![]() |
TUNDU LISU |
Maneno
hayo mazito yalitamkwa na Mheshimiwa Tundu Lissu, Waziri Kivuli wa Sheria na
Mnadhimu Mkuu wa “Kambi Rasmi” ya Upinzani Bungeni wakati akitoa hitimisho lake
siku ya Jumapili ya Oktoba 27 mwezi huu katika Mdahalo Maalum juu ya Mchakato
wa Katiba Mpya uliopewa jina la “Tanzania Tuitakayo”.
Mdahalo
husika uliomhusisha pia Msomi kutoka Zanzibar Dk. Nassor Aboud Alley na
kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam uliendeshwa na Mwandishi
Rosemary Mwakitwange na kurushwa hewani na Vituo vya ITV na Radio One.
Mdahalo
huo uliofana sana, ulijadili mambo mbalimbali yaliyohusu mchakato wa Katiba
mpya, Muundo wa Muungano na nafasi ya wananchi na vyama vya siasa katika Bunge
la Katiba, japo Mwakilishi wa Serikali katika mdahalo huo, Anjela Kairuki
hakutokea kwa sababu ambazo hazikuelezwa.
Nilisikiliza
mdahalo husika kwa kina, baada ya kuyatafakari yaliyonenwa kwenye mdahalo nami
nimeona niseme machache kutokana na hayo yaliyozungumza. Niseme tu kwamba kwa
kirefu machache yangu haya yatajikita, pamoja na mambo mengine, kwenye hilo
hitimisho la Mwanasheria mbobezi Tundu Lissu katika mdahalo ule.
DHORUBA
ZA MUUNGANO NA UWEPO WA CHAMA KIMOJA
Ziitwazo
dharuba za Muungano ni matukio mbalimbali ya mikinzano na mikingamo juu ya
masuala kadhaa ya Muungano ambayo kilele chake kilikuwa ni “kulazimishwa
kujiuzulu” nafasi zote uongozi, ndani ya Chama na Serikali, kwa Mwalimu Aboud
Jumbe Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
Ni
tukio hilo la mwaka 1984 ambalo lilizalisha kitabu cha Mwalimu Jumbe “The
Partnership: Miaka 30 ya Dhoruba” kilichotolewa mwaka 1994 ambacho kwa kirefu
kilijikita kwenye kuzieleza hizo dhoruba za Muungano ndani ya hiyo miaka 30
(1964-1994) ya Muungano.
Kitabu
husika ni mawazo ya Mwalimu Jumbe juu ya Uzoefu wake serikali, misingi na
migongano ya kisheria juu ya Muungano na hata kadhia mbalimbali juu ya
kuongezwa mambo ya Muungano kutoka yale 11 yaliyo kwenye Hati ya Muungano.
Miongoni
mwa kadhia hizo ni pamoja na Kitendo cha Rais Nyerere na Rais Karume, waliokuwa
waasisi wa Muungano huu, kukaa kwa kipindi cha Mwaka mmoja wakiwa hawapikiki
chungu kimoja na hawasemezani. Rais Nyerere akitaka kuongea na Rais Karume
anamtumia Bhoke Munanka na Rais Karume akitaka kuongea Rais Nyerere anamtumia
Mwalimu Aboud Jumbe.
Matukio
na kadhia kama hayo na nyengine za aina hiyo ndizo ambazo kwa kirefu
zinaonyesha dhoruba ambazo nyenzo hii ya kuendeleza Umoja wetu (Muungano)
ilikumbana nazo na ikapita salama.
Tukio
la Mwalimu Aboud Jumbe kuondolewa madarakani kupitia vikao vya Chama kwa sababu
ya misimamo yake juu ya Muungano lina mengi ndani yake ambayo hayasemwi, kubwa
kati ya hayo ni dhamira ya Mwalimu Jumbe juu ya misimamo hiyo “iliyoonekana
kuzuka ghafla” juu ya Muungano.
Historia
inamuonyesha Mwalimu Jumbe kama mtetezi mkuu wa Muungano na mtu ambaye
ameufikisha Muungano huu hapa ulipo. Ni yeye ambaye aliishi Tanganyika (Mara)
kwa muda mrefu zaidi akimsaidia Rais wa Muungano majukumu mbalimbali ya
kuendesha nchi huku akiiacha Zanzibar ikiongozwa na Waziri Kiongozi, Brigedia
Jenerali Ramadhani Haji Faki. Ni Mwalimu Jumbe ambaye aliunganisha Chama chake
cha ASP na Tanu cha Nyerere na kuasisi CCM.
Wakati
wa kuundwa kwa Muungano huu Vyama vya siasa havikuwa katika moja ya mambo ya
Muungano, hivyo vyama vya ASP na TANU bado vilibaki kama vyama tawala katika
pande mbili za Muungano kwa muda wa miaka 13 ya mwanzo ya Muungano (1964-1977).
Hivyo kauli ya Tundu Lissu kuwa Muungano huu wa Serikali mbili umedumu kwa
sababu ya uwepo wa Chama kimoja si sahihi sana kwa kuwa hakukuwa na Chama
kimoja kwa muda wa miaka 13 ya mwanzo ya Muungano na bado Muungano ulidumu.
Dalili
za kutokudumu kwa muundo wa muungano tulionao sasa ambazo zimejitokeza
hazitokani na kukosekana kwa uwepo wa chama kimoja bali ni kwa sababu ya
kupuuzwa kwa haja ya maboresho ya muungano huu kwa miaka nenda rudi,
ushirikishwaji mdogo wa wananchi, muundo husika kutokuwa wa haki na usawa nk.
Kwa
hali ya sasa ilivyo hata kama bado kungekuwa na chama kimoja bado tishio la
kutokudumu kwa Muungano lingekuwepo tu, maana hata tishio la kuvunjika Muungano
lililokuwepo mwaka 1984 halikuweza kutokuwepo hata pamoja na uwepo wa hicho
chama kimoja.
Tukio
la kushindwa kwa hoja juu ya Muundo wa Muungano wakati ule wa kadhia ya Mwalimu
Jumbe si kwa sababu ya uwepo wa Chama kimoja bali ni kwa kuwa hoja husika
haikujengwa na dhamira safi katika wakati ule. Madai ya kina Jumbe yalijificha
nyuma ya dhamira chafu ya kutaka Zanzibar yenye Mamlaka zaidi kwa lengo la
“kutaka kujipa uwezo” wa kuwadhuru vijana wapenda mabadiliko (Frontliners) na si
kuwapa Wanzanzibari fursa zaidi.
Katika
Mdahalo husika alikuwepo pia Mzee wetu Njelu Kasaka, Kiongozi wa Wabunge 55 wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Tanganyika ambao waliibua hoja
ya kutaka uwepo wa Serikali ya Tanganyika katika muundo wa Muungano Bungeni.
Kundi hilo ni maarufu zaidi kama G55.
Tukio
la kuzuiwa kwa Wabunge hawa kutimiza dhamira yao hiyo na Mwalimu Nyerere
linatajwa kama msingi mkuu wa kuonyesha nguvu za Chama kimoja katika kudumisha
Muundo wa Muungano uliopo sasa kwa mabavu. Lakini wajengao hoja hiyo
hawatuonyeshi kwanini sasa ambapo kuna vyama vingi tofauti hakujaibuka kundi la
wabunge hata nusu ya idadi hiyo ya G55 kutoka Tanganyika ambao wangejenga hoja
juu ya kuihuisha Tanganyika katika muundo wa sasa wa Muungano.
Kwangu
kuzuiwa kwa G55 kilikuwa ni kitendo cha busara na hekima zaidi kilichowahi
kufanywa na Mwalimu Nyerere. Dhamira ya G55 haikujengwa juu ya haja ya
kuboresha na kujenga Muungano wa haki na usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar
bali ni juu ya mhemko wa kitendo cha Zanzibar kujiunga na OIC. Hapakuwepo na
hali ya kupelekea “muafaka” bali kulikuwa na hali ya kutaka kukomoana, na hoja
ile ingeruhusiwa wakati ule tusingekuwa na Muungano huu adhwimu sasa.
Hivyo
hapa hoja ya kuwa kilichozuia ni chama kimoja si sahihi, kwa kuwa wakati husika
tayari tulikuwa na vyama vingi, na wabunge hao wa G55 walipewa fursa ya
kujiunga na vyama vingine ambavyo vitakuwa na sera ya kuihuisha Tanganyika
tofauti na CCM.
“KINA
LUMUMBA WETU”
Mwaka
1969, raia kadhaa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao waliwahi kuwa
Viongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano “walipotezwa” (kuuawa) kidhalimu katika mazingira ya kutatanisha.
Raia
hao ni pamoja na Abdullah Kassim Hanga, Abdulaziz K. Twalla, Saleh Sadalla,
Othman Sharifu Mussa na Mdungi.
Siku
kadhaa zilizopita, wakati wa maadhimisho ya miaka 14 ya Kifo cha Mwalimu
Nyerere niliandika makala katika gazeti la “Sura ya Mtanzania” iliyokuwa na
kichwa cha habari “Nyerere aliokoa maisha yetu” (Makala husika pia inapatikana
hapa kwenye wall yangu kwa kwa kichwa cha habari “Nyerere alituokoa”). Kwa
kirefu makala husika ambayo ni sehemu ya masimulizi ya Komredi Ali Sultan Issa
kutoka katika kitabu “Race, Revolution and Struggle for Human Rights in
Zanzibar: Memoirs of Ali Sulatn Issa & Maalim Seif Sharrif Hamad”, imeeleza
juu ya matukio yawahusuyo raia hao wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
waliopotezwa (kuuawa) kwa dhulma na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makala
husika ilieleza jambo moja lililo dhahiri, kuwa kuuawa kwa hao wote hakukuwa ni
kwa sababu walikuwa wanapinga Muungano, bali ni kwa sababu walikosana na Karume
(wengine hata kabla ya Mapinduzi) na baadhi ya wajumbe wa kamati ya watu 14.
Abdallah
Kassim Hanga alikuwa adui kwa Sheikh Abeid Amani Karume kama alivyokuwa adui
Oscar Salathiel Kambona kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Uadui huo haukuwa
ni kwa sababu wawili hao (Hanga na Kambona) walipinga Muundo wa Serikali mbili
wa Muungano wetu bali ni kwa kuwa walikuwa tishio kwa utawala wa Karume na
Nyerere.
Siamini
kama Tundu Lissu haijui historia hii ya mauaji ya kidhalimu ya “Kina Lumumba
Wetu” hawa, Abdallah Kassim Hanga, Mdungi, Othman Sharifu Mussa na wenzao,
kiasi cha kuyahusisha mauaji haya na suala la kupinga Muundo wa Muungano huu wa
Serikali mbili usio wa haki na usawa, naamini lengo lilikuwa ni upotoshaji ili
kufikia matlaba.
“KIZUIANI”: UBAYA WA SHERIA NA MAZINGATIO YA MAZINGIRA NA NYAKATI
“KIZUIANI”: UBAYA WA SHERIA NA MAZINGATIO YA MAZINGIRA NA NYAKATI
Mara
baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Aboud Jumbe Mwinyi pamoja na Wasaidizi
wake kama Aboud Maalim na Brigedia Jenerali Ramadhani Haji Faki, aliwekwa kwa
muda katika makazi maalum Kigamboni, Jijini Dar es salaam kwa lengo la
kujiepusha na “athari za ushawishi wake kwenye utulivu wa siasa za Zanzibar”.
Msaidizi
wake mwengine, Dk. Bashiru Kwaw Swanzy (Mwanasheria aliyeandaa waraka wa Jumbe
uliovujishwa na kusababisha kung’olewa kwake) aliwekwa “kizuizini” kwa muda na
kisha kuvuliwa kabisa Uraia (Ikumbukwe kuwa Kiasili Swanzy alikuwa ni Mghana
mwenye mafungamano makubwa na Zanzibar tokea harakati za Uhuru) na kisha
kupelekwa uhamishoni nchini Uingereza.
Baadaye
Mwanasheria Wolfango Dourado naye aliwekwa kizuizini kwa sababu hiyo ya
kuuzumza hadharani msimamo wake juu ya kupinga muundo wa Muungano huu wa
Serikali mbili.
Kwa
Msaada wa Vyanzo kotoka Z’bar
Post A Comment: