Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Ghalib Billali, alipokuwa akifungua kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa.

Makam wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na mmoja ya wawekezaji kutoka Kampuni ya AURIC Air, ambao nao ni washiriki katika Kongamano hilo.



Makam wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Gharib Bilal, akiongea na Mkurugenzi wa T.I.C nchini, Bi Julieth Kairuki.



Makam wa Rais hapa akingalia mabanda wakati wa Kongamano hilo.



Makam wa rais hapa akikagua moja ya mabanda ya wajasiriamali wazalendo.

Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza. Elibarick Mmari, Makam wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdalah Kigoda wakishangaa jambo.

Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Makam wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania.

Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikillo, Makam wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr. Mohamed Billali, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sir. George Kahama na Balozi wa Afrika kusini.

Jamani tunakwenda kwenye majadiliano, tujitahidi kuwashawishi hawa wawekezaji hadi waikubali kanda yetu.

Huduma zenu hapa ni zipi?

Balozi wa Afrika kusini nchini, hawa amakweli itabidi tuwahimize wananchi wetu kuja kuwekeza huku. Nchii hii ina amani sana.


Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuondoa urasimu,miundombinu ya uhakika, amani na utulivu na suala la kutokomeza rushwa ili kuwafanya wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza katika nchi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Billal Jijini mwanza alipokuwa akifungua kongamano la uwekezaji kwa mikoa sita ya Kanda ya Ziwa.

Akifungua kongamano hilo Dr. Billali amesema pamoja na mambo mengine, Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ambayo yatawafanya wawekezaji kufurahia kuwekeza katika Nchi ya Tanzania.

Dr. Billali amesema ni dhamira ya serikali ni kuhakikisha serikali inaweka mazingira mazuri yakuwavutia wawekezaji na kuwafanya wawekezaji kufurahia kuwekeza, “ Napenda nielezee kwa kifupi juhudi zinazofanywa katika kuwavutia wawekezaji hususan wa kanda ya ziwa” alisema na kuongeza kwamba mikoa ya kanda ya ziwa ndio mikoa inayopakana na za jirani za maziwa makuu, hivyo ni fursa muhimu kwa nchi kuiona kanda hiyo na kuiwekea mazaingira mazuri na yenye kuvutia kama miundo mbinu imara, na kwamba  hadi sasa mikoa hiyo ndiyo inayobeba idadi kubwa ya watu, na kutaja kuwa idadi yake inafikia Mil.15 takriban theluthi Moja ya watanzania wote ya wapatao Mil. 45. Kwa sasa.

Awali akitoa salam kwa niaba ya Wenyeviti wenza, mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikillo, alisema mikoa ya kanda ya ziwa ndio kitovu kikubwa cha biashara kwa nchi za maziwa makuu, lakini ndio mahali ambapo kuna fursa nyingi  kama za Madini ambayo huchangia kwa asilimia 4 ya mapato ya nchi, kilimo ambacho hutegemewa kwa asilimia 80 ya wananchi wote lakini pia ametaja kanda ya ziwa kuwa na mifugo mingi ambayo bado ufugaji wake sio ule wenye tija, hivyo kuwepo kwa kongamano hilo itakuwa kama “Platform” ya kujitangaza kwa wawekezaji.

Kwa upande wake waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdalah Kigoda, alisema  suala la uhamasishaji ni jambo moja na suala la kuwekeza ni suala jingine, hivyo sisi kama serikali hatuna budi kuhakikisha vile vikwazo vya uwekezaji kama urasimu usio wa lazima unaondoka, kodi nyingi, maamuzi ya kuchelewa, utoaji wa vibali vya ardhi na mengine mengi tunaviondosha, “ tutakuwa nyuma kwa maana hiyo lazima tuvitokomeze vikwazo vyote alisema na kuongeza, kuwa, katika siku za hivi karibuni nchi ya Tanzania imeshuka katika suala la uchumi kwa sababu sekta binafsi haijapata mashiko vya kutosha.

Naye mwenyekiti wa kongamano hilo, Sir. George Kahama, kabla ya kuanza kwa kongamno hilo, alisema amefurahishwa sana na kongamano hilo kwani ni kongamano lililo mkumbusha mbali, huku akisema kihistoria mikoa yote sita iliyo andaa kongamani hilo hapo zamani ilikuwa ni mkoa mmoja, ukijulikana kama (Lake Province) na badae kugawanyika na kutengeneza (West and East Province). Hivyo  kukutanishwa na kongamano hilo ni historia nyingine inayo andikwa kwa mikoa hiyo sita ya kanda ya ziwa. Akasema kupitia kongamano hilo isiwe mlango tu wakujitangaza bali pia kuhakikisha wawekezaji wanatimiza azma yao yakuwekeza Tanzania  na hususani kanda ya Ziwa.


Wengine tulikuwa twapunga
kaupepo ka Beach kidogo.
Kongamano la uwekezaji kwa kanda ya ziwa ni kongamano linalo kutanisha mikoa ya Mwanza Shinyanga, Kagera, Geita, Simiyu na Mara, mikoa inayotajwa kuwa na idadi kubwa ya watu na ambayo inafursa nyingi za uwekezaji kuliko kanda yeyote hapa nchini na litafanyika kwa siku tatu Mfulululizo.

Hata hivyo kabla ya kufungwa kwa mijadala ya majadiliano hayo, Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini Bi Julieth  Kairuki alitiliana saini mikataba ya uwekezaji kwa kanda ya ziwa na Wakuu wa Mikoa ya kanda hiyo.

Kongamano hilo la siku tatu la uwekezaji linakutanisha mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao, Mwaziri, Wawekezaji wakubwa kutoka mbali mbali duniani.

 

 

Axact

Post A Comment: