Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeilaumu Uganda kwa kushindwa kufikiwa makubaliano katika mazungumzo kati yake na waasi wa Machi 23.

Lambert   Mende  Msemaji wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Lambert Mende msemaji wa serikali ya Kongo amesema kuwa Uganda inajifanya kama sehemu ya mgogoro wa Kongo na kwamba hakuna nchi yoyote katika historia iliyosaini makubaliano na kundi lolote lililojitangazia kuvunjika.

 Kwa upande wake Luteni Kanali Paddy Ankunda msemaji wa timu ya usuluhishi ya Uganda ametetea nafasi ya Kampala katika mazungumzo kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa harakati ya M23 na kueleza kuwa Uganda inasalia kuwa mshiriki pekee wa kutumainiwa wa Kongo. Amesema kile kinachoidhuru Kongo kinaiathiri pia Uganda.

 Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa Machi 23 yaliakhirishwa hapo jana baada ya ujumbe wa serikali kutofika mahala palipopangwa kutekelezwa utiaji saini wa makubaliano kati ya pande mbili hizo. Serikali ya Kongo imetangaza kuwa, kunahitajika muda zaidi kwa ajili ya kuweka wazi baadhi ya vipengee vya makubaliano hayo.
Axact

Post A Comment: