Zaidi ya abia miambili walikuwa wakisafiri na Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia Wamekwama katika uwanja wa Ndege wa Arusha.

Kwa mujibu habari  ambozo mtandao huu zimeupata ni kwmba bado haijajulikana ndege hiyo yenye uwezo wa kuchukua abiria miatatu ilikuwa inaelekea nchi gani.

Hata hivyo hakuna mtu alidhurika katika ajali hiyo kwani, Ndege hiyo ilipitiliza hadi eneo lenye majani katika uwanja huo na hakuna madha yoyote kwa sasa.

Shghuli zinazo endelea hivi sasa nikutafuta ngazi itakayowezesha abiria kushuka kutoka ktk Ndege hiyo kwani kwa mujibu wa Mashuhuda Ndege hiyo iliypotengenezwa Nchini Ujerumani inangazi maalum kwa ajili ya kushushia abiria.

Mtandao huu utaendelea kuwapatia habari kadri zinavyo tufikia.
Axact

Post A Comment: