MKULIMA WA PAMBA WILAYANI KWIMBA AKI NYUNYUZIA DAWA YA KUUWA WADUDU KATIKA PAMBA. |
Chama kikuu cha ushirika katika Mkoa wa Mwanza (Nyanza Cooperative Union). kinatarajiwa kufanya Mkutano wake wa mwaka siku ya tarehe 04.04.2014 siku ya Ijumaa katika chuo cha ualimu Butimba Mwanza ikiwa ni Mkutano wake wa 24.
Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na kupokea taarifa ya Utekelezaji ya mwaka 2012/2013 na 2014/2014, taarifa za hesabu zilizo kaguliwa, kuridhia makisio ya mapato na matumizi na ukomo wa madeni kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Katika hatua nyingine Mkutano huo utapitia mpango mkakati wa kukiwezesha chama hicho kusonga mbele vile vile Mkutano huo kuridhia kuajiriwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani, kutoa idhini ya kuuza magari Chakavu lakini pia kuona namna nzuri ya kuanzishwa kwa Chama cha Ushirika katika Mkoa Mpya wa Geita.
Katika siku za hivi karibuni chama hicho kimekuwa katika mgogoro mkubwa kiasi cha kukifanya chama hicho kushindwa kujiendesha hadi pale Serikali ilipo ingilia kati na kuamua kuajiri baadhi ya watendaji ili waweze kukinusuru.
Nyanza ndicho chama pekee kikubwa kilicho kuwepo mkoani Mwanza, ambacho kinatajwa kuwa mkombozi kwa Mkulima wa Mkoa huo na mikoa ya jirani.
Kufufuliwa kwa Nyanza na kuanza kufanya shughuli zake kama kawaida ni dhahiri Shahiri kwamba, sasa ukombozi wa Mkulima kuacha kunyanyaswa na Wafanyabiashara na makampuni ya watu binafsi itakuwa imefikia ukomo.
Imeandaliwa na Atley Kuni.
Changamoto kubwa iliyopo mbele hivi sasa ni chama hicho, kujitahidi kiweze kujiendesha chenyewe na kuweza kuwatafutia wakulima masoko ya Uhakika ya zao la pamba, ambalo katika siku za hivi karibuni imeonekana kukabiliwa na Changamoto nyingi.
Post A Comment: