Ujerumaini imeamua kupiga marufuku simu
zote za "smart" aina ya iPhone baada ya afisa mmoja wa zamani wa
kijasusi wa Marekani Edward Snowden kufichua kuwa, simu aina hiyo zilitumika
kufanyia ujasusi mazungumzo ya simu ya viongozi wa nchi 35 duniani.
Kabla ya hapo ilibainika kuwa, Wakala
wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA ulikuwa unadoya na kudukua mazungumzo ya
simu ya Kansela wa Ujerumaini, Angela Merkel tangu mwaka 2002, ujasusi ambao
umeikasirisha mno Bundestag (bunge la Ujerumani).
Huku hayo yakiripotiwa, wabunge wa
vyama viwili vikuu katika bunge la Ujerumani wamepasisha sheria inayowapiga
marufuku wabunge wa nchi hiyo na viongozi wote wa ngazi za juu serikalini
kutumia simu ambazo hazina kinga ya kufanyiwa ujasusi yaani simu zisizo na
chujio la kudhibiti mawasiliano na barua.
Imebainika kuwa machujio hayo hayawezi
kufanya kazi kwenye simu za "smart" aina iPhone zinazotengenezwa na
shirika la Apple la Marekani na hivyo kuwapiga marufuku wabunge na viongozi wa
ngazi za juu wa Ujerumaini kutumia simu hizo maarufu.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa,
kutofanya kazi programu hizo zinazokusudiwa na wabunge wa Ujerumaini
ambazo zinachuja mazungumzo na barua katika simu ya iPhone kumetumiwa kama
kisingizio tu bali ukweli wa mambo ni kuwa shirika la Apple lina makubaliano ya
siri na Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA yanayoruhusu mawasiliano
yote ya simu za iPhone yapitishwe kwenye chujio linalowasilisha taarifa zake
moja kwa moja kwa wakala huo wa kijasusi wa Marekani.
Post A Comment: