KUFA KUFAANA, HAPA GARI HILI LA MIZIGO LILIGEUKA KUWA LA ABIRIA. |
Bajaji leo inafanya kazi ya kusafirisha abiria badala ya Mizigo. |
Madereva hapa walikutwa nje ya Ofis ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana. |
Mama huyu alilazimika kulipa kiasi cha Tshs 5000/= kwa safari ya Mjini kati hadi uwanja wa ndege, kwa kawaida nauli ya daladala ni sh. 400. |
Mama hapa akiwa na Wanawe akiwa anapatana Bei ya kusafiri kwa Pikipiki kati ya Mjini kati Eneo la Idara ya maji kwenda Uwanja wa Ndege Mwanza. |
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Jiji Mwanza akizungumza na Bw. Ashirafu Mmoja ya madereva waliogoma. |
Hapa tunalazimika kufanya kazi kwa kificho, maana tumewasiliti wenzetu. |
·
Safari hii ni wenye dala dala.
·
Walalamikia Udogo wa Vituo vya daladala na Faini
kubwa kwakukiuka taratibu.
Katika hali inayo onekana
kuendelea kwa migomo katika Jiji la Mwanza, na habari ambazo ni (habari mpasuko)
zinazo tufikia hivi sasa, wenye daladala katika Jiji la Mwanza wamegoma kutoa
huduma katikati ya Jiji hilo huku wakishinikiza Mamlaka husika kuchukua hatua
za haraka ili kuondoa tatizo lililopo.
Mwandishi wetu ameshuhudia
misafara ya watu, wakitembea kwa miguu kutoka viunga mbali mbali vya Jiji hilo,
Barabara bara ambazo zimeoneka kuwa na watu wengi ni ile itokayo maeneo ya
Nyakato, Igoma, kuingia Jijini humo maarufu kwa jina la “Nyerereroad”, barabara
nyingine zingine ni ile itokayo Nyegezi na maeneo ya Chuo kikuu cha Mtakatifu
Augustino kuingia Jiji humo ijulikanayo kwa Jina la “Kenyatta road”na Baraba iliyo
shuhudiwa kuwa na misafara ya watu wengi ni pamoja na ile itokayo Airport
kuingia katikati ya Jiji maarufu kwa jina la “Makongoro road”.
Katika kutaka kujua kulikoni,
mwananchi mmoja aliye fahamika kwa jina la Antony Mkaima, ameuambia mtandao wa kuninews.blogspot.com kuwa, chanzo kikuu cha mgomo huo,
ni eneo dogo la kituo ambalo daladala hizo zimetengewa katika eneo la Igoma na
hivyo kufanya msongamano mkubwa ambao huwalazimisha madereva wa daladala
kuvunja sheria za usalama bara barani ikiwa ni pamoja na kuegesha magari bila
utaratibu katika eneo hilo na pindi wanapovunja taratibu hizo za usalama
barabarani hutozwa tozo ya shilingi za kitanzania Elfu sitini (60,000/=), jambo
ambalo limepingwa na wamiliki wa vyombo hivyo wakidai ni kutowatendea haki, Na
kuzitaka mamlaka husika kuweka mazingira mazuri ya kuegesha magari yao kwa
nafasi ndipo waweze kuendelea na kutoa huduma hiyo muhimu kwa wananchi la si
sivyo wataendelea na mgomo huo.
Kugoma kwa daladala huko, kumetoa
mwanya kwa magari madogo yasiyo rasmi kwa abiria, Bajaji za Mizigo, Pikipiki
kutumika kama njia mbadala ya usafiri, jambo ambalo imeonekana kuwa hatari,
kwani vyombo hivyo si rasmi kwakubeba abiria lakini pia weledi wa madereva wa
vyombo hivyo bado si wakutumainiwa kwani baadhi yao hawana Leseni zinazo
waruhusu kuendesha abiria.
Katika siku za hivi karibuni Jiji
la Mwanza limekuwa likikubwa na migomo ya mara kwa mara, huku mgomo mwingine
ukiwa ni ule ulio wahusisha baadhi ya wafanya biashara wa jumla katika Jiji
hilo ambapo waligoma wakishinikiza Serikali kuangalia upya matumizi ya mashine
za kielektroniki katika ulipaji wa kodi.
Juhudi za kuwapata mamlaka ya
usafiri wan chi kavu na majini SUMATRA zinaendelea na pindi tutakapo zungumza
nao tutawapatieni kilicho jiri na hatua madhubuti zilizo chukuliwa katika
kumaliza mgomo huo
Jiji la Mwanza linalokuwa kwa
kasi miongoni mwa miji iliyoko kusini mwa
jangwa la Sahara, ambao kwa hivi sasa unakadiriwa kuwa na watu Mil. 2.7,
pamoja na shughuli zingine za kilimo, Uvuvi, Madini na Viwanda suala la
Biashara ni moja ya sekta muhimu kwa uchumi wa Mkoa huo wa pili katika
kuchangia pato la taifa, kwani kwa mujibu wa takwimu Mkoa huo kwa sasa huchangia
kiasi cha asilimia 9.15 kwa mwaka 2012
ukitanguliwa na Dar es salaam ambao ulichangia kwa asilimia 16.93.
Kutokana na hali hiyo wadadisi wa
mambo wanasema migomo kama hiyo huenda kwa namna moja au nyingine ikasababisha
kushuka kwa uchumi wa Mkoa kwani shughuli nyingi za uzalishaji mali zitakwama
na hivyo kuathiri hata ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa.
Imeandaliwa na Atley Kuni - Afisa
habari Mkoa wa Mwanza.
Post A Comment: