Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Elias Mangu Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mwanza. |
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Eliasi Mangu aliyasema hayo jana jijini Mwanza alipokuwa anaelezea mikakati ya jeshi hilo katika kupambana na uhalifu wakati wa maadhimisho ya sikuukuu hizo.
Alisema
jeshi la polisi tayari limeainisha njia ambazo watumia magari na
watembea kwa miguu watazitumia wakati wa maadhimisho hayo na kuwataka
watu watakaotumia maadhimisho hayo katika kuchoma ovyo matairi
barabarani na kuziba njia kuwa watadhibitiwa.
“Kuzuaia barabara
kwa kuchoma tairi ni kosa la jinai, hivyo tunawataka watu
watakaojihusisha na vitendo hivyo, najua wanafanya hivyo kwa furaha ya
kusherehekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya, lakini kusherehekea kwao
kusiwe ni kero kwa watu wengine”, alisema
Alisema kwa
maadhimisho ya mwaka huu, jeshi la polisi limejizatiti kufanya doria
maalum kwa kutumia magari, kuvaa sare za binafsi ili kuweza kuwabaini
watu na wahalifu wenye lengo la kupora mali za wananchi.
“Polisi watakuwa
kila mahali makanisani na barabarani ili kudhibiti hali ya usalama kwa
wananchi, na kwa watu watakaoenda makanisani kusali nao watawekewa
ulinzi wa maaskari ili wasiweze kuporwa”,
Aliwataka wananchi
kutoa taarifa maalum pindi watakapoona watu wenye nia ya kuiba mali au
kutaka kufanya uvamizi kwenye maeneo yao.
MWISHO
Post A Comment: