HII NI MOJA YA MIKUSANYIKO YA WATU KUSIKILIZA NENO LA MUNGU. |
Polisi wa Kenya na viongozi wa
dini wanashirikiana kuzuia kuenea kwa itikadi za imani kali katika mikusanyiko
ya umma inayoandaliwa na wahubiri wa Kikristo na Kiislamu.
Katika mikusanyiko hiyo, ambayo
ni ya kawaida kando ya mitaa na katika masoko ya wazi nchini Kenya, wahubiri
wanalenga kuwaelimisha wafuasi wao na kuwabadili dini watu wa imani nyingine.
Mikusanyiko ya Wakristo inajulikana nchini kama "crusades" wakati
mikusanyiko ya Waislamu inajulikana kama "muhadara".
Lakini hivi karibuni, mikusanyiko
kama hiyo imekuwa chanzo cha hamaki na hotuba za uchochezi ambazo zimechokoza
mivutano ya madhehebu.
Ingawa uhuru wa kujumuika,
kuabudu na kukusanyika umewekwa katika katiba ya Kenya, Inspekta Jenerali wa
Polisi David Kimaiyo alisema kwamba baadhi ya mikusanyiko inaweza kuchochea
kiurahisi mvutano na vurugu za kidini.
"Tunao waumini wenye imani
kali kutoka katika Ukristo, Uislamu na hata katika Uhindi ambao wanaweza kujibu
kwa vurugu kama wataona kwamba dini yao inashambuliwa," aliiambia mtandao
huu.
"Hatuna tatizo lolote na
wakusanyikaji katika mikusanyiko hiyo kwa kuwa wanajaribu kueneza dini yao na
katika hatua hiyo wanapata roho chache zinazobadili dini kuingia katika dini
yao," Kimaiyo alisema. "Lakini katika wakati ambayo nchi iko katika
uchungu wa mashanbulizi ya al-Shabaab, tuna wasiwasi kwamba baadhi ya
mikusanyiko inaweza kusaidia tu kuchochea uhasama wa kidini."
'Hali tete ya usalama' hatarini.
"Kitu tunachowaomba tu
kutoka kwa wanaokutana katika mikusanyiko hiyo ni kuzingatia hali tete ya usalama
wa nchi na kuepuka kutovumiliana dhidi ya dini nyingine," alisema.
Baadhi ya viongozi wa mikusanyiko
hiyo huko Nairobi, Garissa, Wajir na Mombasa wako katika uchunguzi wa polisi
ili kufuatilia hotuba zao na sheria, Kimayo alisema. "Tumezungumza na wakusanyikaji
kadhaa kutoka katika imani zote mbili na wamekubali kupunguza," alisema.
Kama umoja, amani na utulivu
vinatishiwa, Kimaiyo alisema, polisi itapiga marufuku mikusanyiko yote ya dini,
maandiko, hotuba na vitu vingine vinavyoonekana kuleta uchochezi.
Upigaji marufuku wa kudumu wa
mikusanyiko hiyo tayari umeshafanyika katika Kaunti ya Mombasa kufuatia msururu
wa matukio ya vurugu yaliyochochewa na mauaji ya wahubiri wa dini.
Kaimu Kamanda wa kaunti ya
Mombasa Tom Okoth aliiambia Sabahi kaunti iliweka marufuku hiyo tarehe 4
Februari baada ya uchunguzi kugundua kwamba mikusanyiko inaweza kuleta vita ya
kidini na kuchochea vurugu. Wafuasi wa mikusanyiko wana tabia ya kubeza imani
ya wengine na kuchukuliana kama mahasimu, alisema.
"Kipekee tunataka [kuzuia]
hao watu wanaojadili Biblia na Korani," Okoth alisema, akiongeza kwamba
mikusanyiko ya kisiasa na kidini imezuiwa pia kwa sababu inalengwa kiurahisi na
magaidi.
"Hakuna ajenda mbaya katika
kuzuia mikusanyiko hiyo ya barabarani na mitaani. Ni suala la usalama tu na
tunawataka viongozi wa dini kutii na kushirikiana nasi hadi tutakapokabiliana
kikamilifu na vitisho vya usalama," alisema.
Kuendeleza umoja wa kidini sio suala muhimu hapa!
Adan Wachu, katibu mkuu wa Baraza
Kuu la Waislamu la Kenya (SUPKEM), alitahadharisha kwamba serikali isionekane
kupendelea dini fulani katika uzuiaji huo.
"Muhadhara imekuwepo kwa
miongo kadhaa na idadi kubwa ya watu wanaofika kutoka imani zote mbili
imethibitisha [kupata] kwake umaarufu," alisema.
"Hatuwezi kuamua kabisa
kwamba baadhi ya wahubiri wa mitaani wana kazi tofauti, lakini kwa ujumla
mikusanyiko, ambayo kwa kawaida inaanza alasiri, inatafuta hasa waumini wapya
katika Uislamu na kuwaimarisha wale walio katika dini hiyo," alisema.
Wachu alisema SUPKEM imefanya
mikutano na wale wanaofika katika mikusanyiko na kuwaomba kupunguza kebehi zao
na kuwa wavumilivu na kujali dini nyingine.
"Wanapaswa wasionekane kuwa
wanapinga Ukristo. Mikusanyiko ina vipindi vya maswali, majibu na
mijadala," alisema. "Vinafanyika kwa uwazi, na polisi inayotoa vibali
vya mikusanyiko wako huru kuhudhuria na kuingia kukamata kama [wahubiri]
wanaenda kinyume na mahubiri yao."
Mchungaji Canon Peter Karanja,
katibu mkuu wa Baraza la Taifa la Makanisa ya Kenya (NCCK), alisema wahubiri wa
Kikristo watafuata maombi ya serikali.
"Katika kila dini ukiwemo
Ukristo (wakati wote kuna) watu wachache ambao wanafurahia mawazo ya kuogofya.
Wakati makanisa na viongozi wa Kikristo wanajitegemea, tunajitahidi kadri
[aiwezekanavyo] kuomba uvumilivu," .
Hata hivyo, Karanja alisema
serikali inapaswa kutoa ulinzi wakati wa mikusanyiko ya kidini badala ya
kuipiga marufuku.
"Kadri kulivyo na vitisho
vya usalama, kuna haja ya kueneza injili. Tunafikiri serikali inapaswa kutoa
ulinzi wakati wa mikusanyiko ya kidini badala ya kuipiga marufuku,"
alisema.
Karanja alisema NCCK pia
imewaomba waumini wa makanisa kupunguza mtindo kudharau dini nyingine wakati wa
ibada.
"Sio katika mikutano ya
Kikristo tu ambako mahubiri yanaweza kuonekana ya uchochezi. Hata ndani ya makanisa,
hususan Jumapili, yanaweza kuwa majukwaa ya kuchochea kutokuwa na uvumilivu wa
kidini," alisema. "Tumewaomba viongozi wa dini kutumia nafasi zao
kuhimiza upendo, kusamehe, umoja na maendeleo miongoni mwa waumini wa
Wakristo."
Je Nini kauli ya umma kuhusu
hili?
Suleiman Bilal Hassan, mwenye
umri wa miaka 35 na meneja wa kituo cha intaneti katika mtaa wa Eastleigh wa
Nairobi, alisema kuwa mihadhara hiyo ilikuwa imekusudiwa kuwajulisha watu
kuhusu mafundisho ya Kiislamu, lakini kuna baadhi wa wahubiri ambao wamekuwa
wakilitumia vibaya jukwaa hilo.
"Wahuburi wa kweli wanapaswa
kutoa tu mafundisho ya Kiislamu, lakini serikali inapaswa kuwakandamiza
wahubiri waongo wanaokusudia kusababisha uadui miongoni mwa waumini
tofauti," aliiuambia mtandao"Baadhi ya wahubiri hao hawaaminiki na ni
waenezaji chuki."
Waandaaji wa mihadhara lazima
wawe na leseni za mahubiri kuthibitishwa na wakuu wa dini kabla ya kutolewa kwa
umma, alisema.
Hata hivyo, alisema, serikali
inapaswa kuendelea na tahadhari "hasa wakati huu ambapo idadi kubwa ya
jamii ya Waislamu inahisi kulengwa na serikali katika vita dhidi ya
ugaidi".
Anita Achieng mwenye umri wa
miaka 23 na mwanafunzi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema kuwa
viongozi wa dini wanapaswa kuchukua dhima kwa ujumbe wao wanautoa kwa umma.
"Baadhi ya ujumbe unakaribia
kuwa ukafiri na serikali inapaswa kuchukua hatua ili kudumisha umoja wa
wananchi," aliiambia Sabahi.
"Wahubiri lazima wazingatie
maneno yao hasa wakati wakihutubia umma. Kama kauli za wahubiri katika mahubiri
zinachochea vurugu mahali pengine, wanapaswa kuwajibishwa na polisi lazima wakamate
na kuwashtaki kwa uchochezi," alisema.
Habari hii nikwa msaada wa Mtandao wa Sabahi.com
Post A Comment: