WAZIRI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE UWEKAJI JIWE LA MSINGI.
|
MALORI YALIO PIGWA STOP NA MAGUFULI.
MKUU WA MKOA WA MWANZA, MHANDISI EVARIST NDIKILO KWENYE UWEKAJI JIWE LA MSINGI.
Na:
Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
Waziri wa Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli, ameonya wenye malori
kupita katikati ya jiji la Mwanza mara baada ya kukamilika kwa Mradi wa ujenzi
wa barabara ya km. 17 kutoka Kisesa hadi Usagara ili kuweza kuzifanya barabara
hizo ziweze kudumu.
Magufuli aliyasema hayo, wakati alipokuwa akiweka jiwe la Msingi
kwenye maradi wa ujenzi wa daraja la Mabatini linalojengwa kwa ajili ya
kuepusha ajali za mara kwa mara zilizo kuwa zinatokea katika eneo hilo, alisema
“ilikuzifanya barabara za katikati ya Jiji ziweze kudumu ni lazima tuzitunze na
kuzitunza ni kwa wenye malori kuhakikisha wanapita kwenye bara bara tunazo
zifungua pembezoni mwa mji, alisema na kuongeza kuwa katika hilo hakuna mjadala”
kwa kuwa yeye aliaminiwa na Mhe. Rais hivyo anazo nguvu zote za kuweza
kudhibiti, pindi barabara zitakapokamilika wenye malori wasivumiliwe tena
kupita katikati ya Jiji.
Katika hatua nyingine Magufuli ameahidi kuwekewa kwa uzio kwenye
darajahilo la mabatini ili waenda kwa miguu wasiweze kukatisha kwa urahisi,” Ni
kweli Mstahiki Meya amenikumbusha jambo la maana, ilituweze kuepusha ajali za mara
kwa mara tutahakikisha tunaweka uzio mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa
daraja hili na kabla ya kuanza kutumika” alisema Magufuli.
Awali kabla kuhutubia umati wa watu waliofika kumshuhudia
uwekaji wa jiwe la Msingi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliwasilisha ombi la
kupanuliwa kwa barabara ya Airport, ambayo inategemewa na idadi kubwa ya watu, “Mhe.
Waziri wahenga walinena unapokutana na Jumbe, umsalimie hapo hapo,na mimi
Mhe waziri sisi wana Mwanza Jiji letu linakuwa kwa kasi sana na msongamano wa
watu unazidi kuongezeka, alisema na kuongeza “kukamilika kwa Soko la kimataifa
la Ghana, ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua magari 2000 kwa wakati mmoja na
pikipiki 200 ni dhahiri kwamba…! hata msongamano utakuwa mkubwa…..! lakini sio
hilo tu Mhe Waziri kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza ni
ishara kwamba, tuna kila sababu ya kuongeza barabara hiyo na kuwa njia nne alisema
Ndikilo huku akishangiliwa na umati wa watu waliokuwa wamefurika eneo hilo la
mabatini.
Akijibu, Magufuli alisema ameyasikia maombi hayo na tayari
mchakato umekwisha anza ikiwa ni pamoja na kuona awezekano wa kuwa na usafiri
wa majini ambao utarahisisha usafiri na kuondoa msongamano wa watu mjini lakini pia Boti zitakazo kuwa zinatumika ni
haraka (Speedboats), na itawawezesha watumia Boti kufanya utalii wa Majini
alisema waziri.
Katika hatua nyingine Waziri Magufuli, alisema ameyapokea maombi
yaliyotolewa na Diwani wa kata ya Mbugani bwana Hashimu Kijuu kwa niaba ya
wananchi wa mabatini juu ya ujenzi wa barabara ya Nyerere “A” ambayo inahudumia zaida ya watu 5000 kwa siku,” Huyu
Diwani ni mtu mzuri kwa sababu amesema juu ya maendeleo na sio ushabiki wa
vyama ombi lake nimelielewa na nipende kumuahidi kuwa katika mwaka ujao wa
fedha halmashauri ya jiji imuandikie barua ili aweze kulishughulikia, Diwani
huyo aliwasilisha maombi ya ujenzi wa barabara moja miongoni mwa tatu alizo zitaja.
Kwa upande wao wananchi waliongea na mtandao huu wamesema kukamilika
kwa mradi huo itakuwa ni ukombozi kwa wananchi wa jiji la Mwanza kwani itasidia
kupunguza ajali za barabarani ambazo zinatajwa kutokea ajali 48 kati ya kipindi
cha 2010/2013 ambapo ajali 22 zilisababisha watu kupoteza maisha na watu 26
kupata vilema vya maisha” Ni ukweli kwamba kipato cha wachuuzi wa picha madhari
ya Jiji kunakishka ni vitu ambavyo tutegemee” aliniambia Mwandishi mwandamizi
wa ITV na Radio One, bw. Mabere Makubi.
Post A Comment: