Mkuu wa Mkoa wa Mwanza hivi leo amefika Nyumbani kwa wazazi wa mototo aliye uwawa na aliye kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza bw. Clement Mabina  kwa bahati mbaya, tarehe 15.12.2013 katika Kijiji cha kisesa na kuzikwa tarehe 17 mwezi huu katika makaburi wa wananchi wa Kisesa.

Taarifa ambazo Mtandao huu zimepata mara baada ya kutoa salam za pole, mkuu wa Mkoa pamoja na msafara wake walielekea  nyumbani kwa Marehemu Mabina kwa ajili yakutoa salam za pole pia, ambaye naye pia aliuwawa na wananchi baada  ya kusababisha kifo cha  kufyatua risasi iliyo mpata kijana aliye uwawa kwa bahati mbaya.

 Akiwa katika familia ya Marehemu huyo  Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pia ubani kwa ajili ya kusadia shughuli za msiba huo, ambapo alichangia magunia Mawili ya Mahindi pamoja na ubani wa Tsh.160,000/=

Akielezea hali halisi Balozi wa eneo hilo la Kanyama Paul, alisema wao kama wana kijiji wa kanyama Wanaipongeza sana Serikali Mkoani Mwanza kwa juhudi walizo zionesha toka Mwanza wa msiba hadi mwisho wa msiba huo, kwani viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wameshafika katika eneo hilo kabla na baada ya msiba kwa ajili ya kutoa faraja kwa wafiwa.

Aidha Balozi hiyo alimumba Mkuu huyo wa Mkoa kufatilia kwa karibu ahadi iliyotolewa na Vijana wa CCM Mkoa wa Mwanza ya kuhakiksha wanajengea kaburi la Mtoto huyo.

Vivyo vya wawili hao vilitoka na Mgogoro wa muda mrefu wa kugombe mashamba, ambapo wananchi kwa upande wao walikuwa akidai Eneo hilo la Mlima ni la Kijiji, huku naye bw. Clement Mabina (marehemu), akisema yeye ndiye Nyaraka halali la umiliki wa eneo hilo.

Mara baada ya Vuta ni kuvute ya mda mrefu ndipo siku ya tarehe 15.12.2013, Bw. Mabina alipo amua kuwatuma watu kwenda kuweka alama katika Mlima huo wa kanyama, jambo ambalo liliwakera wananchi na kuanza kwakataza waweka alama hao, mara baada kuona hivyo Mabina akiwa na silaha ya Moto aina ya  Shotgun aliamua kwenda yeye mwenyewe na ndipo lilipozuka zogo baina ya pande hizo mbili na katika kujihami Bw. Mabina alifyatua risasi ambayo kwa bahati mbaya ilimpata motto wa miaka 12 na kufariki dunia, kuona hivyo wananchi hao wenye hasira waliamua kumshambulia Mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM Mkoa wa Mwanza hadi umauti ulipo mkuta.

Axact

Post A Comment: