Kufuatia kuzingirwa na wanamgambo wenye silaha wako
kwenye hatari ya kupata maradhi yatokanayo na maji machafu ikiwa hawatapata
msaada wa haraka wa kibinadamu, lilionya Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya
(KRCS) siku ya Jumanne (tarehe 26 Novemba).
Wanajeshi wakijiandaa kwenda kuwaokoa watu walio zingirwa. |
Shirika la KRCS limesambaza msaada wa chakula na mengine
iliyochangwa na serikali ya Kaunti ya Turkana kwa familia zilizookolewa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa huko, Lucas Ngasike,
hali ya utulivu imerejea kwenye eneo hilo lakini licha ya kuwepo kwa jeshi,
kuna wasiwasi sana.
Aliiambia Sabahi kwamba kulikuwa na hofu kwamba watu wa
jamii ya Pokot nchini Uganda walikuwa wanapanga kuivamia jamii ya Turkana na
kuwatoa kwenye eneo hilo, na matokeo yake jamii ya Turkana wanajihami kwa
silaha.
Lakini msemaji wa polisi ya Kenya, Zipporah Gatiria
Mboroki, alisema mzingiro wa kijiji hicho ulimalizika pale wazee wa huko
walipoingilia kati na kuwashawishi wanamgambo kujiondoa.
"Utulivu umerejea na barabara imefunguliwa na hakuna
mtu aliyejeruhiwa," alisema na kuongeza kwamba polisi bado walikuwa
wanaondosha miti iliyowekwa njiani kuzuia kijiji hicho kufikika.
Shirika la KRCS limeitolea wito serikali ya Kenya kuunga
mkono suluhisho endelevu kwa mzozo huo kati ya jamii hizo mbili, ikiashiria
kwamba mgogoro huo si jambo jipya, kiliripoti kituo cha Capital FM cha Kenya.
Post A Comment: