MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage
ameliambia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania lililomtaka aitishe Mkutano
Mkuu wa Dharura ndani ya siku 14, ili kutatua mgogoro kati yake na Kamati ya
Utendaji.
Rage aliyasema hayo Dar es Salaam jana
alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia agizo hilo sanjari na la Kamati
ya Utendaji ya Simba iliyomsimamisha siku chache zilizopita.
“Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa na
kuamua kunisimamisha ni batili kwa kuwa aliyeitisha mkutano huo hana mamlaka ya
kufanya hivyo kwa Katiba ya Simba, hivyo ni sawa cha harusi,” amesema.
Amesema alidhani kwa kitendo hicho
(kusimamishwa), TFF ingepinga jambo hilo kwa kuwa ni kinyume na taratibu za
michezo kuhusu kufanya mapinduzi lakini na wao ndio kwanza wamempa siku 14
kuitisha mkutano.
Amesema kutokana na kukiukwa kwa Katiba ya TFF na
Klabu ya Simba, hataitisha mkutano wowote kama alivyotakiwa ili naye asivunje
Katiba na kama atalazimishwa kufanya hivyo yuko tayari kujiuzulu.
Rage ame tolea mfano wa msuguano uliotokea katika
kipindi cha uchaguzi wa TFF uliofanya Serikali kuingilia kati sanjari na
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (Fifa), amesema baada adha hiyo
kutokea, Fifa iliamuru TFF iitishe uchaguzi na kuwapangia tarehe na agenda.
Anadai kuwa kitendo cha TFF kumwagiza
kuitisha mkutano ndani ya siku 14 pamoja na kumchagulia agenda ni kinyume cha
Katiba yake (TFF) , hivyo hatoitisha mkutano kama alivyotakiwa.
Akizungumzia kuhusu tuhuma zinazomakabili
zilizochangia kusimamishwa kwake, kuhusu mshambuliaji wao za zamani, Emmanuel
Okwi, alisema suala hilo linashughulikiwa na Ofisa wa Fifa anayeitwa Laura
Santaniel.
Ameongeza kuwa suala la uchelewashaji wa fedha
hizo ilitokana na klabu iliyomsajili ya Etoile du Sahel (ESS) ya nchini
Tunisia kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi hali iliyofanya baadhi ya viongozi
wa Simba akiwemo Hanspoppe kulifuatilia na sasa linashughulikiwa na Fifa.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura
alipotakiwa kueleza ni hatua gani zitachukuliwa ikiwa Rage hataitisha Mkutano
Mkuu wa Dharura kama alivyoagizwa, alisema kwa kuwa bado siku 14 hazijaisha
watasubiri ili kuchukua hatua nyingine.
“Tunashukuru kuwa amekiri kupokea barua yetu,
hivyo tunasubiri hadi siku 14 ziishe ndio atajua TFF nini itafanya dhidi yake,
tusubiri muda uishe na leo (jana) ikiwa ni siku ya pili, alisema.
Awali TFF ilitoa agizo la kumtataka Rage aitishe
Mkutano Mkuu wa Dharura ili kumaliza mgogoro uliopo, kwa kutumia Ibara 1(6) ya
Katiba ya Simba inayosema, “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu
Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na Fifa na kuhakikisha kuwa
zinaheshimiwa na wanachama wake.”
Wakati huohuo, Rage katika mkutano huo,
alitangaza kumteua, Richard Wambura kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji
wa klabu ya Simba.
Rage akizungumzia suala la kusaini Mkataba na
Azam TV alisema suala hilo halihitaji shule kwa kuwa mhusika mkuu ni TFF, hivyo
iwe isiwe ni lazima klabu isani na ndio sababu alifanya hivyo miezi minne
iliyopita na klabu kupewa mil 100.
Akiweza wazi Rage alishangazwa kusikia Joseph
Itang’ale na Evans Aveva kushiriki katika mazungumzo Zook na kubainisha kuwa
yuko tayari kujiuzuru ikiwa Zouk watatoa mil 700.
Post A Comment: