Na Julius Kithuure,
Nairobi.
MAMBO YA UGATUZI KENYA. |
Francis
Mokaya, ambaye anamiliki duka dogo katika kaunti ya Kisii na majengo matatu ya
ghorofa ya makaazi katika mji wa Kisii, alisema alitarajia huduma mara tu
gavana alipoapishwa kuingia katika kazi mwezi Machi uliopita.
"Nilitumaini
kwamba hadi sasa majosho mengi yaliyoharibika yangekuwa yamekarabatiwa lakini
kwa bahati mbaya, hakuna kilichotokea na inaonekana nitasubiri kwa muda mrefu,"
alisema Mokaya, ambaye pia anamiliki mifugo, kama zilivyo familia nyingi za
vijijini." Sina jinsi nyingine zaidi ya kunyunyuzia dawa mifugo yangu
nyumbani ambayo ni ghali na inatakiwa jitihada."
Majosho
ya ng'ombe, ambayo ni ya kawaida katika maeneo ya vijijini, ni mashimo marefu
ambapo mifugo wanatumbukia katika maji ambayo yana kemikali za kuua kupe na
vimelea vingine.
Mokaya
alisema serikali ya kaunti pia inazuia mapato yake ya kodi kwani haijawahi
kutoa viwango vya kodi kwa huduma na umiliki wa mali, ambayo matokeo yake
inazifanya zishindwe kutoza vizuri wapangaji wake.
Sijui
ni kiasi gani ninapaswa kutoza kwani sijui tozo gani ambazo serikali ya kaunti
[itanitoza] mimi," Mokaya alisema.
Kero
ya Mokaya inawakabili wakaazi wengi nchini kote Kenya. Kaunti nyingi
hazijajadili na kupitisha viwango vya mwisho vya kodi kama ilivyoelezwa katika
miswada yao ya fedha ya 2013, ambayo imewapa mamlaka kusimamia kodi, tozo na
adhabu kwa wasiolipa.
"Inachanganya,
lakini nina matumaini kwamba wajumbe wa baraza la Kaunti watatoa kipaumbele
katika kupitisha miswada hii ambayo imecheleweshwa baada ya [wajumbe wa baraza la kaunti] kugoma
mwezi Novemba kudai kuongezewa mishahara ," alisema Charity
Ngina, mwenye umri wa miaka 37, mfugaji wa kuku huko Nyandarua.
Ngina
alisema ana matumaini ya kuongeza bei yake mara tu serikali ya Kaunti ya
Nyandarua itakapoamua kiasi cha tozo anachopaswa kulipa kwa ugugaji wa ndege.
Kukosekana kwa mipango, uwekaji vipaumbele
Stephen
Manoti, mbunge wa jimbo la Bobasi katika Kaunti ya Kisii, alisema maendeleo ya polepole katika utekelezaji
wa miradi ya maendeleo katika nchi nyingi hutokana na kukosekana kwa
mipango mizuri na uwekaji wa vipaumbele.
"Magavana
wengi na wajumbe wa mabaraza ya nchi hawana nyaraka za kutunga sheria au nakala
kwa ajili ya matamko yao. Malengo yao yalikuwa kwanza kupata mamlaka, kisha
mambo mengine yatafuata -- na hii ndiyo sababu wanapambana kuweka miradi yoyote
ya maendeleo yenye mafanikio, lakini wanahitaji kulenga upya na kuweka
mikakati," aliiambia Sabahi.
Damaris
Wanja, mama wa watoto watatu mwenye umri wa maiaka 51 na mmiliki wa mgahawa
huko Machakos, alisema hakuwa na furaha kutokana na kushindikana kwa maendeleo
katika nchi yake.
"Gavana
wangu, Dkt. Alfred Mutua, ameanzisha miradi ya mabilioni ya shilingi kujenga
mji mpya wa Machakos kuanzia chini. Ninamkosoa kwa hili," alisema.
"Je, tunahitaji jiji la kisasa wakati nchi haina maji ya kutosha [na]
vituo vya afya vipo katika hali mbaya vikiwa na dawa muhimu chache? Hapana.
Tunahitaji miradi ya umwagiliaji kusaidia upatikanaji wa kudumu wa vyakula na
umeme vijijini kuwezesha vijana kuanzisha biashara ndogondogo."
Katika
Kaunti ambazo kuna sera ya kodi, wananchi kama wajumbe wa baraza hawaachi
kushauriana na jamii na kulumbana hadharani kuhusu sera kabla ya kutoa mamlaka
ya kodi mpya.
Serikali
ya Kaunti ya Kiambu imependekeza kuwatoza wakulima kodi ya shilingi 2,000 kwa
kila eka ya ardhi wanayolima, kuleta upinzani kutoka kwa wakulima wadogo kama
David Kariuki mwenye umri wa miaka 43.
"Kodi
hizi na adhabu zinaanzisha vikwazo visivyo vya lazima kwa wafanyabiashara.
Wanaadhibu na kuumiza uwekezaji," aliiambia Sabahi. "Je, wanasema
kuwa ninapaswa kuacha na kutoilima ardhi yangu? Hii si kukatisha tamaa kufanya
kazi kwa bidii na kualika njaa nchini?"
Kariuki
alisema alitarajia serikali kuanza jitihada kama vile za kuwapa wakulima miche
inayotoa mazao mengi, mbolea za msaada na upatikanaji wa kilimo cha kutumia
zana rahisi za kilimo, badala ya kuanzisha "ushuru wa kuturejesha nyuma
kwa ajili tu ya kukusanya fedha zaidi, ambazo hazimfaidishi mtu wa kawaida".
Kariuki
aliliomba bunge la taifa na seneti kubana bajeti na kudhibiti matumizi katika
kaunti 47 na kuanzisha kamati ya usimamizi kufuatilia
matumizi ya kaunti ili "fursa za mabadiliko yaliyokusudiwa kwa
ajili ya watu wa kawaida yasidharauliwe wala kupotea".
Serikali za mitaa zinapaswa kuanzia chini
Hata
hivyo, magavana wa kaunti ambao walizungumza na Sabahi walipinga malalamiko
hayo, wakisema kuanza taratibu ilikuwa ni kwa sababu ya urefu wa muda iliotumia
kupokea rasilimali kutoka katika serikali ya taifa na kupanga miundo ya
serikali za kaunti kwa mara ya kwanza.
Sasa
ofisi hizo na wafanyakazi wake tayari wapo, magavana walisema wapo tayari
kusongesha mbele huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo wananchi
wamekuwa na wakiitarajia kwa shauku, kama vile ujenzi wa barabara, kukarabati
shule, masoko na taasisi nyingine za serikali, uanzishaji wa mikopo isiyo na
riba na misaada, maendeleo ya kilimo na programu za kuanzisha ajira.
Gavana
wa Kaunti ya Meru Peter Munya aliiambia Sabahi anasikitika kwamba maendeleo
yaliyotarajiwa bado hayajakamilika, lakini alizitetea serikali za mitaa,
akisema zilipaswa kuimarisha utawala wake kuanzia chini.
"Ni
kweli bado hatujatekeleza sera yoyote kuhusu kilimo, usafirishaji, leseni za
biashara, usafi wa mazingira, elimu ya shule za awali na vituo vya afya,
ambavyo ni mamlaka muhimu zinazoangukia katika serikali za kaunti,"
alisema.
Lakini
sasa, kwa kuwa na mabaraza ya kaunti yanayofanya kazi, kupitisha bajeti za
mwaka, wafanyakazi na fedha, watu wataanza kuona tofauti na mabadiliko
waliyokuwa wakiyatarajia, alisema Munya.
"Kwa
Hazina ya Taifa kutoa shilingi bilioni 20 (Dola milioni 233) katika serikali ya
kaunti Alhamisi tarehe 16 [Januari], tupo tayari kuanza kutekeleza miradi kama
ukarabati wa masoko, zahanati na barabara," alisema
Post A Comment: