Na Atley Kuni.
Hakuna lisilokuwa na mwanzo likakosa kuwa na
mwisho, wengine wakanena hakuna marefu yasiokuwa na ncha.
Kweli mwisho wa baba Mandela Umefika mwisho
pengine wengi wetu tulipenda aishi hata milele na milele lakini kama maandiko
matakatifu yasemavyo, kila mja atarejea kwake na kuonana ni majaliwa, kwaheri
Tata mandela.
Nachukuwa fursa hii kukuomba msomaji wangu wa
kuninewsblog, wakati Mzee huyu anakwenda kwake aliye muumba sisi tuliobakia
tunacho cha kujifunza, kama sio kumuenzi kwa vitendo baba yetu kwake.
Mengi sana yameandikwa na Vyomo vingi vya
habari na sisi kama kuninews tunaomba japo tuiguse sehemu ya Safari
ya Tata mandela, Mzee huyu ambaye alikuwa kipenzi kikubwa cha Hayati baba wa
Taifa, hata baada ya kifo chake wengi walisema ilikuwa sio rahisi kwa mzee
Madiba kuhudhuria katika msiba ule na hofu kubwa ilikumbwa kutokana na
ukaribu na ujamaa waliokuwa nao hawa wana majumuhi wa Afrika.
Tarehe 26 Novemba 1999, Mzee Mandela alifunga
safari hadi Butima mahali ambapo baba wa taifa alizikwa, alikuja na Ndege ya
Shirika la ndege la Afrika kusini na kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza
kIsha alipata usafiri wa Helkopta na kwenda Butima kijijini kwa baba wa Taifa
kwa ajili ya kwenda kuhani msiba huo wa rafiki yake kipenzi na badeye alirejea
Mwanza na kupanda ndege kurudi kwao Afrika kusini.
Kifo hiki cha Mandela Pengine sasa kinatupapicha
kwamba wana Majumuhi wa Afrika pengine wamekwisha kama sio kubakia wachache.
Nyerere kaenda, Nkwame kaenda, Jommo Kenyatta
kaenda, Haile Silas kaenda, Rais wa kwanza wa Nigeria kaenda, Edward Mondelane,
Samora Mchel na wengine wengi hata akina Mohamad Ghadafi ambao kwetu sisi
tuliona kama watu waliowapenda watu wa Afrika nao hawapo tena
Naweza kuwataja wachache ambao kama bara la
Afrika tunaweza kusema ndio waliobakia, kwani hao wana mawazo chanya juu ya
bara hili nao si wenguine ni Mzee Keneth Kaunda wa Zambia, Robert Mugabe
wa Zimbabwe, Joachim Chissano wa Msumbiji kutaja kwa baadhi.
Haya sasa wanamajumuhi chipukizi wa Afrika kama
Dotto Bulendu kazi ni kwenu kama wasemavyo kampuni moja ya simu hapa Tanzania
kwamba kunani cha kujifunza je! Tuendelee kuishi chini ya Mtego huu wa deni kwa
kunyonywa na kungojea misaadA ya Bwana wakubwa au tuamke sasa wana wa Afrika na
kusema sasa basi.
Tunaposema basi tuya bebe maneno ya rais wa
Marekani Barack Obama alipozulu Afrika kwa mara ya kwanza huko nchi
Ghana, alipo ulizwa na waandishi wa habari kwamba Unadhani nini shida ya Afrika
machafuko hayeshi? alisema " Africa need a strong Institution" Its
our time now to Build the strongest Institution for the benefit of African.
Mwenda kaenda zake Mungu Tubariki Afrika, tuamini
kwamba Binadamu wote ni sawa na tunastahili heshma sawa bila kujali Rangi, Dini
Itikadi za kisiasa,wala Eneo analotoka mtu.
Kila mwenye nia na Afrika ndio apewe kuongoza
nchi na sio mtu ili mradi alikuwa ni rafiki wa Fulani.
Pengine hata hao wanataka kupata uongozi kwa
kupitia mwamvuli wa Dini, Rangi, kabila, Ukanda Washindwe kwa Jina la
Mungu na kamwe tusithubutu kuwakabidhi nchi watu ambao rais wa kwanza wa
Kenya Mzee Jommo Kenyatta aliwaita Nyang'au. Kamwe tusishindwe kuwata
manyang'au kwa sababu wanacho kiangalia wao ni maslahi binafsi na sio maslahi
ya nchi,.
Mzee mandela ameondoka akiwa na miaka 95, kwa
wasomaji wa Biblia inasema umri wa kuishi binadam ni miaka 70 ukiwa na nguvu
80. Lakini Babu huyu aliyetesa ameishi miaka 95 hii si miaka ya kubeza hata
kidogo, pengine alikuwa anawaheshimi sana baba na mama yake Ndio maana akapata
Miaka Mingi na heri Duniani.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA,
kila wakati kumbuka:
Post A Comment: