Katibu Mkuu wa TUCTA Nicolous Mugaya akizungumza na waandishi wa habari nje Ukumbi mara
baada yakufungua Semina hiyo.
Mamlaka ya Mifuko ya hifadhi ya Jamii na udhibiti SSRA, wameendelea na utoaji wa Semina kwa makundi tofauti tofauti safari hii wakitoa semina hiyo kwa Viongozi wa Vyma vya wafanyakazi katika Mkoa wa Mwanza.

Akifungua mkutano huo hii leo Katibu Mkuu wa TUCTA Taifa Nicolous Mugaya amesema lengo kuu la vyama vyama vya wafanyakazi ni kuhakikisha mfanyakazi anaboreshewa maisha kwa kumpatia mafao mazuri lakini pia mazingira mazuri yakufanyia kazi.

 Mugaya amesema, wao kama vyama vya wafanyakazi lazima wafute na kuiga kwenye nchi ambazo zimekuwa na mifuko michache na hivyo kufanya mafao kuwa bora huku akitolea mfano wa nchi ya Kenya na Zambia. akaongeza kwamba Utaratibu wa kukokotoa mafao hivi sasa upo katika hatua za awali za mchakato na itafika wakati mafao yatakuwa yana kokotolewa kwa fomula moja.

Akizungumza katika semina hiyo mgaya amesema " Tunataka siku moja mifuko ya hifadhi ya Jamii inabaki kuwa miwili ambayo itakuwa na ushindani wa dhati na hivyo kufanya maslahi ya Mtumishi kuwa bora na kuleta tija" amesema na kuongeza kuwa,  kwa hivi sasa ni mifuko michache ndio  ambayo kwa kiasi Fulani imekuwa hailalamikiwi, hivyo kama vyama vya wafanyakazi wanajukumu la kuhakikisha maslahi yanaboreshwa.

Fatilia habari kwa Picha kwa zaidi na zaidi.......!!!!

Wafanyakazi wakiimba wimbo wa Mshikamano kabla yakuanza kwa Semina hiyo.

Nasaha za Mugaya wakati wa kufungua Semina hiyo ya Siku moja.

Hapa wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada yakufungua Semina hiyo, iliyo fanyika katika Ukumbi wa CWT Mkoa wa Mwanza.


Darasa linaendelea na Umakini ni suala la Muhimu sana Bibi Sarah Kibonde Msika akitoa somo.

Tunanukuu yale ya Muhimu unayo tufundisha.

Lazima tuelewe manufaa ya hii mifuko inawigo mpana sana, kuna kitu kina itwa Multiply effects
 kutokana na uwekezaji.

Mshikamano sio kwa wanachama pekee bali pia viongozi wao.

Tunakupenda sana sana tuachie maoni yako basi ndugu.!!!




Axact

Post A Comment: