UMATI WA WATU KATIKA BARA BARA YA KENYATTA HAPA WAKISHUHUDIA FOLENI YA MAGARI NI BAADA YA KARANDINGA KUSABABISHA AJALI. |
Fatilia kwa karibu picha hizo ambazo tumezipata kwa hisani ya Blogu ya G. Sengo.
Pic up aina ya Toyota Dutsun T387 AAH ikiwa imenasa kwenye moja ya maduka mara baada ya kugongwa na karandinga hilo la mahabusu. |
Utaratibu wa kufaulisha mahabusu ukiendelea kufanywa na kikosi cha kuzuia vurugu FFU jeshi la polisi Mwanza. |
Usalama ulizingatiwa na wananchi walikatazwa kulifikia eneo la tukio umbali wa mita 100. |
Kasheshe ya msongamano barabara ya Kenyata jijini Mwanza. |
Fundi akijaribu kuweka japo sawa kwa muda ili karandinga hilo lipate kuondoshwa eneo hilo kuondoa usumbufu wa kuziba njia ya barabara hiyo muhimu.... |
Si suala la kubeza twahitaji kuboresha vitendea kazi jeshi la polisi nchini kwani ipo siku yatazuka makubwa kuliko hili lililotokea hapo jana. |
Post A Comment: