Watangazi wawili wa Australia waliopiga simu ghushi hospitalini alipokuwa amelazwa mkewe Prince William, ambaye ni mjamzito wamesema wamehuzunishwa sana na kifo cha muuguzi aliyepokea simu hiyo.
Jacintha Saldanha alikutwa kafariki siku tatu baada ya kupokea simu iliyokuwa inaulizia kuhusu hali ya Duchess wa Cambridge, aliyekuwa hospitalini akiuguzwa ugonjwa unaohusika na mimba yake.
Watangazaji hao walimhadaa muuguzi huyo kwa kujifanya kuwa walikuwa Malkia na Prince Charles.
Rhys Holleran, anayemiliki kituo hicho kilichohusika, alisema kifo cha Bi Saldanha kilikuwa cha kusikitisha, lakini hakingeweza kutabirika.
Katika mahojiano na kituo cha redio cha 3AW, mjini Melbourne, Holleran alisema wafanyikazi wake walijaribu mara kadhaa kuwasiliana na Bi Saldhana na muuguzi mwingine katika Hospitali hiyo ya King George the 7th mjini London ili kujaribu kupata idhini yao kutangaza simu hiyo ya mzaha.
Axact

Post A Comment: