KINANA AKIHUTUBIA WANANCHI HUKO SUMBAWANGA. |
Katika safari iliyomchukua zaidi ya saa tisa, Kinana na msafara wake alikumbana na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara kutoka Namanyere hadi kwenye vijiji vya kata hiyo kutona na magari kunasa mara kwa mara kwenye tope na makorogoro kwa kuwa barabara haijapata kufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu.
Kufuatia kujionea changamoto hiyo, Kinana amewambia wananchi wa vijiji vya Wampembe na Ntemba, kuwa ataishauri serikali kuifanya barabara hiyo iwe chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) badala ya sasa ambapo ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na hivyo kuwa vigumu kupatikana fedha za kutosha kujenga barabara hiyo. Pichani Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Wampembe, jana,Aprili Mosi, 2014. Na zinazoendelea ni picha zaidi za ziara hiyo na changamoto hizo alizokumbana nazo kama zilizvyopigwa na Bashir Nkoromo aliyeko kwenye ziara hiyo.
Kinana akizungumza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Wampembe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Wananchi wa Kijiji cha Wampembe wakijimwayamwaya kwenye mkutano wao na Kinana
Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Pamoja naye ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka akimpa maelezo.
Kinana akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Nyuma yake ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka
Kinana akiwafurahia vijana aliowakuta wakifanya kazi katika kijiji cha Wampembe kilichopo kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi. Vijana hao wanafanyakazi katika sekta ya afya na ujenzi
Kinana mama, baba na watoto wakimpokea kwa hamasa kubwa Kinana katika kijiji cha Wampembe
Kinana akizungumza na wananchi saa mbili usiku, baada ya kuzuia msafara wake eneo la kijiji cha Ntemba kaya ya Kate akitoka Kata ya Wampemba kwenda Sumbawanga mjini
Wananchi katika kijiji cha Ntemba Kata ya Kate wilayani Nkasi wakimsikiliza Kinana, alipoamua kuzunguza nao baada ya kumzuia njiani akitoka Wapembe kwenda Sumbawanga
CHANGAMOTO ZA BARABARA
Kinana akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara wake kunasa kwenye pori la akiba la Nkasi, wakati Kata ya Wampembe
Kinana akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara wake kunasa kwenye pori la akiba la Nkasi, wakati akitoka Kata ya Wampembe
Kinana (kulia) akitazama moja ya gari la msafara wake ambalo lilinasa porini katika harakati za dereva kujaribu kukwepa eneo baya kwenye barabara katika pori la akiba la Nkasi, wakati akienda Kata ya Wampembe
Gari la polisi waliokuwa wakisindikiza msafara wa kinana likisukumwa baada ya kukwama katika barabara ya kutoka Wampemba kwenda Namanyere wilayani Nkasi
Kinana akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete walipokuwa wakitembea kwa miguu baada ya kushindwa kupita kwa magari katika eneo korofi la barabara
MTI WA NGUVU ZA KIME
Waandishi wa habari kwenye msafara wa Kinana akishangaa mti ambao unakarinia kuanguka kutokana na kumegwa vbanzi na watu wanaoamini kwa vibanzi kutoka mti huo ni dawa ya nguvu za kiume. mti huo upo pembeni mwa barabara ambako magari ya msafara wa Kinana yalinasa wakati wa kwenda na kutoka kijiji cha Wampembe.
Jamaa akigema kibanzi kwenye mti huo. Imetayarishwa na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
Post A Comment: