BAADHI YA PICHA KUTOKA MAKTABA ZIKIMUONESHA RC AKIWA ZIARANI.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, anaanza ziara ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara hizo ambazo amekuwa akizifanya mara kwa mara.
 
Kwa mujibu taarifa iliyopatikana kutoka katika ofisi hiyo, mkuu huyo wa Mkoa atanza rasmi ziara yake katika Wilaya ya Misungwi katika kijijicha Mwalolabagole ambapo atakagua mwalo wa eneo hilo na kujionea maradi wa Udhibiti wa Magugumaji, uzalishaji vifaranga wa samaki na ufugaji wa samaki.
 
Mara baada yakuhitimisha ziara yake siku ya leo hapo kesho ata tembelea katika Wilaya ya Sengerema kabla yakuendelea na ziara yake katika  Wilaya ya Magu kwa siku inayofuata.
 
Mkoa wa Mwanza ni mmoja ya Mikoa inayotekeleza mpango wa BRN ambapo mambo yaliyopewa kipaumbele katika Mkoa huo ni Maji na suala la Elimu.
Axact

Post A Comment: