Hii ndio Keki Maalum iliyo andaliwa na AGPAHI mara baada yakumalizika kwa Kambi ya siku tano ya Malezi ya Vijana
Mkoani Mwanza.
Vijana wapatao 50 kutoka Mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga, ambao walikuwa katika kambi ya malezi kwa vijana waishio na VVU/UKIMWI kwa muda wa siku tano katika Jiji la Mwanza  wamelipongeza Shirika AGPAHI kwa jinsi linavyoweza kutumia ipasavyo fedha wazipatazo kutoka kwa wadau wa Maendeleo.


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa AGPAHI Dkt. Safila Telatela, Dkt Silas Wambura
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na mmoja ya Vijana wa kambi wakikata keki maalum iliyoandaliwa.



Dkt. Silas Wambura akimkabidhi cheti mmoja ya Wakufunzi wa Semina hiyo ya Vijana Bibi Tunsume Mlawa kutoka Mkoa ya Mwanza.

 Wakizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo, vijana hao wamesema wao kama vijana wanafarijika sana na kambi ambazo zimekuwa zikiendeshwa na AGPAHI.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa vijana hao kutoka mkoani shinyanga ambaye jina lake tumelihifadhi kwa sababu za kimaadili amesema, wanafahamu yapo mashirika mengi yanayo hudumia watu wenye VVU lakini mashirika hayo yameshia kuwa mifukoni mwa watu na wengine kujinufaisha wenyewe.

“Sisi tunawapongeza sana AGPAHI kwakuwa, wao wamekuwa wakituleta kutoka sehemu mbali mbali za nchi na tunapokutana tunajifunza mambo mengi ikiwapo maswala ya ushauri Nasaha, Michezo lakini pia tunapata fursa yakwenda kutembelea maeneo mbali mbali yenye historia ya nchi” alisema mmoja wa vijana hao.

Akihitimsha kambi hiyo ya siku tano, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Silas Wambura, amewataka vijana hao wakawe mabalozi wa vijana wengine ambao hawakupata fursa yakuhudhuria katika kambi hiyo. “Najua sio wote mlio hudhuria katika kambi hii lakini ninaamini kwa uwakilishi wenu ninyi mtakuwa Mabalozi wa kweli kwa wengine” alisema Silas na kuongeza wao kama Serikaliwataendelea kushirikiana na AGPAHI katika kuhakikisha bajeti inaongezeka ili kwa kipindi kingine vijana hao wawe wengi zaidi.

Akizungumza kabla yakumkaribisha Kaimu Mganga mkuu wa mkoa, Mkurugenzi wa miradi wa AGPAHI Dkt. Safia Telatela, amesema ndoto zao kama AGPAHI nikuona ndoto za vijana hao zinatimia na wanakuwa viongozi wajao katika mashirika mbali mbali yaliyopo nchini na Duniani lakini pia viongozi wa Serikali.

“Jamani Mgeni rasmi na wageni waalikwa naamini miaka ijayo kutokana na ndoto zao hawa vijana, tunaimani humu humu ndio watakuwepo Madaktari, wakurugenzi, wanasheria, wanahabari na watu wa kada tofauti tofauti alisema Dkt. Safia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Dkt.Silas Wambura,akitoa Hotuba ya Kufunga kambi ya Vijana.
Jumla ya vijana 50 kutoka mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga pamoja na walimu wao 11 walikuwepo kwenye kambi ya malezi kuhu VVU/UKIMWI mkoani Mwanza

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  Dkt.Silas Wambura, akifurahi Michoro mbali mbali ya Miti ya Maisha iliyo chorwa na Vijana waliokuwepo kwenye kambi ya AGPAHI.

Axact

Post A Comment: