Rais Morsi anapingwa kwa kujiongeza mamlaka
Upinzani nchini Misri umebatili kauli yao ya awali ambapo walisema wako tayari kukutana hii leo kujadili wito wa Rais Mohammed Morsi, wa kutaka maauzngumzo kati ya serikali na makundi ya upinzani.
Sasa wanasema hawako tayari kwa mazungumzo hayo huku nchi hiyo ikijiandaa kwa siku nyingine ya maandamano kupinga hatua ya Rais Morsi kujilimbikizia mamlaka.
Taarifa zinazohusiana
Hii ni kufuatia mzozo wa kisisia uliotokea kufuatia uamuzi wa kujipa mamlaka zaidi.
Mmoja wa viongozi wa kisiasa , mkuu wa zamani wa jumuiya ya nchi za kiarabu,Amr Moussa, amesema kuwa wanachotaka ni kuakhirishwa kwa kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba inayotarajiwa kufanywa wiki ijayo.
Waandamanaji wa upinzani nao wameelezea ghadhabu kufuatia tangazo la rais Morsi kuhusu maandamano yao huku mzozo wa kisiasa ukitokota
Msemaji wa upinzani alisema kuwa rais alikosa fursa muhimu ya kihistoria ya kuweza kupatanisha wananchi.
Hali ilikuwa ya mshikemshike waandamanaji wakiapambana na polisi
Makao makuu ya chama cha Muslim Brotherhood ambvacho ndiocho kinaongoza serikali yalishambuliwa mjini Cairo kwa kuteketezwa.
Wananchi walikuwa na hasira kama ilivyotarajiwa tu. Rais naye hakutoa dalili yoyote kuwa yuko tayari kulegeza msimamo wake kuhusu kura ya maoni juu ya rasimu ya katiba ambayo inatarajiwa kufanyika katika muda wa wiki moja ijayo.
Badala yake aliwalaumu wafuasi wa utawala uliopita kwa kufanya maandamano hayo.
Na alisema kuwa walilipia silaha na risasi kwa faida za kifisadi walizopata katika serikali iliyopita.
Axact

Post A Comment: