Mzee Nelson Mandela-Rais Mstaaf wa Afrika Kusini |
Maafisa wamesema kwamba amekuwa akifanyiwa uchunguzi, ingawaje haijajulikana kwamba ni uchunguzi wa aina gani.
Rais Jacob Zuma, aliyemtembelea Jumapili, alisema kwamba hali yake ilikuwa nzuri. Bwana Mandela ana miaka 94.
Awali, Mandela alilazwa hospitali mnamo Februari ili kutibiwa matatizo ya tumbo yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu.
Hajaonekana hadharani tangu Afrika Kusini ilipofungua michezo ya Kombe la Dunia mwaka wa 2010.
Post A Comment: