Huu ndio mkono wa Bandia, aliowekewa binadamu. |
Mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis Aabo amekuwa binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia kama ule wa binadamu.
Katika tukio linalopigiwa upatu kuimarisha
hali ya walemavu katika siku za usoni, madaktari huko Italia wameuunganisha
mkono huo wa kielektroniki na neva za mabaki ya mkono wa Dennis uliokatwa baada
ya ajali mbaya ya fataki na hivyo kumwezesha kuhisi kupitia kwa vidole vya
mkono huo wa kielektroniki .
Silvestro Micera aliyeongoza upasuaji huo
alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake kuutumia mkono huo bandia .
'' tumeshangazwa sana na urahisi wa mgonjwa
wetu kuwasiliana mara moja na mkono huu bandia wa kielektroniki kuekelea
majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti .
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Dennis hakuficha furaha yake alisema mkono
huo umebadilisha kabisa hali yake.
''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida''
''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida''
Post A Comment: