Articles by "Matukio"
Showing posts with label Matukio. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Serikali mkoani Mwanza imeitaka jamii kote nchini kuwapeleka watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) shule, badala ya kuwanyanyapaa na baadhi kuwaficha ndani na kisha kufifisha ndoto zao za maisha.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
kuni mkubwa
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akipokea maelezo kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa Madawati kwa mkoa wa Mwanza hususan Jiji la Mwanza.
kuni mkubwa
Mmmoja wa maafisa wa Jiji la Mwanza aliyekutwa eneo la Utengeneza akisimamia zoezi hilo.



kuni mkubwa
Twende nikajionee mwenyewe hatua mliyopiga hadi hivi sasa.


Gari lililokutwa eneo la Buhongwa chuoni likiwa linapakia madawati yaliyo kamilika kwaajili yakupeleka mashuleni.

Na.  Atley Kuni. RS Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amefanya ziara ya kushtukiza katika chuo cha Ufundi Buhongwa kwa lengo la kujionea utengenezaji wa madawati ambapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepiga kambi katika eneo hilo kwa ajili ya madawati ya Wilaya ya Nyamagana.

Ziara hiyo imekuja ikiwa zimesalia siku ishirini na mbili kabla ya tarehe ya mwisho kwa mikoa kukabidhi takwimu za madawati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, ambaye alitoa muda kwamba hadi kufikia tarehe 30, Juni, 2016 kila mkoa uwe umejitosheleza kwa madawati.

Akiwa katika eneo la tukio mkuu wa mkoa amewahimiza watengenezaji hao kuongeza bidii ili ifikapoa tarehe yakuwasilisha wawe wamekamili shughuli hiyo.

“Nadhani  mnafahamu muda umekwenda, ni vema mkaongeza spidi yenu ya utengenezaji ili tuweze kumaliza kwa wakati kama mkoa kisha nasi tuweze kuwasilisha kama jinsi maelezo ya Mhe. Rais yalivyo  elekeza.

Kwa upande wake, mkufunzi katika chuo hicho ameahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kusema kama hali itakwenda vizuri basi kufikia tarehe 20, Juni watakuwa wamekamilisha “Tulikuwa na changamoto ya vyuma hapa katikati lakini hivi sasa tatizo hilo limekwisha na spidi yetu kama mnavyo iona niyakuridhisha”.

Mkoa wa Mwanza wenye mahitaji ya madawati 277,865 kwa takwimu za mwisho kabla yakuanza zoezi hilo ulikuwa unakabiliwa na upungufu wa madawati 168,354. Kukamilika kwa madawati hayo kutauwezesha mkoa kujitosheleza kwa kila shule mtoto kukaa juu ya daati.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha na OMR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini nyaraka wakati wa hafla fupi ya kumwapisha, George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi nyaraka za Serikali, George Mcheche, baada ya kumwapisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kutoka kulia) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makindajaji Mkuu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othuman, Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche, aliyeteuliwa, wakiwa katia ukumbi wakisubiri zoezi hilo la kuapishwa. Picha na OMR
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na viongozi wa ngazi za juu.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wakuu wa Ulinzi na usalama.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na wanafamilia wa Bw. George.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
Picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi Tume ya Sheria.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akisubiri kuapishwa, George Mcheche, akizungumza jambo na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakati wa hafl hiyo.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

. Yazipiku Nyamagana, Ilemela.

. Yafaulisha kwa asilimia 78.9

. Magu yaing'ang'ania nafasi ya tatu.

KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, DK. FAISAL ISSA ALIPOKUWA AKIFUNGUA KIKAO HICHO CHA KUTANGAZA MATOKEO.
Wilaya ya Ukerewe imeibuka kidedea katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2014 na kuzipiku wilaya za Nyamagana na Ilemela ambazo mwaka 2013 zilishika namba moja na mbili ambazo zilifikia ufaulu wa asilimia 74.6 kwa Nyamagana na Ilemela iliyo faulisha kwa asilimia 71.3, hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu wa 2014 ambapo wilaya ya Ukerewe iliyongoza, imefikia asilimia 78.9  na kuzidi ufaulu wa mwaka 2013 wa  Nyamagana iliyopata asilimia 77.2 na Ilemela asilimia 72.2 na kufanikiwa kuwa namba moja.
 
Wakati huo huo Ilemela imezidiwa na Wilaya ya Magu iliyoshika nafasi ya tatu kwa mwaka huu na kuisukuma Ilemela hadi nafasi ya nne na kuizidi kwa kupata asilimia 75.5 hali inayo chagiza  kuwa huenda kama kasi hiyo itaendelea basi zipo dalili za wazi kuwa Wilaya za pembezoni mwa mji kuongoza katika miaka ijayo na Wilaya za mjini kushushwa katika suala la ufaulu.
Akitangaza matokeo hayo ya darasa la saba kwenye sekondari ya Mwanza hivi karibuni, Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwalimu Hamis Maulid, alisema "Tarehe 10/9/2014 na  11/9/2014 mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi ulifanyika hapa nchini.  Mkoa wa Mwanza ulishiriki katika zoezi hilo,  na jumla ya wanafunzi 54384 walitarajiwa kufanya mtihani huo, kati yao wavulana walikuwa 25889 na wasichana ni 28495 anasema Wanafunzi wote hawa ni kutoka katika jumla ya shule za msingi 891 zilizoshiriki mtihani huo" anasema Maulid na kuongeza kuwa, mbali ya Wilaya ya Ukerewe kuwa na ufaulu mzuri lakini pia imesaidia kuinua ufaulu wa mkoa  mzima wa Mwanza ambao uko chini ya mpango wa Tekeleza sasa kwa matokeo makubwa (BRN) na kuifikia wastan wa asilimia 69.07 kutoka asilimia 57.9 za mwaka 2013 ongezeko la zaidi ya asilimia 10 ambalo sasa linakaribia tarajio la BRN la mwaka 2014 la ufaulu wa asilimia 72. hata hivyo mkoa unabakia katika kibarua kigumu cha kufikisha ufaulu wa asilimia 82 kwa mwaka ujao wa 2015
 
Mbali ya ufaulu huo mkoa pia umeweza kushika nafasi ya 3 kitaifa katika mikoa 25 na umefanikiwa kuingiza shule  19 bora kati ya  shule bora 100, huku shule ya Mugini iliyopo Wilayani magu ya  ikishika nafasi ya pili kitaifa na  ya kwanza kimkoa.
 
AFISA ELIMU MKOA AKIJADILIANA JAMBO NA
KATIBU TAWALA MKOA WAKATI WAKUTANGAZA MATOKEO HAYO.
Maulid pia anasema "Waliofanya mtihani huo kwa mwaka 2014 ni wanafunzi 53597 wakiwemo wavulana 25484 na wasichana 28113  sawa na asilimia  98.5  ya Wanafunzi   waliofanya mtihani huo amabao walianza darasa la kwanza mwaka 2008  wakiwa jumla  ya wanafunzi 72054    kati yao wavulana 35262  na wasichana  36792  Kwa hiyo waliofanya mtihani huu ni sawa na asilimia 74.4 ya wanafunzi wote walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2008". anasema Maulid.
 
Aidha Maulid, alibainisha kwamba ,wanafunzi ambao hawakuweza kufanya mtihani kwa mwaka huo wa 2014 ni kama ifuatanvyo, alisema  "Kati ya wanafunzi 54384  waliotarajiwa kufanya mtihani huo, wanafunzi 787  hawakufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za utoro, kifo, ugonjwa, kuhama, na mimba kwa wasichana. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 1.46".
 
 
BAADHI YA WATENDAJI KUTOKA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MWANZA  WAKIFATILIA UTANGAZAJI MATOKEO KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWANZA.
 
AFISA ELIMU  MSINGI WILAYA YA UKERWE FIDES MUNYOGWA AKIELEZA SIRI YAKUFANIKIWA HADI KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KIMKOA.
Kwa upande wake Afisa Elimu msingi wa Wilaya ya Ukerewe, bibi Fides Munyogwa ,amesema siri kubwa yakupata ufaulu ulio iwezesha wilaya kushika nafasi ya kwanza kimkoa ni pamoja na ushirikiano baina ya walimu, wazazi pamoja na uongozi mzuri wa wilaya, lakini pia kutatuliwa kwa changamoto ya madai ya walimu waliokuwa wakiidai wilaya hiyo.
Aidha mazoezi ya mara kwa mara pia yamechagiza katika kupata ufaulu huo " Mwenyekiti sisi Wilaya ya Ukerewe tumefanikiwa kulipa madeni ya walimu kwa kutumia fedha za ndani na kuawafanya walimu waliokuwa wanadai waweze kuifanya kazi yao kwa moyo" anabainisha bibi Munyogwa.
   Imeandaliwa na Afisa Habari. Mwanza RS. 

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amekutana na viongozi wa dini pamoja watendaji wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili yakuzungumzia suala la maendeleo ya Mkoa huo na wa kwanza kukutana nao walikuwa watendaji wa Sekretarieti Mkoa na badaye jioni viongozi wa dini.
 
·        Awapa rungu watendaji, awaambia wasifanye kazi kwa mazoea.

·        Viongozi wa Dini wakerwa na Uchawi, Ukame, na hali duni katika zao la Pamba.

·        “Vijana wengi wana ndoto za kuhamia  Mwanza kuwa Machinga”- Askofu AIC asema.
 

 

SHEKHE HASSAN FEREJI WA MKOA WA MWANZA AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO KILICHO WAKUTANISHA VIONGOZI WA DINI NA MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIFUNGUA KIKAO NA VIONGOZI WA DINI MKOANI HAPA.

VIONGOZI WA DINI WAKIFURAHIA JAMBO, ANAYE PIGA MAKOFI NI KIONGOZI WA KANISA LA SDA, AITWAE BULENGELA. KUTOKA DAYOSISI YA NYANZA


ASKOFU ANDREW GULLE WA KKKT DAYOSISI YA MASHARIKI YA ZIWA VIKTORIA AKICHANGIA MADA KATIKA KIKAO HICHO.

KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA ALIYE SIMAMA FAISAL ISSA AKIWA ANATOA MUONGOZO JUU YAKUCHANGIA KATIKA KIKAO HICHO.





Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rsmi Kivuko cha Tegemeo tayari kuanza kufanya safari zake kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza leo, Septemba 26, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya viongozi. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza Kitufye kuashiria uzinduzi  rasmi wa Kivuko cha Tegemeo tayari kuanza kufanya safari zake kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza leo, Septemba 26, 2014. Kuhoto  kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya viongozi. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala Ufundi wa Umeme-TEMESA, Eng. Mseline Magesa, wakati alipokuwa akikagua Kivuko cha Tegemeo baada ya kukizindua rasmi leo Septemba 26, 2014 kwa ajili ya kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala Ufundi wa Umeme-TEMESA, Eng. Mseline Magesa, wakati alipokuwa akikagua Kivuko cha Tegemeo baada ya kukizindua rasmi leo Septemba 26, 2014 kwa ajili ya kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati akikagua Kivuko hicho. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Kahunda Wilaya ya Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika leo, Septemba 26, 2014. Picha na OMR

Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Uzinduzi huo alipiga picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi waliokuwa wamehudhuria katika hafala hiyo

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Waziri Sitta akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Bunge la Bajeti jana linaloendelea Jijini Dodoma.


Waziri Sitta pamoja na Naibu wake Mhe. Abdulla Juma Abdulla wakifuatilia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ushirikiano jana Bungeni Dodoma.


Baadhi ya Wabunge wa EALA wakifuatilia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano jana Bungeni Dodoma


Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Abdulla Juma Abdulla akijibu hoja za wabunge kuhusu Wizara yake wakati wa uwasilishaji bajeti jana Bungeni Dodoma


Uongozi wa Wizara ya Ushirikiano katika picha ya pamoja mara baaada ya kupitishwa kwa Bajeti yao.
(Picha zote na Maelezo na: Ofisa habari wa Wizara hiyo Antony Ishengoma)

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda mjini Mombasa pwani ya Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya Jumapili na kuwapiga risasi waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo amefikishwa Nairobi mwa matibabu maalum.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
Idadi ya waliofariki kufuatia shambulio la Likoni imeongezeka na kufikia 6 huku 9 waliokua wakipokea matibabu wameruhusiwa kurudi nyumbani na 6 hao walifariki kufuatia majeraha ya risasi,Polisi nchini Kenya imesema bado hawajafutilia mbali uwezekano wa kuwa lilikua shambulio la kigaidi.

Mwandishi wa habari kutoka Dw nchini  Kenya anaelezea kwa sasa kinachoendelea Mombasa>>’Hali ilivyo mjini Mombasa ni hali ya kutatanisha kukosekana kwa usalama kwa sababu kama unavyojua tukio hili  limezua hofu sana hasa kwa wakazi wa mji huu wa Mombasa’

‘Nakumbuka tukio la watu 5 waliuwawa kwenye kanisa moja hapa Likonyi ni kitendo kilichotokea siku 2 baada ya Waziri wa usalama kutoa taarifa kwa wakazi wa hapa kuwa usalama utadumishwa’

‘Hali ni tete hapa Mjini Mombasa baada ya tukio hilo ambalo watu hao waliuwawa msako wa polisi uliendelea kuimarishwa kuanzia saa 8 na msako huo uliendelea usiku kucha na taarifa tulizopokea kwa sasa ni kwamba watu 59 wametiwa nguvuni’

‘Wasiwasi upo kwa sababu hiki ni kitendo kilichotengenezwa ndani ya kanisa na unajua si mara ya kwanza kitendo hiko kutokea hapa Mombasa nakumbuka fujo zilizozuka baada ya kitendo cha ugaidi kutokea hapa Mombasa kuliokua na taharuki miongoni mwa wakazi wake hasa baina ya wakristo na waislam’

‘Hiki ni kitendo ambacho watu wanahofia kimetekelezwa kuzua hofu hasa miongoni mwa waumini wa dini hizo mbili lakini viongozi wa kidini wamekuja pamoja na kusema kwamba hiki ni kitendo kilichofanywa na magaidi tu ili kuzua mtafaruku miongoni mwa waumini baina ya wakristo na waislam hilo ni tukio linaloendelea kuchunguzwa’

‘Hadi kufikia sasa hakujawa na taarifa za kuthibitisha kitendo hiki kilitekelezwa kwa malengo gani na wakina nani hasa,hali ya wasiwasi mjini Mombasa bado ipo na kama unakumbuka kuwa tukio hili limetokea siku chache baada ya watu wawili kukamatwa wakiwa na mabomu Mabomu ambayo yaliharibiwa hivi juzi tu kwa hivyo ni tukio linalozidi kutia hofu kwa wakazi wa Mombasa’.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
KATIBU WA UENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NAPE MNAWIYE, AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MSIMAMO WA CHAMA, HII NI BAADA YA HOTUBA YA JAJI WARIOBA ALIYO ITOA TAREHE 18.3.2014.

Tarehe  18/03/2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha kwenye Bunge maalum la Katiba rasimu ya pili ya katiba.

Toka awasilishe rasimu ile bungeni , kumekuwa na maombi mengi sana ya kutaka kujua kama msimamo wa CCM juu ya baadhi ya mambo hasa muundo wa muungano bado ni uleule.

Kwasababu ya maombi hayo CCM imeona bora kueleza kwa mara nyingine tena msimamo na imani ya CCM juu ya swala zima la Muungano na muundo wake.

Kimsingi CCM ndio waasisi wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar. CCM inamasilahi makubwa na mapana na Muungano huu kama waasisi pengine kuliko taasisi nyingi ndani na nje ya nchi yetu.

Bado CCM inaamini changamoto za Muungano huu suluhisho lake sio kubadili muundo wa Muungano bali ni kuufanyia maboresho muundo wa muungano tulionao wa serikali mbili. Hivyo basi CCM bado inaamini muundo bora kwasasa utakao dumisha muungano wetu ni muundo wa SERIKALI MBILI.

Kwakuwa kazi ya Warioba na Tume yake sasa imekwisha rasmi, kuisha kwa kazi yao ni mwanzo wa awamu nyingine ya mchakato huu. Mwisho wa kazi ya Tume sio mwisho wa mjadala juu ya Katiba tuitakayo bali ni mwanzo wa awamu nyingine ya mjadala mpana na maboresho kama sio marekebisho ya kuondoa mapungufu kwenye rasimu iliyowasilishwa.

Mwanzo wa awamu hii nyingine ni furusa nzuri ya kupima kama kweli yaliyomo kwenye rasimu na maelezo ya ziada yaliyotolewa na Jaji Warioba yana akisi maoni ya Watanzania walio wengi.

CCM ina amini awamu mbili zilizobaki kwakuwa zinahusisha wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge maalum la Katiba, na hatimaye itawahusisha wananchi wenyewe moja kwa moja kupitia kura yao, zitatumika vizuri kutupa ni nini hasa matakwa ya Watanzania juu ya Katiba waitakayo na sio maoni au matakwa ya wachache.

Wakati haya yote yakiendelea CCM bado tunaamini Muungano huu ni muhimu ukadumishwa na kuimarishwa. CCM tunaaamini ili Muungano huu udumu njia pekee kwasasa ni kufanya marekebisho kwenye Muundo wa serikali mbili ili ujibu vizuri zaidi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kukidhi mazingira ya sasa.

Tunawaomba wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi hiki. Ni vizuri Watanzania tukavumiliana,tukashindana kwa hoja tukitanguliza mbele uzalendo na masilahi ya kweli ya nchi yetu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
20/03/2014

(MM)
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Sudan, waasi wapewa siku 10 kuanza mazungumzo.  

Thabo Mbeki.
   
Thabo Mbeki, mkuu wa kamati ya upatanishi ya Umoja wa Afrika katika mgogoro wa Sudan  
ametangaza kuwa, umoja huo umeipa serikali na waasi wa nchi hiyo muda wa siku 10. Sambamba na kuashiria kusimamia mazungumzo kati ya serikali ya Khartoum na waasi yaliyokuwa yakifanyika kwa lengo la kuhitimisha vita katika eneo la Kordofan na Blue Nile, Umoja wa Afrika umezipa pande mbili hizo hasimu muda wa hadi siku 10 ili kuanza tena mazungumzo hayo. Akielezea sababu za kusimama mazungumzo hayo, Mbeki amesema kuwa mazungumzo hayo yamesimama kutokana na Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Sudan, tawi la kaskazini (SPLM-N) kusisitiza kufikiwa makubaliano kuhusu masuala yote, huku upande wa serikali ukisisitiza kufikiwa tu makubaliano juu ya maeneo ya Kordofan na Blue Nile.
Tangu mwaka 2011 maeneo ya Kordofan kusini na Blue Nile ya kusini mwa Sudan yamekuwa yakishuhudia mapigano kati ya waasi wa harakati ya SPLM kaskazini na serikali ya Khartoum.


 



Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kati ya mambo ambayo yamewahi kuwashangaza watu katika ulimwengu wa jumuiya ya Kikristo, ni hatua ya mchungaji Jamie Coots wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus Name, ambaye alikuwa akihubiri kwa kutumia nyoka, na kusema kuwa kuna ukombozi kupitia nyoka huyo.


Siku zimeenda naye akaendeleza injili hiyo ya nyoka, ambapo mwisho wa siku ameripotiwa kufariki baada ya kung'atwa na nyoka akiwa madhabahuni kanisani kwake.

Siku zimeenda naye akaendeleza injili hiyo ya nyoka, ambapo mwisho wa siku ameripotiwa kufariki baada ya kung'atwa na nyoka akiwa madhabahuni kanisani kwake.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea siku ya Jumamosi, ambapo alikuwa akihubniri madhabahuni, kabla ya nyoka kumng'ata, jambo ambalo alilichukulia kawaida na kukataa kwenda hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Mkuu wa polisi wa Middlesboro, eneo ambalo mchungaji huyo alikuwa akiishi, Jeff Sharpe, amesema kuwa mchungaji Coots alifariki kwenye majira ya saa nne usiku baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwake, ambapo aliondoka kanisani punde tu kabla ya watu wa huduma ya kwanza kufika kwa ajili ya kumhudumia na kumkosa mida ya saa mbili na nusu usiku - kisha wakanyookea nyumbani kwake ili kumpatia huduma, ambapo aliwakataliwa - nao wakaondoka maeneo hayo majira ya saa tatu na dakika kumi usiku.



video inayoonesha namna alivyokua akifanya ibada zake ni hii hapa chini.

Mara baada ya kuondoka, baadae walipokea siku kuwa mchungaji Coots amefariki dunia nyumbani kwake kutokana na sumu ya nyoka ambaye alimng'ata kwenye mkono wake wa kulia.

Mchungaji Coots ambaye amezaliwa mwaka 1971, amewahi kunusurika kufariki mara mbili, ambapo mwaka 1990 na 1998 aliwahi kuumwa na nyoka kwa nyakati tofauti, kwenye mkono wa kushoto na pia kwenye kidole cha kati cha mkono wa kulia, ambapo mara zote hizo alikataa msaada wa kitabibu.

Mwaka 1995, Bi Melinda Brown wa Parrotsville alifariki dunia baada ya kuumwa na nyoka kwenye kanisa la mchungaji Coots, ambapo polisi waliamua kumfungulia mashtaka Coots, hadi pale jaji alipotoa hukumu kumuachia huru, akitaka asisumbuliwe kutokana na imani yake.

Swali hapa mtaani ni kwamba, baada ya kufariki huyu mchungaji sijui ndo ameenda kwa nyoka ama wapi, anasikika akisema kijana mmoja mtaani.

Mchungaji Coots amekuwa akiendesha vipindi kupitia kituo cha runinga cha National Geographic, kiitwacho Snake Salvation, ambao wametoa tamko siku ya Jumapili la kusikitishwa na kifo cha mchungaji huyo, huku

 ukiwa umeshapata wadau (likes) zaidi ya 1,600 ambapo michango imekuwa ikiombwa kwa maelezo kuwa mchungaji huyo hakuwa na bima katika huduma yake hiyo.

Credits:gospel kitaa blog
   
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
 
Hatimaye Magari madogo ya usafiri wa abiria katika  jiji la Mwanza hivi leo yamerejea  bara barani mara baada yakusababisha adha kwa wasafiri kwa siku nzima ya Jumatatu ya tarehe 17.2.2014.
 
Katika pita pita zetu na ufatiliaji wa karibu hivi leo Mtandao wa kuninews umeshuhudia idadi kubwa ya magari yakiendelea na shughuli kama kawaida.
 
Katika siku ya jana kulizuka kizaa zaa mara baada ya watoa huduma hao wakiongozwa na madereva na makondakta kugoma kwa takriba ni saa 12 na kusababisha adha kubwa kwa abiria waliokuwa wanasafiri kuingia katikati ya Jiji.
 
Wafanyakazi, wafanya Biashara siku ya jana walilazimika kutembea kwa Miguu, kupanda katika malori na Bajaji za Mizigo, kutoka katika sehemu mbali mbali za Viunga vya jiji hilo.
 
Hata hivyo kutokana na madai ya Msingi yaliyokuwa yakilalamikiwa na Watoa huduma hao ni  kuongezwa  kwa Upana wa Vituo vya Dala dala vya maeneo ya Buzuluga na Natta, wakidai kutokuwa na upana unao kidhi mahitaji yao yamepokelewa na Mhandisi wa bara bara Mkoa wa Mwanza TANROAD Eng. Leonard Kadashi ambapo aliwaeleza waandishi wa habari hapo jana kwamba, madai yao yamepokelewa na yatapitiwa ili kuona mapungufu yaliyopo.
 
Katika hatua nyingine wamiliki hao wamedai kwamba mgomo huo pamoja na kwamba ulitendeka lakini ulikuwa hauna Baraka za wamiliki wa Magari na badala yake ilikuwa ni mawazo ya Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la  Dede na kwamba wamiliki hao walikana kumuunga mkono katika sakata hilo.
 
"Huyu mtu.. anayeitwa Dede amelala nyumbani kwake na mke wake anagomesha watu bila hata kutushirikisha sisi wamiliki wa Magari" alisikika mwananchi mmoja akisema mbele ya waandishi wa habari hapo jana.
 
Mkoa wa Mwanza katika siku za hivi karibuni umekumbwa na migomo isiyokuwa na tija wala manufaa kwa  maendeleo ya  mkoa, kwani, siku moja kabla ya Kongamano la uwekezaji la kanda ya Ziwa lililo shirikisha Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Simiyu, na Kagera. Wafanya biashara walishiriki mgomo kwa siku tatu wakigomea mashine za EFD zinazo uzwa na wkala wa TRA kwa ajili ya ulipaji kodi.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


KUFA KUFAANA, HAPA GARI HILI LA MIZIGO LILIGEUKA KUWA LA ABIRIA.



Bajaji leo inafanya kazi ya kusafirisha abiria badala ya Mizigo.


Madereva hapa walikutwa nje ya Ofis ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.


Mama huyu alilazimika kulipa kiasi cha Tshs 5000/= kwa safari ya Mjini kati hadi uwanja wa ndege, kwa kawaida nauli ya daladala ni sh. 400.


Mama hapa akiwa na Wanawe akiwa anapatana Bei ya kusafiri kwa Pikipiki kati ya Mjini kati Eneo la Idara ya maji kwenda Uwanja wa Ndege Mwanza.


Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Jiji Mwanza akizungumza na Bw. Ashirafu Mmoja ya madereva waliogoma.

 
Hapa tunalazimika kufanya kazi kwa kificho, maana tumewasiliti wenzetu.

 
·         Safari hii ni wenye dala dala.

·         Walalamikia Udogo wa Vituo vya daladala na Faini kubwa kwakukiuka taratibu.

Katika hali inayo onekana kuendelea kwa migomo katika Jiji la Mwanza, na habari ambazo ni (habari mpasuko) zinazo tufikia hivi sasa, wenye daladala katika Jiji la Mwanza wamegoma kutoa huduma katikati ya Jiji hilo huku wakishinikiza Mamlaka husika kuchukua hatua za haraka ili kuondoa tatizo lililopo.

Mwandishi wetu ameshuhudia misafara ya watu, wakitembea kwa miguu kutoka viunga mbali mbali vya Jiji hilo, Barabara bara ambazo zimeoneka kuwa na watu wengi ni ile itokayo maeneo ya Nyakato, Igoma, kuingia Jijini humo maarufu kwa jina la “Nyerereroad”, barabara nyingine zingine ni ile itokayo Nyegezi na maeneo ya Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino kuingia Jiji humo ijulikanayo kwa Jina la “Kenyatta road”na Baraba iliyo shuhudiwa kuwa na misafara ya watu wengi ni pamoja na ile itokayo Airport kuingia katikati ya Jiji maarufu kwa jina la “Makongoro road”.

Katika kutaka kujua kulikoni, mwananchi mmoja aliye fahamika kwa jina la Antony Mkaima, ameuambia mtandao wa kuninews.blogspot.com kuwa, chanzo kikuu cha mgomo huo, ni eneo dogo la kituo ambalo daladala hizo zimetengewa katika eneo la Igoma na hivyo kufanya msongamano mkubwa ambao huwalazimisha madereva wa daladala kuvunja sheria za usalama bara barani ikiwa ni pamoja na kuegesha magari bila utaratibu katika eneo hilo na pindi wanapovunja taratibu hizo za usalama barabarani hutozwa tozo ya shilingi za kitanzania Elfu sitini (60,000/=), jambo ambalo limepingwa na wamiliki wa vyombo hivyo wakidai ni kutowatendea haki, Na kuzitaka mamlaka husika kuweka mazingira mazuri ya kuegesha magari yao kwa nafasi ndipo waweze kuendelea na kutoa huduma hiyo muhimu kwa wananchi la si sivyo wataendelea na mgomo huo.

Kugoma kwa daladala huko, kumetoa mwanya kwa magari madogo yasiyo rasmi kwa abiria, Bajaji za Mizigo, Pikipiki kutumika kama njia mbadala ya usafiri, jambo ambalo imeonekana kuwa hatari, kwani vyombo hivyo si rasmi kwakubeba abiria lakini pia weledi wa madereva wa vyombo hivyo bado si wakutumainiwa kwani baadhi yao hawana Leseni zinazo waruhusu kuendesha abiria.

Katika siku za hivi karibuni Jiji la Mwanza limekuwa likikubwa na migomo ya mara kwa mara, huku mgomo mwingine ukiwa ni ule ulio wahusisha baadhi ya wafanya biashara wa jumla katika Jiji hilo ambapo waligoma wakishinikiza Serikali kuangalia upya matumizi ya mashine za kielektroniki katika ulipaji wa kodi.

Juhudi za kuwapata mamlaka ya usafiri wan chi kavu na majini SUMATRA zinaendelea na pindi tutakapo zungumza nao tutawapatieni kilicho jiri na hatua madhubuti zilizo chukuliwa katika kumaliza mgomo huo

Jiji la Mwanza linalokuwa kwa kasi miongoni mwa miji iliyoko kusini mwa  jangwa la Sahara, ambao kwa hivi sasa unakadiriwa kuwa na watu Mil. 2.7, pamoja na shughuli zingine za kilimo, Uvuvi, Madini na Viwanda suala la Biashara ni moja ya sekta muhimu kwa uchumi wa Mkoa huo wa pili katika kuchangia pato la taifa, kwani kwa mujibu wa takwimu Mkoa huo kwa sasa huchangia kiasi cha asilimia  9.15 kwa mwaka 2012 ukitanguliwa na Dar es salaam ambao ulichangia kwa asilimia 16.93.

Kutokana na hali hiyo wadadisi wa mambo wanasema migomo kama hiyo huenda kwa namna moja au nyingine ikasababisha kushuka kwa uchumi wa Mkoa kwani shughuli nyingi za uzalishaji mali zitakwama na hivyo kuathiri hata ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa.

Imeandaliwa na Atley Kuni - Afisa habari Mkoa wa Mwanza.