30, Juni, 2016 kila mkoa uwe umejitosheleza kwa madawati.

Akiwa katika eneo la tukio mkuu wa mkoa amewahimiza watengenezaji hao kuongeza bidii ili ifikapoa tarehe yakuwasilisha wawe wamekamili shughuli hiyo.

“Nadhani  mnafahamu muda umekwenda, ni vema mkaongeza spidi yenu ya utengenezaji ili tuweze kumaliza kwa wakati kama mkoa kisha nasi tuweze kuwasilisha kama jinsi maelezo ya Mhe. Rais yalivyo  elekeza.

Kwa upande wake, mkufunzi katika chuo hicho ameahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kusema kama hali itakwenda vizuri basi kufikia tarehe 20, Juni watakuwa wamekamilisha “Tulikuwa na changamoto ya vyuma hapa katikati lakini hivi sasa tatizo hilo limekwisha na spidi yetu kama mnavyo iona niyakuridhisha”.

Mkoa wa Mwanza wenye mahitaji ya madawati 277,865 kwa takwimu za mwisho kabla yakuanza zoezi hilo ulikuwa unakabiliwa na upungufu wa madawati 168,354. Kukamilika kwa madawati hayo kutauwezesha mkoa kujitosheleza kwa kila shule mtoto kukaa juu ya daati.