Nina
wapongeza wananchi waliojitokeza na kujenga Nyumba bora katika
Vijiji hivi vya Nyampanda, Isole na Luchili Wilaya ya Sengerema, lakini pia niwa
ahidi kushirikiana nanyi katika kupata unafuu wa vifaa vya Ujenzi ili muweze
kuwa na nyumba bora.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo wakati
akikabidhi mabati miamoja na ishirini tatu kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema
kwenye Vijiji vya Isole, Nyampande na Luchili yaliyotolewa na Halmashauri ya
Wilaya hiyo kama sehemu ya kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo hayo, ikiwa
ni mkakati wa halamashauri hiyo kutenga bajeti ya Mil.15 kila mwaka kwenye vyanzo
vyake vya ndani.
Ndikilo
alisema ilikuwaboreshea maisha wananchi serikali ya Mkoa haitasita kuwasiliana
na Mheshi,iwa waziri mkuu na wenye viwanda ili wananchi watakaoweza kujenga
maboma waweze kupatiwa mabati kwa bei nafuu ya kiwandaani “ Kama serikali ya
Mkoa tutaona namna nzuri ya kuwasiliana na Mheshimiwa waziri mkuu ili tuweze
kuwasaidia wananchi waondokane na makaazi duni” alisema na kuongeza kuwa “hizi
jitihada zinazofanywa na halmashauri nizakupongezwa kwakuwa hata nchi ya Korea
kusini ambapo viongozi wenu walikokwenda kujifunza nao walikuwa kwenye umaskini
miaka mingi iliyopita lakini kubuniwa kwa mkakati kama huu ndio maana wanachi
hao walifanikiwa kuboresha maisha yao.
Adha
Ndikilo aliongeza kuwa lengo la mikakati kama hiyo ambayo imebuniwa na
Halmashauri ya Sengerema ni mfano wa kuigwa kwa halmashauri zingine za Mkoa wa
Mwanza, “ Ndugu zangu mpango huu ambao Wilaya ya Sengerema imeamua kuufanya ni
dhahiri kwamba hii ni dhamira ya dhati katika kuwaletea wananchi maendeleo”.
Aidha
alisema endepo kama kuna watu ambao ni akina Tomaso kwao kuamini hadi waguse
makovu na Vidonda vya Yesu sasa waje waone jinsi ninyi mlivyonufaika na mpango
huu, maana inasemekana wengine walipokuwa wanaambiwa unajenga nyumba na
serikali inakupatia mabati walikuwa wanadhani ni mzaha sasa leo waje wajionee
hapa kwenu “ Serikali hii ni sikivu iki ahidi inatimiza, alisema mkuu huyo wa
Mkoa na kuongeza kuwa mradi huo kwamba sio wa kilaghai wananchi wakijiunga na
kufyatua matofali wakajenga Halmashauri itawapatia mabati.
Awali
kabla ya hotuba ya mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, alisema Mradi
wa Saemaul Undong ulianzishwa wilayani humo mwaka 2009, ukiwa na vijiji vitatu
vya mfano vya Isole Nyampande na Luchili, kufatia maarifa yaliyopatikana kutokana
na wajumbe Mathew Lubongeja na Ndg Silas B Ntego waliotembela nchini Korea
Kusini kujifunza kwa jinsi wananchi wanavyo ungana katika kuchuochea shughuli mbali mbali za maendeleo na hapo
awali ulijikita kwa kaya ambazo ni masikini sana katika suala la makaazi duni.
Alieleza
kwamba tayari mradi huo ulikwisha nunua mabati 920 na kuyagawa kwa kaya 20 na
kuyagawa kwa wanachi wa kijiji cha Isole na bade mabati 123 yaliyo gawiwa na
Mkuu wa Mkoa kwenye kaya 3 na hivi sasa wannchi wengine wanaendelea na ujenzi.
Kwa
upande wao wananchi walio nufaika na mradi huo walisema wanaipongeza Serikali
kwa kuwajali na kuwa na mipango inayo tekelezeka, Msagwa Kafula ambaye alikuwa
mmoja wa wanufaika wa mpango huo alisema “ Kama serikali ina ahidi na
kutekeleza unadhani sisi tufanyeje siku ishukuru,…, Mhhh.., kuwa kiongozi ni
pamoja na kuwa mbunifu na uthubutu” alisema na kuongeza kama hawa madiwani
wasingethubutu kwenda Korea unadhani wangetoa wapi huu ujuzi? Naye Nestori
Malimbita alisema “ nadhni na wale wengine waliokuwa hawaamini sasa watajua
kwamba ni kweli.
Hata
hivyo pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto zinazo jitokeza katika
kutekeleza mpango huo wa makaazi bora ikiwapo mwamko mdogo kwa wananchi pamoja
na upatikanaji wa rasilimali fedha na mbao, jambo ambali Ndikilo aliahidi
kulipaatia ufumbuzi
Mkuu
huyo wa mkoa alikuwepo Wilayani humo kwa ziara ya kikazi kwa kukagua shughuli
za maendeleo, kuzungumza na wanachi na kusikia kero zao lakini pia kufanya
Mikutano ya hadhara kuelezea Mipango iliyopo ya Serikali katika kuwaletea
wananchi maendeleo yao.
Post A Comment: