Krimas 2012

Kiongozi wa waumini wa kikatoliki duniani Papa Benect XVI ameitumia nafasi ya kutoa ujumbe wa Christmas kushambulia ndoa za jinsia moja, na kuwatuhumu mashoga kuwa ni watu ambao wanaubadilisha uhalisia wao ili waweze kuendana na jinsia ambayo ni chaguo lao.


Papa Benedict ame-dedicate hotuba yake kwa “thamani ya familia na ubora wa familia”, na alisema kuwa umoja wa desturi nzuri umeshambuliwa na sheria ya ndoa za jinsia moja ikipata sapoti Uingereza, Marekani na Ufaransa.


Alisistiza kuwa theories za jinsia hazikua sahihi, na kuongeza kuwa watu walikuwa wamepotoka kwa kuchagua utambulisho wao kijinsia kitu ambacho kilikuwa kinyume na uhalisia.



Hapa Papa Benect alikuwa anapinga nadharia ambazo ziliibuka miaka 85 iliyopita baada ya kuanzishwa na Simone de Beauvoir, na kuitwa Beauvoir’s gender theory toka kwa mwanafalsafa aliyekuwa mwanaharakati wa kupigania haki za wanawake, theory ambayo ilikuwa inasema, “mwanamke hazaliwi mwanamke bali ‘anakua’ mwanamke, na kwamba jinsia ni kitu ambacho nitofauti na maswala ya kibaiolojia.”



Papa Benedict amewaambia watu wa Vatican, “ watu wanakana ukweli kuwa wana uhalisia, waliopewa kwa utambulishowa wa miili yao, kitu ambacho kinakuwa ni element ya kumtambua binadamu.”

Akaongeza kuwa, “ watu wanakana uhalisia wao na kuamua kuwa sio kitu ambacho walipewa kabla, lakini wanajitengeneza wenyewe.”



“kubadilisha uhalisia, ni kitu ambacho tunakipinga leo ambapo mazingira yetu yanahusika, sasa inakuwa ni uamuzi wa wa msingi wa binadamu ambapo yeye mwenyewe anahusika.”
Axact

Post A Comment: