Wasimamizi waaswa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu
Imefahamika kwamba maandalizi muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku, waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba 25 mwaka huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi kumalizika. endelea baada ya picha.......
Mwanasheria wa tume ya uchaguzi Bw.Mtibora Seleman akifafanua jambo wakati wa semina hiyo. |
Wanasemina wakifatilia kwa karibu mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. |
Wanasemina ya masuala ya Uchaguzi kanda ya ziwa wakiwa darasani. |
Msisitizo kutoka kwa mwanasheria. |
Bi. Jescar Mongi kutoka tume ya uchaguzi hapa akionesha mfano wa utaratibu wa upigaji kura utakavyokuwa. |
Imefahamika kwamba maandalizi
muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku, waratibu
wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba
25 mwaka huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi
kumalizika.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na kuhusisha
Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi, na
maafisa uchaguzi kutoka katika mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu wa mkoa wa
Mwanza Manju Msambya, amesema watumishi hao wanayo dhima ya kuhakikisha zoezi
la uchaguzi linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Msambya amesema nilazima dhamana
waliopewa watumishi hao watambue ni
muhimu kwakua inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako taka kuelekea
kwa kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais. “Ndugu wanasemina
tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge uwezo katika mchakato mzima
wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha pamoja na kutangaza
matokeo ya uchaguzi” hivyo suala la umakini ni muhimu sana.
Msambya amesema, kwakutumia uzoefu walionao
watumishi hao katika mazoezi mbali mbali ya kitaifa wataweza kufanya kazi hiyo
kwa ufanisi mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki katika zoezi
kama hilo kwa mwaka 2010.
Awali akimkaribisha kufungua semina
hiyo Mratibu wa uchaguzi wa kanda ya ziwa Deogratius Nsanzugwanko alisema tayari
maandalizi kadhaa kuhusiana na uchaguzi yamekwisha kamilika ikiwapo madaftari
ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa tayari vimekwisha
anza kusafirishwa kwenda kwenye mikoa husika.
Kanda ya ziwa inayoundwa na mikoa
ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mara, ambapo kwa mkoa wa Mwanza
pekee inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,442,391 sawa na asilimia 103% ya lengo
lililokuwa limewekwa hapo awali na bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya
kuandikisha wapiga kura 1,403,763.
Imeandaliwa
Na: Atley Kuni- The Power of Media grew.
MWISHO.
Post A Comment: