Articles by "Afrika Mashariki"
Showing posts with label Afrika Mashariki. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 


RAIS WA KENYA UHURU MWIGAE KINYATTA
Mauaji ya Mpeketoni yemesababisha vifo vya watu zaidi ya hamsini
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja kupitia kwa televisheni siku moja baada ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku.
Kenyatta emesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema na kwamba wanasiasa walihusika nao.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu jioni.
Alisema kuwa ujasusi ulitolewa kuwa mashambulizi hayo yangefanyika lakini hawakuchukua hatua zozote kuzuia mashambulizi hayo.
Rais amesema kuwa maafisa waliohusika tayari wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa. Amesema kuwa kwa sasa wanachunguza wanasiasa waliohusika na mauaji hayo ili sharia iweze kuchukua mkondo wake.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa jamii.
 
Hata hivyo Kenya katika siku za hivi karibuni imekuwa katika hali tete ya mashambulio ya kigaidi likiwepo shambulio kubwa lililowahi kutokea katika Jengo kubwa la Westgate la Jiji Nairobi na kusababisha vifo vya watu kadhaa na mamia wengi kujeruhiwa.
 
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema kipigo wanachokipata nchi hiyo ni kutokana na kupeleka wanajeshi wake Nchini Somalia kwa ajili ya kukabiliana na makundi ya kigaidi
 
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Waziri Sitta akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Bunge la Bajeti jana linaloendelea Jijini Dodoma.


Waziri Sitta pamoja na Naibu wake Mhe. Abdulla Juma Abdulla wakifuatilia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ushirikiano jana Bungeni Dodoma.


Baadhi ya Wabunge wa EALA wakifuatilia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano jana Bungeni Dodoma


Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Abdulla Juma Abdulla akijibu hoja za wabunge kuhusu Wizara yake wakati wa uwasilishaji bajeti jana Bungeni Dodoma


Uongozi wa Wizara ya Ushirikiano katika picha ya pamoja mara baaada ya kupitishwa kwa Bajeti yao.
(Picha zote na Maelezo na: Ofisa habari wa Wizara hiyo Antony Ishengoma)

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.(Hudugu Ng,amilo)


Picha za Filamu zilizonaswa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila ya kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hawana virusi vinavyosababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda, Kampala zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
BBC ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda, ushahidi huo, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashitaki wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia.
IMERIPOTIWA NA  BBC
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
MHE. BERNAD MEMBE WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA.
Serikali ya Tanzania itafanya mazungumzo na Rwanda ili "kutatua tofauti za kisiasa kuhusu mgogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti Alhamisi (tarehe 27 Machi).
 
Mazungumzo rasmi yanakusudiwa kuondoa kile Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe alichokiita "vita ya kimaandishi" kilichosukumwa na propaganda ya vyombo vya habari.
 
"Mazungumzo hayo rasmi yatakuwa ndiyo mwanzo," alisema Membe, akiongeza kwamba watarejesha imani kati ya nchi hizo mbili.Membe alikariri kwamba kwa wajibu wa Tanzania katika mgogoro huo uliopo nchini  DRC ni kwa ajili ya jitihada za kuleta amani tu chini ya umoja wa mataifa.  wajibu wa Tanzania katika mgogoro uliopo nchini DRC ni kwa ajili tu ya jitihada za kuleta amani tu chini ya Umoja wa Mataifa.
 
"Kwa mujibu wa ujumbe wetu ulioko huko Goma [mashariki mwa DRC], amani hatimaye inarejea katika eneo hilo na vijana wetu wataendelea kuwa kule kwa mwaka mmoja hadi amani itakaporejea kikamilifu," alisema Membe.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda mjini Mombasa pwani ya Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya Jumapili na kuwapiga risasi waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo amefikishwa Nairobi mwa matibabu maalum.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
Idadi ya waliofariki kufuatia shambulio la Likoni imeongezeka na kufikia 6 huku 9 waliokua wakipokea matibabu wameruhusiwa kurudi nyumbani na 6 hao walifariki kufuatia majeraha ya risasi,Polisi nchini Kenya imesema bado hawajafutilia mbali uwezekano wa kuwa lilikua shambulio la kigaidi.

Mwandishi wa habari kutoka Dw nchini  Kenya anaelezea kwa sasa kinachoendelea Mombasa>>’Hali ilivyo mjini Mombasa ni hali ya kutatanisha kukosekana kwa usalama kwa sababu kama unavyojua tukio hili  limezua hofu sana hasa kwa wakazi wa mji huu wa Mombasa’

‘Nakumbuka tukio la watu 5 waliuwawa kwenye kanisa moja hapa Likonyi ni kitendo kilichotokea siku 2 baada ya Waziri wa usalama kutoa taarifa kwa wakazi wa hapa kuwa usalama utadumishwa’

‘Hali ni tete hapa Mjini Mombasa baada ya tukio hilo ambalo watu hao waliuwawa msako wa polisi uliendelea kuimarishwa kuanzia saa 8 na msako huo uliendelea usiku kucha na taarifa tulizopokea kwa sasa ni kwamba watu 59 wametiwa nguvuni’

‘Wasiwasi upo kwa sababu hiki ni kitendo kilichotengenezwa ndani ya kanisa na unajua si mara ya kwanza kitendo hiko kutokea hapa Mombasa nakumbuka fujo zilizozuka baada ya kitendo cha ugaidi kutokea hapa Mombasa kuliokua na taharuki miongoni mwa wakazi wake hasa baina ya wakristo na waislam’

‘Hiki ni kitendo ambacho watu wanahofia kimetekelezwa kuzua hofu hasa miongoni mwa waumini wa dini hizo mbili lakini viongozi wa kidini wamekuja pamoja na kusema kwamba hiki ni kitendo kilichofanywa na magaidi tu ili kuzua mtafaruku miongoni mwa waumini baina ya wakristo na waislam hilo ni tukio linaloendelea kuchunguzwa’

‘Hadi kufikia sasa hakujawa na taarifa za kuthibitisha kitendo hiki kilitekelezwa kwa malengo gani na wakina nani hasa,hali ya wasiwasi mjini Mombasa bado ipo na kama unakumbuka kuwa tukio hili limetokea siku chache baada ya watu wawili kukamatwa wakiwa na mabomu Mabomu ambayo yaliharibiwa hivi juzi tu kwa hivyo ni tukio linalozidi kutia hofu kwa wakazi wa Mombasa’.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
HII NI MOJA YA MIKUSANYIKO YA WATU KUSIKILIZA NENO LA MUNGU.
Polisi wa Kenya na viongozi wa dini wanashirikiana kuzuia kuenea kwa itikadi za imani kali katika mikusanyiko ya umma inayoandaliwa na wahubiri wa Kikristo na Kiislamu.
Katika mikusanyiko hiyo, ambayo ni ya kawaida kando ya mitaa na katika masoko ya wazi nchini Kenya, wahubiri wanalenga kuwaelimisha wafuasi wao na kuwabadili dini watu wa imani nyingine. Mikusanyiko ya Wakristo inajulikana nchini kama "crusades" wakati mikusanyiko ya Waislamu inajulikana kama "muhadara".
Lakini hivi karibuni, mikusanyiko kama hiyo imekuwa chanzo cha hamaki na hotuba za uchochezi ambazo zimechokoza mivutano ya madhehebu.
Ingawa uhuru wa kujumuika, kuabudu na kukusanyika umewekwa katika katiba ya Kenya, Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo alisema kwamba baadhi ya mikusanyiko inaweza kuchochea kiurahisi mvutano na vurugu za kidini.
"Tunao waumini wenye imani kali kutoka katika Ukristo, Uislamu na hata katika Uhindi ambao wanaweza kujibu kwa vurugu kama wataona kwamba dini yao inashambuliwa," aliiambia mtandao huu.
"Hatuna tatizo lolote na wakusanyikaji katika mikusanyiko hiyo kwa kuwa wanajaribu kueneza dini yao na katika hatua hiyo wanapata roho chache zinazobadili dini kuingia katika dini yao," Kimaiyo alisema. "Lakini katika wakati ambayo nchi iko katika uchungu wa mashanbulizi ya al-Shabaab, tuna wasiwasi kwamba baadhi ya mikusanyiko inaweza kusaidia tu kuchochea uhasama wa kidini."

'Hali tete ya usalama' hatarini.

"Kitu tunachowaomba tu kutoka kwa wanaokutana katika mikusanyiko hiyo ni kuzingatia hali tete ya usalama wa nchi na kuepuka kutovumiliana dhidi ya dini nyingine," alisema.
Baadhi ya viongozi wa mikusanyiko hiyo huko Nairobi, Garissa, Wajir na Mombasa wako katika uchunguzi wa polisi ili kufuatilia hotuba zao na sheria, Kimayo alisema. "Tumezungumza na wakusanyikaji kadhaa kutoka katika imani zote mbili na wamekubali kupunguza," alisema.
Kama umoja, amani na utulivu vinatishiwa, Kimaiyo alisema, polisi itapiga marufuku mikusanyiko yote ya dini, maandiko, hotuba na vitu vingine vinavyoonekana kuleta uchochezi.
Upigaji marufuku wa kudumu wa mikusanyiko hiyo tayari umeshafanyika katika Kaunti ya Mombasa kufuatia msururu wa matukio ya vurugu yaliyochochewa na mauaji ya wahubiri wa dini.
Kaimu Kamanda wa kaunti ya Mombasa Tom Okoth aliiambia Sabahi kaunti iliweka marufuku hiyo tarehe 4 Februari baada ya uchunguzi kugundua kwamba mikusanyiko inaweza kuleta vita ya kidini na kuchochea vurugu. Wafuasi wa mikusanyiko wana tabia ya kubeza imani ya wengine na kuchukuliana kama mahasimu, alisema.
"Kipekee tunataka [kuzuia] hao watu wanaojadili Biblia na Korani," Okoth alisema, akiongeza kwamba mikusanyiko ya kisiasa na kidini imezuiwa pia kwa sababu inalengwa kiurahisi na magaidi.
"Hakuna ajenda mbaya katika kuzuia mikusanyiko hiyo ya barabarani na mitaani. Ni suala la usalama tu na tunawataka viongozi wa dini kutii na kushirikiana nasi hadi tutakapokabiliana kikamilifu na vitisho vya usalama," alisema.

Kuendeleza umoja wa kidini sio suala muhimu hapa!

Adan Wachu, katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu la Kenya (SUPKEM), alitahadharisha kwamba serikali isionekane kupendelea dini fulani katika uzuiaji huo.
"Muhadhara imekuwepo kwa miongo kadhaa na idadi kubwa ya watu wanaofika kutoka imani zote mbili imethibitisha [kupata] kwake umaarufu," alisema.
"Hatuwezi kuamua kabisa kwamba baadhi ya wahubiri wa mitaani wana kazi tofauti, lakini kwa ujumla mikusanyiko, ambayo kwa kawaida inaanza alasiri, inatafuta hasa waumini wapya katika Uislamu na kuwaimarisha wale walio katika dini hiyo," alisema.
Wachu alisema SUPKEM imefanya mikutano na wale wanaofika katika mikusanyiko na kuwaomba kupunguza kebehi zao na kuwa wavumilivu na kujali dini nyingine.
"Wanapaswa wasionekane kuwa wanapinga Ukristo. Mikusanyiko ina vipindi vya maswali, majibu na mijadala," alisema. "Vinafanyika kwa uwazi, na polisi inayotoa vibali vya mikusanyiko wako huru kuhudhuria na kuingia kukamata kama [wahubiri] wanaenda kinyume na mahubiri yao."
Mchungaji Canon Peter Karanja, katibu mkuu wa Baraza la Taifa la Makanisa ya Kenya (NCCK), alisema wahubiri wa Kikristo watafuata maombi ya serikali.
"Katika kila dini ukiwemo Ukristo (wakati wote kuna) watu wachache ambao wanafurahia mawazo ya kuogofya. Wakati makanisa na viongozi wa Kikristo wanajitegemea, tunajitahidi kadri [aiwezekanavyo] kuomba uvumilivu," .
Hata hivyo, Karanja alisema serikali inapaswa kutoa ulinzi wakati wa mikusanyiko ya kidini badala ya kuipiga marufuku.
"Kadri kulivyo na vitisho vya usalama, kuna haja ya kueneza injili. Tunafikiri serikali inapaswa kutoa ulinzi wakati wa mikusanyiko ya kidini badala ya kuipiga marufuku," alisema.
Karanja alisema NCCK pia imewaomba waumini wa makanisa kupunguza mtindo kudharau dini nyingine wakati wa ibada.
"Sio katika mikutano ya Kikristo tu ambako mahubiri yanaweza kuonekana ya uchochezi. Hata ndani ya makanisa, hususan Jumapili, yanaweza kuwa majukwaa ya kuchochea kutokuwa na uvumilivu wa kidini," alisema. "Tumewaomba viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuhimiza upendo, kusamehe, umoja na maendeleo miongoni mwa waumini wa Wakristo."

Je Nini kauli ya umma kuhusu hili?

Suleiman Bilal Hassan, mwenye umri wa miaka 35 na meneja wa kituo cha intaneti katika mtaa wa Eastleigh wa Nairobi, alisema kuwa mihadhara hiyo ilikuwa imekusudiwa kuwajulisha watu kuhusu mafundisho ya Kiislamu, lakini kuna baadhi wa wahubiri ambao wamekuwa wakilitumia vibaya jukwaa hilo.
"Wahuburi wa kweli wanapaswa kutoa tu mafundisho ya Kiislamu, lakini serikali inapaswa kuwakandamiza wahubiri waongo wanaokusudia kusababisha uadui miongoni mwa waumini tofauti," aliiuambia mtandao"Baadhi ya wahubiri hao hawaaminiki na ni waenezaji chuki."
Waandaaji wa mihadhara lazima wawe na leseni za mahubiri kuthibitishwa na wakuu wa dini kabla ya kutolewa kwa umma, alisema.
Hata hivyo, alisema, serikali inapaswa kuendelea na tahadhari "hasa ​​wakati huu ambapo idadi kubwa ya jamii ya Waislamu inahisi kulengwa na serikali katika vita dhidi ya ugaidi".
Anita Achieng mwenye umri wa miaka 23 na mwanafunzi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuchukua dhima kwa ujumbe wao wanautoa kwa umma.
"Baadhi ya ujumbe unakaribia kuwa ukafiri na serikali inapaswa kuchukua hatua ili kudumisha umoja wa wananchi," aliiambia Sabahi.
"Wahubiri lazima wazingatie maneno yao hasa wakati wakihutubia umma. Kama kauli za wahubiri katika mahubiri zinachochea vurugu mahali pengine, wanapaswa kuwajibishwa na polisi lazima wakamate na kuwashtaki kwa uchochezi," alisema.
 
Habari hii nikwa msaada wa Mtandao wa Sabahi.com
 
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Muonekano wa Bandari ya Dar.

The Tanzania Ports Authority (TPA) signed on Monday (February 10th) an agreement with stakeholders in the Dar es Salaam port to keep the port open 24 hours a day, seven days a week, Tanzania's The Citizen reported.
The agreement is part of the government's Big Results Now initiative and also brings new standard operating procedures into effect.
"This commitment now means that all stakeholders will operate 24 hours throughout the year," said TPA Acting Director General Madeni Kipande.
The new operating schedule is expected to increase the port's competitiveness by speeding up clearance time for goods with the intention of attracting more business and boosting Tanzania's economy.
Even as they signed the agreement, however, some of the stakeholders held reservations.
Recommendations made at a stakeholders' meeting last month, including the imposition of a fine for late transactions, were not incorporated into the final document, said President of the Tanzania Freight Forwarders Association Steven Ngatunga.
"We came up with recommendations and formed a committee that could incorporate them by mid-last month, but nothing has been done," he said. "Today, we have been called to sign the document which may mean the commitment to hang ourselves."
 

 

no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Watu 3 akiwemo polisi wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa kwenye ghasia katika mji wa Mombasa, Kenya, baada ya polisi kuvamia msikiti unaosemekana kutoa mafunzi ya itikadi kali za dini ya kiisilamu
Polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za raba dhidi ya waandamanaji na kuwakamata watu 100.
Viongozi wa mombasa wamelaani kitendo cha polisi wakisema kuwa ni kinyume na sheria.
Mashekhe wawili ambao wakihubiri katika msikiti wa Masjid Mussa walipigwa risasi na kuuliwa na watu wasiojulikana katika miezi ya karibuni.
Polisi wa Kenya wameuhusisha msikiti huo na kuajiri wapiganaji wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, ambalo mwaka jana lilishambulia jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi.
 
Habari hii ni kwaniba ya Shirika la habari la Uingereza BBC Swahili.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Na Rajab Ramah, Nairobi.

Utengaji wa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika utekelezaji wa mipango ya muungano kunaweza kusababisha kuvunjika kwa jitihada za muungano kamili wa kanda, wachambuzi wasema.

 

Kutoka kushoto kwenda kulia, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wakitembea pamoja wakati walipowasili kwenye mkutano wa kawaida wa 14 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Nairobi tarehe 30, 2012. [Tony Karumba/AFP]

Wakuu wa usalama kutoka Uganda, Kenya na Rwanda walikutana mjini Kigali, Rwanda mapema mwezi huu ambapo walitia saini mkataba wa usalama na ulinzi kurahisisha harakati za raia na watalii za kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika kanda unaolenga kuongeza biashara kati ya mpaka wa nchi moja na nyingine.

Mkutano huo wa tarehe 9 Januari wa maofisa wa jeshi, polisi, upelelezi na uhamiaji umefuatia uanzishwaji wa visa ya pamoja ya utalii na nchi hizo tatu ambayo ilianza rasmi tarehe 1 Januari.

Hii ilikuwa ni mara ya nne viongozi hao wa Uganda, Kenya na Rwanda kufanya makubaliano kuhusu masuala ya muungano pasipo ushiriki wa Tanzania na Burundi, ambazo pia ni mwanachama wa muungano huo wa nchi tano.

Tanzania na Burundi hazikuhudhuria mkutano uliofanyika Uganda na Kenya mwezi Agosti mwaka uliopita, au mkutano uliofanyika huko Kigali mwezi Oktoba 2013.

Tanzania ililalamika kutengwa katika mazungumzo, na rais Jakaya Kikwete alisema, "Wameunda umoja wa hiari. Nani ambaye hana hiari?"

Kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki siku zijazo?

Katika Mkutano wake wa Kawaida wa 15 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Wakuu wa Nchi huko Kampala mwezi Novemba mwaka jana, viongozi walisema watajitolea kufanya kazi pamoja, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hakuna uwezekano wa kutokea hilo.

"Nina wasiwasi kama wakuu wa nchi tatu -- Museveni, Kenyatta na Kagame -- walikuwa makini wakati wa mkutano kuhusu ahadi yao ya kusaidia wanachama wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika shughuli zao kwa sababu kinyume na azimio lao walikuwa Rwanda peke yao," alisema Rais wa Chama cha Sheria Afrika Mashariki (EALS) James Aggrey Mwamu. "Huo ni uthibitisho wa kutosha kwamba wanajitoa kufanya kazi bila ya Tanzania na Burundi."

Makubaliano ya pande tatu ni tishio kwa mtangamano wa kanda kwa kuwa yanazitenga kwa makusudi Tanzania na Burundi, alisema.

"Kile tunachokiona kinachoitwa hatua ya 'muungano wa hiari' ni ujengaji wa wingu la wasiwasi na jambo baya miongoni mwa nchi wanachama ambavyo vinaweza kuchochea mgawanyiko na kupanda mbegu ya kutoelewana ikisababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama ilivyofanya mwaka 1977," Mwamu aliiambia Sabahi. "Kwetu sisi, 'muungano huo wa hiari' haukubaliki kwa kuwa ni kinyume na mkataba ambao uliiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki."

Kushindwa kwa nchi zote wanachama kuungana katika mipango ya pamoja kisiasa na kimaendeleo ni sawa na kuiacha kanda isambaratike, alisema.

"Kwa sasa kanda inakabiliwa na changamoto nyingi zikianzia katika kukosa utulivu wa kisiasa, uharamia na ugaidi, kwa hiyo, [hatutarajii] kuwatenga wengine na kuhisi kwamba tutafanikiwa," Mwamu alisema, akiwaomba viongozi wa kanda kushauriana mara kwa mara ili wasiendelee kufanya makosa.

Mgawanyiko wadhoofisha mshikamano wa kanda

Ingawa kujumuika pamoja kunachukuliwa kuwa bora na viongozi wa kanda walio wengi, Tanzania imepata sifa ya kutoharakisha masuala ya mtangamano na Burundi inachukuliwa kama nchi isiyo na chochote cha kutoa, alisema George Omondi, mwandishi wa habari wa gazeti la The East African anayeandika kuhusu masuala ya kanda.

"Tanzania imekuwa ikiibua masuala ya umiliki wa ardhi, shirikisho la kisiasa na uraia ambavyo inataka mwongozo ulio wazi, lakini washirika wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, badala ya kukaa chini kutatua hili, wanaliona kama dalili ya kuleta mvutano," Omondi aliiambia kuninews"Wamechagua njia iliyo rahisi zaidi, ambayo ni kujitenga, [na] ambayo sio sahihi."

"Burundi inaonekana kama mshirika masikini ambaye hana thamani katika mtangamano hivyo wanachagua kuipuuza wakisahau kwamba nchi ina watu zaidi ya milioni 9 ambayo inaweza kwa urahisi kuwa soko kwa bidhaa za Kenya, Uganda au hata Rwanda," alisema.

Manu Chandaria, mfanyabiashara wa Kenya na mwenyekiti wa Kundi la Comcraft ambalo linazalisha bidhaa za chuma, plastiki na aluminiamu katika Afrika Mashariki, alisema mgawanyiko wa hivi karibuni utadhoofisha ufanikishaji wa malengo ya mtangamano wa kanda yaliyowekwa.

"Sisi katika sekta ya biashara tunahisi kuwa kuvunjika tena au kujitenga kutaanzisha vikwazo vipya katika biashara," Chandaria aliiambia kuninews. "Kila nchi inaanzisha na kutumia mifumo yake tofauti ya biashara … itakuwa ni pigo kwa biashara huria ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo muda wote huu."

Ili kufurahia kikamilifu faida inayotokana na umoja wa forodha na itifaki ya soko la pamoja, na kukamilisha uanzishaji wa fedha ya pamoja na shirikisho la kisiasa, alisema viongozi wa kanda hiyo wanapaswa kuvumiliana na kuwa tayari kushughulikia masuala ya msingi.

Kuiacha nchi moja nyuma kutazuia mchakato mzima, alisema.

"Tunachokiona ni kutokuwa na uvumilivu kwa baadhi ya viongozi. Hatuwezi kudhani kwamba tutaendelea kwa kuwaacha wale walioibua maswali kuhusu mchakato," alisema Chandaria. "Wangepaswa kukaa na kujaribu kutatua matatizo yaliyoibuliwa na Tanzania badala ya kuamua kuendelea."

EAC imeungana na ni yenye malengo, asema Kandie

Kwa upande wake, Katibu wa Wizara ya Masuala ya Afrika Mashariki Kenya Phyllis Kandie alipinga hisia za kujitenga, akisema muungani wa EAC utafanyika kama ilivyopangwa.

"Sitapenda kuingizwa katika mjadala huo 'muungano wa hiyari', lakini ninachoweza kukueleza ni kwamba sisi ni muungano kama tulivyokuwa awali na kwamba tuna malengo ya kufanikisha misingi ya EAC," Kandie aliiambia Sabahi.

Katika kujibu swali la iwapo mikutano ya nchi hizo tatu zinapingana na mkataba wa EAC, alisema, "Uganda, Kenya na Rwanda wanatumia utengano wa nchi kadhaa ambayo imeelezwa katika mkataba."

Utengano huo ni msingi katika Kifungu cha 7 cha Mkataba wa EAC, ambacho kinaruhusu maendeleo katika umoja miongoni mwa kundi dogo la wajumbe katika muungano mkubwa katika maeneo tofauti na katika kasi tofauti.

Hata hivyo, chini ya kifungu hicho, nchi wanachama ambazo zinataka kuendeleza kwa haraka bado zinatakiwa kuwafahamisha wajumbe wengine, ambalo halijafanyika katika suala hili, kwa mujibu wa Mwamu.

Jaribio la kumpata Katibu Mkuu wa EAC Richard Sezibera kwa ajili ya maoni halikufaulu

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Raia wa Uswisi Magd Najjar (kulia) akifikishwa mahakamani mjini Nairobi kushitakiwa rasmi kwa kuwa na mafungamano na al-Shabaab. Najjar ni mmoja wa washukiwa wengi wa al-Shabaab wenye utaifa wa nchi mbalimbali wanaodhaniwa wapo Kenya. [Simon Maina/AFP]


Jamii ya Kisomali nchini Kenya imelaumiwa sana kwa mashambulizi ya al-Shabaab, lakini wachambuzi wa masuala ya usalama wanaonya kwamba kuwasingizia Wasomali kunaongeza hatari ya mashambulizi ya baadaye kwani wanamgambo wa jamii nyingine wanaweza kufanya shughuli zao za kigaidi bila kufahamika.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Somalia
Ujumbe wa juu kutoka serikali ya Somalia ulikutana na kiongozi wa wapiganaji wa Ras Kamboni Sheikh Ahmed Mohamed Islam huko Kismayu Alhamisi (tarehe 27 Disemba), Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Faith Kabura Makena alivunja kikwazo cha kijinsia kwa madereva wa kike wa bodaboda mjini Garissa. [Bosire Boniface/Sabahi]
 Picha ya teksi ya pikipiki ya Faith Kabura Makena kwenye barabara za Garissa nchini Kenya inatoa taswira ya nadra sana.

Makena, mwenye umri wa miaka 30, alisema anajua kwamba kuchagua kwake biashara hii kumesababisha utata na mara kadhaa huwashangaza wakaazi wa huko anapowapita.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi
Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mr Nelson Tugume, the chief executive officer of Inspire Africa, and his wife Atukunda, admire their new born baby girl at Nakasero

hospital on Christmas Day. PHOTO BY STEPHEN OTAGE.
By Frederic Musisi, Abdu Kiyaga, Farahani Mukisa, Abubaker Kirunda, Martin Okudi & Geoffrey Mutegeki
Kampala
Hospitals in Kampala District have registered the largest number of babies born on Christmas
Day, according to a mini-survey done by this newspaper. Out of the 175 babies recorded
countrywide, Kampala hospitals had 119 babies. Out of these, 58 were girls and 61 boys.