Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na Mjumbe wa UN. Ikulu JIji Dar es Salaam |
Mary Robinson Mjumbe
Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika
amewasili nchini Tanzania, akiwa katika safari ya kiduru itakayochukua muda wa
wiki moja katika nchi za eneo hilo.
Mara baada ya kuwasili
mjini Dar es Salaam, Bi Robinson ameunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa kwa
ajili ya kurejesha amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aidha mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, analipa kipaumbele
kwenye safari yake hiyo suala la kufikiwa kwenye tija na mazungumzo ya amani
kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 huko Kampala Uganda.
Taarifa zinasema kuwa,
jana Bi Robinson alikutana na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, ambapo nchi hiyo
hivi sasa inaongoza kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachopambana na makundi ya
waasi mashariki mwa Kongo. Imeelezwa kuwa, mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa
katika eneo la Maziwa Mkuu ya Afrika leo ataelekea Rwanda na baada ya hapo
ataelekea nchini Kongo Brazzaville.
Post A Comment: