Watu wawili wamefariki Dunia na wengine thelasini na sita (36) kujeruhiwa kwenye ajali ya basi la “Bunda Expres” iliyotokea Mkoani Mwanza katika Wilaya ya Magu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, basi hilo lililokuwa likitokea Mkoani Mara katika wilaya ya Bunda na kuelekea Mkoani Kagera katika mji wa Mtukula.
Taarifa zimesema kwamba basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi liliacha njia kufuatia mvua iliyokuwa inanyesha Mkoani humo na hivyo kusababisha hali ya utelezi karibu kila sehemu ya barabara hiyo na hivyo kutokana na mwendo kasi alikuwa nao dereva huyo alishindwa kumudu
hali hiyo hivyo gari kuacha njia na kupinduka.
Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Kamanda Nuru Suleiman amasema, tatizokubwa lililo sababisha ajali hiyo, ni mwendo kasi usio zingatia hali ya hewa. “ Hivi sasa Mkoani Mwanza kuna mvua zinanyesha hivyo, Madereva wasipo kuwa makini nia lazima
ajali kama hizi zitokee.”
Nao mashuhuda wa ajali hiyo,wameuwambia matandao huu kuwa eneo hilo halijawahi kutokea ajali katika siku za hivi karibuni, ila wanavyofahamu eneo hilo nyakati za mvua huwa linakuwa na utelezi sana.
Taarifa zilizopatikana kutoka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando zinasema kuwa majeruhi kumi na watano waliopokelewa, kumi na wawili walitibiwa na kurejea nyumbani ili hali wagonjwa watatu bado wanaendelea na matibabu na wanaendelea vizuri.
Wagonjwa wengine walipelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Magu, na jitihada za Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo ili aweze kuzungumzia hali zao hazikufanikiwa.
Na Atley Kuni- Mwanza
Post A Comment: