Ni msimu mwingine tena ambapo wakristo kote Duniani wanasherekea kuzaliwa Mkombozi Yesu Kristo aliyefariki zaidi ya miaka 2000 ilyopita.
 
Katika msimu huu, ni msimu ambao wakristo wanakuwa wanakumbuka kuzaliwa kwa mokozi Yesu Kristu, ambaye alileta ukombozi Duniani kwa kumwaga damu yake pale msalabani kwa ajili ya dhambi za waliowengi.
 
Tunapo azimisha sikukuu hii kubwa kama Wakristo kuna mambo ya muhimu ya kujifunza na kutafakari wapi tulikuwepo, wapi tulipo na je! Ni wapi tunataka kwenda kwa maana aina gani ya maisha ambayo tunayachagua kama wakristo.
 
Ni kweli kwamba Kristo alikufa kwa ondoleo la dhambi je! Tuyaishi maisha ya kumpendeza Mungu? Je tunapo sherekea sisi kama wakristo tumejihoji tunawatendea vipi wenzetu? Dini safi ni ile yenye kujali Yatima na wajane pamoja na wenye uhitaji, umesha jiuliza moyoni mwako kwamba ni mara ngapi umewasaidia wahitaji? Haya ni baadhi ya Mambo mengi kama mwana jamiii unatakiwa kujiuliza ili uweze kuishi maisha ya kumpendaza Mungu.
 
Lakini mbali na hilo, Hebu tuangalie nafasi zetu ambazo tunazo katika Jamii zetu kwa maana kwamba kila mmoja amepimiwa kulingana na mapenzi ya Mungu, wewe ni karani, mwingine ni waziri na Mwingine ni Mvuvi lakini pia mwingine anaweza kuwa mtoza ushuru, kwa nafasi ambazo nimezitaja hapo jipime wewe mwenyewe je umetenda vipi katika dhamana uliyopewa?
 
Kila dhamana mtu aliyopewa ina mshahara wake na malipo yake, wewe umepewa uongozi katika Serikali kwa ajili ya kuwahudumia watu je! umejiuliza wewe mwenyewe na kujipima kiwango cha huduma unayo itoa na dhamana uliyo nayo? Je hujawa mtu wa kunyanyasa wateja wako?, Mtu mmoja akaniambia unapotoa huduma jaribu kujigeuza kwamba wewe ndiwe mhitaji, mathalani umekwenda hospitalini wewe ni mgonjwa, Daktari au Nesi ajigeuze wewe uwe mgonjwa na Mgonjwa awe wewe kwa maana awe ndiye Nesi au Daktari.
 
Kwa nini nasema hivyo ni kwasababu wapo watu wamegeuka miungu watu ndani ya Ofisi za umma na kuutendea umma nje na mikataba yao ya kazi, fikiria umefika kwenye ofisi ya Serikali lakini mtu anayepaswa kukhudumia anaomba rushwa, anakuwa na majibu yasiyo ridhisha, anakuwa mkali mithili ya simba aliye jeruhiwa nk.
 
Tunapo adhimisha kuzaliwa kwa Noel hili liwe kama Fumbo la Imani kwamba ona aibu kupokea rushwa, Ona aibu kuomba rushwa, ona aibu kutoa huduma kwa vishawishi lakini kumbuka kwatendea wana wa Mungu kile ambacho wewe ungependa kutendewa.
 
Mwisho niwatakie kila la kheri katika kusherekea Krismasi njema "Dini iliyo njema ni ile yenye kuwasidia wenye Uhitaji"
Axact

Post A Comment: