Rais Joyce Banda wa Malawi atishiwa kuuawa
.Ni kutokana na kuwabana Mafisadi
Rais
Joyce Banda wa Malawi ametishiwa kuuawa, baada ya kutekeleza mikakati yake ya
kufichua na kupambana na ufisadi uliokithiri nchini humo. Brown Mpinganjira,
Waziri wa Habari wa Malawi amethibitisha habari hizo na kusema kuwa, mafisadi
wameanza kutishia maisha ya kiongozi huyo wa Malawi kutokana na msimamo wake wa
kuvunja baraza la mawaziri na kufichua ufisadi mkubwa wa kifedha uliofanywa na
viongozi waandamizi nchini humo. Mpinganjira amesema kuwa, baadhi ya vitisho
hivyo vimetolewa toka nje ya nchi hiyo na jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi na hatimaye kubaini wahusika wa njama hizo. Inafaa kuashiria hapa
kuwa, tarehe 10 Oktoba mwaka huu, Rais Joyce Banda aliamua kulivunja baraza la
mawaziri baada ya kufichuliwa kashfa ya ufisadi wa dola milioni tatu uliofanywa
na viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Malawi. Joyce Banda anayehesabiwa
kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo, aliingia madarakani mwaka 2012 baada
ya kufariki dunia Bingu wa Mutharika rais wa zamani nchini humo.
Post A Comment: