Rock City Marathon kutimua vumbi
kesho (JUMAPILI)
Maandalizi ya Rock City
Marathon zinazotarajiwa kufanyika kesho Septemba 25 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
yamekamilika huku ushiriki wa wa wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu kwenye mbio
hizo ukitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio
hizo.
Mbio hizo zinazofanyika kwa
mara ya nane mfululizo
tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na kampuni ya Capital Plus International
kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza zikiwa na baraka zote kutoka Chama
cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) , zikilenga kilenga
kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio
vilivyoko kanda Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Msemaji wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.
Alisema wanatarajiwa kuwa
na washiriki zaidi ya 1200 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka
mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.
“Rock City Marathon inahusisha mbio za kilometa 21 kwa wanaume na
wanawake, mbio za Kilometa tano
zitakazohusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na
watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi
kwa ajili ya wazee, mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati
ya miaka 7 hadi 10 pamoja na mbio fupi za
mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi,’’
“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea
kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation
Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB, New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma
Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.
Kuhusu barabara
zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12:00 asubuhi Bw Kasonta alisema; “Kwa
washiriki wa mbio za km 21 wataanzia Uwanja CCM Kirumba, kwa wale wa Km 5
wataanzia barabara ya Nyerere eneo la Polisi Mabatini, kwa wale wa Km 3 ambazo
ni mbio za wazee wataanzia Barabara ya Nyerere eneo la Makaburi ya Wahindi na
kwa mbio za watoto yaani Km 2 wao wataanzia eneo la Mwaloni kuelekea CCM Kirumba,’’
Kwa upande wa zawadi kwenye mbio hizo Bw Kasonta alisema washindi wa kwanza wa mbio za
kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. mil 1.5/- kila mmoja, sh.
900,000/- kwa washindi wa
pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.
“Kwa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya
Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali
(Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa
makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.,’’
Akizungumzia usalama
katika tukio hilo ambalo litahusisha maelfu ya watu, Mwenyekiti Msaidizi wa
kamati yam bio hizo Bw Zenno Ngowi
alisema kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na jeshi la
polisi na jeshi la hilo limeshajipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo ili
kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama wakiwemo watazamaji na washiriki
mbio hizo
Post A Comment: