JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
mujibu wa
Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria
Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na
kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika
Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Watanzania
wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 482 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama
ifuatavyo:
MASHARTI YA
JUMLA KWA KAZI ZOTE.
ii. Waombaji
wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii.
Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada
tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa
Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi
ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha,
kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na
namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa
kuaminika.
vi. Maombi
yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne
na kidato
cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa
sawa kuondoa
uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Shahada ya
juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada.
- Cheti cha
mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha
Kompyuta
- Vyeti vya
kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja
“Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii.
“Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati
matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii.
Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji
waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama
wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji
kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma
wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na
CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho
wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Aprili, 2014
xiii. Aidha,
uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira
HAURUHUSIWI.
xiv.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa
na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi
yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia
posta kwa anuani ifuatayo;-
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
(NAFASI 1)
Nafasi hii
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki. 1.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kusajili vizazi, vifo na ndoa na kutoa hati za viapo.
. Kuweka
kumbukumbu za matukio muhimu,
. Kuwapokea
na kuwahoji wakimbizi wanaowasili,
. Kuweka
kumbukumbu za Wakimbizi
. Kutunza na
kugawa vifaa vya wakimbizi katika makazi.
. Kuainisha,
kuchambua na kushauri kuhusu matatizo ya wakimbizi.
. Kusimamia
nidhamu ya wakimbizi.
. Kusimamia
utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbalimbali Serikalini
kutegemeana
mahali alipo.
. Kusimamia
kazi za utawala na uendeshaji katika ofisi za Serikali.
. Kutoa
vitambulisho kwa wakimbizi.
1.2 SIFA ZA
MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali
katika fani zifuatazo:- Utawala, Sheria (baada ya internship), na
Menejimenti
ya Umma
. Awe na
ujuzi wa kutumia kompyuta
1.3 MSHAHARA
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 MCHUMI
DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 23)
Nafasi hizi
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki, Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango na
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia .
2.1 MAJUKUMU
YA KAZI
. Kuhudumia
kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati
ya mahesabu
ya mashirika ya Umma)
. Kukusanya
takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na
uandaaji wa
sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
. Kufanya
utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
. Kufanya
utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
. Kukusanya
taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya
ustawi
namaendeleo ya jamii.
.
Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
2.2 SIFA ZA
MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye shahada ya kwanza ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya
fani
zifuatazo;
. Uchumi
(Economics)
. Takwimu
(Statistics )
. Sayansi ya
Uchumi Kilimo (BSc Agriculture Economics & Agribusness) kutoka
Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine au Chuo kingine
chochote
kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
2.3 MSHAHARA
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
3.0 MCHUMI
DARAJA LA II (ECONOMIST GRADE II) – (NAFASI 1)
Nafasi hii
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
3.1 MAJUKUMU
YA KAZI
. Kuhudumia
kamati mbalimbali za Bunge (Kamati za mahesabu ya Serikali, Kamati
ya mahesabu
ya mashirika ya Umma)
. Kukusanya
takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na
uandaaji wa
sera na mipango ya kiuchumi na kijamii
. Kufanya
utafiti na uchambuzi wa sera na vigezo vya kiuchumi jumla
. Kufanya
utafiti na kubainisha fursa zilizopo katika sekta husika
. Kukusanya
taarifa na takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya
ustawi
namaendeleo ya jamii.
.
Kutayarisha na kusambaza takwimu na taarifa za kiuchumi kwa wadau
fani ya
Uchumi (Economics) au Fedha (Finance) kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa
na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta
3.3 MSHAHARA
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
4.0 AFISA
MAENDELEO YA JAMII DARAJA II (COMMUNITY DEVELOPMENT
OFFICER
GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hii
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume
ya Mipango.
4.1 MAJUKUMU
YA KAZI
. Kuandaa na
kupendekeza mipango na mikakakati ya kubadili fikra za watu ili
waweze kuwa
na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali na wakati
uliopo
. Kupitia
mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii kama vile:-
- Usafi wa
mazingira
- Ujenzi wa
nyumba bora
- Ujenzi wa
shule
- Ujenzi wa
zahanati
- Kuchimba
au kuzifanyia matengenezo barabara hasa za vijijini
- Ujenzi wa
majosho
- Uchimbaji
wa visima vifupi
-
Utengenezaji wa malambo
.
Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
. Kusambaza
na kuhamasisha matumizi ya teknolojia sahihi kama vile uvunaji wa
maji ya
mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
.
Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya Maendeleo ya
Wananchi
. Kuwasadia
wanachi vijijini kuandaa maandiko (Project Write ups) ya kuombea
fedha za
kuendesha miradi yao
.
Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia na Utawala bora
. Kukusanya,
kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu muhimu
kwa ajili ya
matumizi ya jamii
. Kuwezesha
wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wanchi
hasa
wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virusi vya UKIMWI na magonjwa
ya mlipuko.
. Kuelimisha
viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali
kuhusu Sera mbalimbali
za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na
kutumia Sera
hizo
. Kutoa
taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali .
4.2 SIFA ZA
MWOMBAJI
. Kuajiriwa
wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii
kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:-
. Maendeleo
ya Jamii (Community Development)
. Elimu ya
Jamii (Sociology)
. Masomo ya
Maendeleo (Development Studies)
. Mipango na
Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management)
. Maendeleo
na Jinsia (Gender and Development)
4.3 MSHAHARA
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
5.0 AFISA
HABARI II – (NAFASI 3)
Nafasi hii
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume
ya Mipango.
5.1 MAJUKUMU
YA KAZI
. Kukusanya
na kuandika habari.
. Kupiga
picha.
. Kuandaa
picha za maonyesho.
. Kuandaa
majarida na mabango (Posters).
. Kukusanya
takwimu mbalimbali.
. Kuandaa
majarida na vipeperushi.
. Kuhifadhi
picha na kuhudumia maktaba na marejeo.
5.2 SIFA ZA
MWOMBAJI
. Awe na
Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu ya Uandishi wa Habari au sifa
inayolingana
nayo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
5.3 MSHAHARA
Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
6.0 MKAGUZI
HESABU WA NDANI II (INTERNAL AUDITOR II) – (NAFASI 3)
Nafasi hii
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais Tume
ya Mipango.
6.1 MAJUKUMU
YA KAZI
. Kufanya
Ukaguzi wa hesabu katika Idara
.
Kusahihisha na kuidhinisha ripoti za ukaguzi
.
Kusahihisha na kuidhinisha hoja za Ukaguzi wa ndani
. Kufanya
kazi zingine atakazopangiwa.
6.2 SIFA ZA
MWOMBAJI
. Kuajiri
wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti cha kati cha uhasibu
(intermediate
stage) kinachotolewa na NBAA au sifa zinazolingana na hizo.
. AU
. Wenye
shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
serikali.
7.0 MHASIBU
DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi
ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
.
Kuidhinisha hati za malipo.
. Kuandika
taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
. Kusimamia
Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.
. Kusimamia
shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
. Kuandika
taarifa ya maduhuli.
6.3 MSHAHARA
. Kwa
kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kuidhinisha hati za malipo.
. Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
. Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila
siku.
. Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
. Kuandika taarifa ya maduhuli.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
. Kuajiri wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye cheti
cha kati cha uhasibu
(intermediate stage) kinachotolewa na NBAA au sifa
zinazolingana na hizo.
AU
. Wenye shahada/Stashahada ya juu ya uhasibu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na
serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
kwa mwezi.
8.0 MHIFADHI
WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 100)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii.
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
. Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
. Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa
picha
. Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
. Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
. Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
. Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao
kwenye hifadhi
. Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa
ushahidi Mahakamani
. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya
wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
. Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na
nyara nje na ndani ya Nchi
. Kudhibiti wanyamapori waharibifu
. Kudhibiti moto kwenye hifadhi
. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na
taaluma yake
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
. Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI
wenye Astashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife
Management) kutoka
Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine
kinachotambuliwa
na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS
B2 kwa mwezi.
9.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III – (NAFASI 327)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
. Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
. Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa
picha
. Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
. Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
. Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
. Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao
kwenye hifadhi
. Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa
ushahidi Mahakamani
. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya
wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
. Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na
nyara nje na ndani ya Nchi
. Kudhibiti wanyamapori waharibifu
. Kudhibiti moto kwenye hifadhi
. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na
taaluma yake
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
. Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI
wenye Astashahada ya Awali
ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate
in Wildlife
Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori
Pasiansi au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS
B1 kwa mwezi.
10.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – (NAFASI 10)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii.
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
. Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
. kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
. kulinda Nyara za Serikali
. Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na
ndani ya Nchi
. Kusimamia matumizi ya magari ya doria
. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya
wanyamapori na kutunza
takwimu zao
. Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
. Kudhibiti moto katika hifadhi
. Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa
ushahidi Mahakamani
. Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na
taaluma yake
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
. Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI
wenye Stashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management)
kutoka Chuo cha
Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
kwa mwezi.
11.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – (NAFASI 2)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais
Tume ya Mipango.
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri
wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua
ubovu unaohitaji
matengenezo,
. Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
. Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa
safari zote.
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
. Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV,
Wenye Leseni daraja la “C”
ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa
muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha
Majaribio ya ufundi Daraja
la II (Trade test II).
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani
TGOS.A kwa mwezi.
12.0 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II (TRANSPORT OFFICER
GRADE II ) –
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais
Tume ya Mipango.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili
ya kusaidia kutoa
maamuzi.
. Kuhakikisha kuwa takwimu na kumbukumbu zinazohusu
vyombo vya usafiri
pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema na kwa usahihi.
Kuandaa takwimu
zinazohusu maendeleo ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji,
na kuwasilisha kwa
watumiaji ndani na nje ya nchi.
. Kukusanya takwimu za usafirishaji nchini.
. Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi
mbalimnbali ya sekta ya
usafirishaji.
. Kutekeleza majukumu mengine yanayohusu sekta ya
usafirishaji
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
. Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya Usafirishaji
kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
kwa mwezi
13.0 AFISA MAZINGIRA DARAJA LA II – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais
Tume ya Mipango.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kukusanya Takwimu na Taarifa mbalimbali zinazohusu
Usimamizi na Hifadhi ya
Mazingira.
. Kutoa (disseminate) elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa
Wadau mbalimbali.
. Kushiriki katika kuandaa Mpango wa kazi na bajeti.
. Kushiriki katika tafiti zinazohusu Usimamizi na Hifadhi
ya Mazingira.
. Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Sheria zinazohusiana
na Usimamizi wa
Mazingira.
. Kufuatilia na Kuainisha Maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa.
. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uwezo
na taaluma yake.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
. Kuajiriwa wahitimu wenye Shahada ya kwanza ya
Sayansi/Sanaa yenye
mwelekeo wa Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira katika moja
ya fani zifuatazo,
‘Geography and Environmental Studies, Aquatic
Environmental Science and
Conservation, Environmental Science and Management,
Environmental
Laboratory Science Technology, Environmental Planning and
Management’ au
sifa zinazolingana na hizo kutoka Vyuo vinavyotambulika
na Serikali.
13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
kwa mwezi.
14.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU (REGISTRY ASSISTANT) –
(NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa
Pembejeo za Kilimo na Mifugo.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
. Kusimamia usahihi (accuracy) wa kumbukumbu.
. Kugawa kazi na kusimamia kazi zote za masjala.
. Kuangalia barua zote zinazoingia, kutoka na kuweka
kwenye majalada husika.
. Kutunza diary za (Bring up) na kuhakikisha zinafanyiwa
kazi kwa wakati muafaka.
. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa kulingana na uwezo
na taaluma yake.
. Kuajiriwa wahitimu wenye Stashahada ya Kumbukumbu
(Diploma in Records
Management) kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
. Awe na uzoefu wa miaka Sita (6) katika fani hii.
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Taasisi yaani GSS 5
kwa mwezi.
15.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE
OFFICER
GRADE II) – (NAFASI 5)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri.
MAJUKUMU YA KAZI
. Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa
Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya kata
. Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati
mbalimbal.i ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini.
. Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
. Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za
maendeleo ya kata, vijiji na Mtaa.
. Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria
ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli
za Uchaguzi katika
Kata.
. Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia
maendeleo ya eneo
lake.
. Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji
wengine katikangazi ya Kata.
. Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na
kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa.
. Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha
wataalamu na watendaji wa
vjiji, na NGO’S katika kata yake.
. Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote
zinazokusanywa katika vijiji,
vitongoji, na kata yake.
15.1 SIFA ZA MWOMBAJI.
. Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa
Sayansi ya Jamii (Social
Sciences) Utawala, (Public Administration and Local
Gorvernment), Sheria au Sifa
nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na
Serikali.
15.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya
Mshahara TGS D. kwa mwezi.
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma.
Post A Comment: