Mkutano wa
viongozi wa nchi wanachama wa jumuiaya ya madola, umeanza nchini Sri Lanka,
lakini mkutano huo umegubikwa na mjadala mkali ikiwa ilikuwa sawa kuandaa
mkutano huo nchini humo.
Mkutano wa Jumuiya ua Madola Sri Lanka |
Canada, India na
Mauritius wamesusia mkutano huo wakilalamika kuwa serikali ya Sri Lanka
ilikataa kuchunguza madai ya ukikuwaji wa haki za binadamu wakati serikali
ilipokuwa inapambana na waasi wa Tamil Tigers na kushinda mwaka 2009.
Rais Mahinda
Rajapaksa amewashukuru watu waliohudhuria mkutano huo na kuinga mkono nchi
yake.
Waziri mkuu wa
Uingeza anahudhuria mkutano huo, lakini atafanya ziara nyingine hadi maeneo la
kaskazini mwa Sri Lanka kukutana na viongozi wa Tamil ili kuelezea wasi wasi
wake.
Warsha hiyo
imefunguliwa huku mwana mfalme Prince Charles,akimwakilisha mama yake Malkia
Elizabeth, kama mkuu wa Jumuiya ya Madola .
Mkutano huu
umeanza kuhusu mkutano mwingine uliokuwa unaangazia haki za binadamu mjini
Colombo ukifungwa na maafisa wakuu nchini humo.
Mkutano huo hata
hivyo ulitarajiwa kufungwa. Mnamo Jumatano na Alhamisi mkutano huo ulivamiwa na
makundi yanayounga Serikali mkono, kukiwemo na watawa wa Kibudha na hali hiyo
ilitokea baada ya muda Polisi kuamuru kuwa mkutano huo ufungwe.
Tayari maafisa
wa usalama Kaskazini mwa Siri Lanka walikuwa wamezuia mabasi yaliyokuwa
yamewabeba watu wa kabila la Watamil kuelekea Colombo kwa mkutano huo wa Haki
za Kibinadamu.
Mashirika ya
kiraia kwa wakati huu yanajitahidi kadiri ya uwezo wao kujaribu kupata habari
kuwahusu maelfu ya watu waliotoweka; wengine wao kuanzia mwaka 1990.
Hadi kufikia
sasa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, pamoja na mwana Mfalme wa
Uingereza, Prince Charles, wamefika nchini Sri Lank kuhudhuria mkutano wa
viongozi wa Jumuiya ya Madola. Prince Charles atafungua rasmi mkutano huo
akimwakilisha mamake, Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Siku chache
zilizopita Bwana Cameron na viongozi kadhaa wa Sri Lanka wamekuwa wakijibizana
vikali kufuatia tangazo la Bwana Cameron kuwa atazua mjadala wa hali mbovu ya
haki za kibinadamu nchini Sri Lanka. Lakini viongozi wa Sri Lanka wamesema kuwa
hawatamruhusu kuzusha mjadala huo ambao Serikali hiyo, mwenyeji wa mkutano huo
inaona kama ni madharau.
Bwana Cameron
ametetea ziara yake ya Sri Lanka, licha ya makundi kadhaa kumshauri aususie
mkutano huo kwa sababu za ukiukaji wa haki za kibinadamu wa taifa hilo. Kwa
upande wake Cameron amesema ukiukaji huo ambapo wanajeshi waliwatendea unyama
waasi wa Tamil Tiger ni swala ambalo lazima alizungumzie.
Waziri Mkuu huyo
wa Uingereza alisisitiza kuwa ni heri ajitokeze na kuangazia swala hilo akiwa
mkutanoni ngambo badala ya kukaa nyumbani.
Mkereketwa wa
Haki za Kibinadamu wa Sri Lanka, Brito Fernando, amesema kuwa jamii ya
kimataifa inapaswa kupida darubini kwa yote yanayoendelea nchini Sri Lanka
Post A Comment: