Arsenal, Chelsea, Barcelona, Porto, Basel na Borussia Dortmond zatakata kwenye ligi ya mabingwa wa Ulaya:

 
Mzunguko wa pili wa ligi ya mabingwa wa Ulaya ulinza jana usiku na kuendelea tena leo jumanne katika viwanja vinanwe barani Ulaya. Siku ya Jumanne usiku, timu zilizopangwa kwenye makundi ya E, F, G na H zilijitupa uwanjani, ili kuwania pointi tatu muhimu.
Mechi zilizochezwa katika kundi E, Basel ya Uswisi iliweza kuitandika Schalke ya Ujerumani bao 1-0. Nchini Romania, klabu ya Steaua Bucharest ya Romania imebugia mabao 4-0  kutoka kwa wageni wao Chelsea ya Uingereza.
Kundi F, Arsenal ya Uingereza  imeonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali msimu huu, baada ya kuibanjua Napoli inayoongoza ligi ya serie A nchini Italia kwa kuitundika mabao 2-0. Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Borussia Dortmund ya Ujerumani iliigaragaza Olimpique Marseille ya Ufaransa kwa mabao 3-0.
Kundi G, Porto ya Ureno  iliigaragaza Atletico Madrid ya Uhispania kwa mabao 2-1. Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Zenit St Petersburg ya Russia ilitoka sare ya tasa na Austria Vienna ya Austria katika dimba la Petrovskiy.
Kundi H, AFC Ajax Amsterdam ya Uholanzi yasimamishwa, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na AC Milan ya Italia, huku Celtic ya Scotland ikisalimu amri ya kufungwa bao 1-0 na Barcelona ya Uhispania.
Leo Jumatano kutashuhudiwa mechi nyingine 8 za makundi A,B,C na D na miongoni mwa pambano linalosubiriwa kwa hamu na washabiki wa soka ni mechi kati ya Manchester City ya Uingereza na Bayern Munich ya Ujerumani.
Axact

Post A Comment: