MWALIMU
wa kujitegemea ambaye pia aliwahi
kuwa Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania(KKKT) mkaoni hapa , Nicodemus Mhana (
umri wa zaidi ya miaka 50) anakabiliwa na kashfa ya
kubaka mwanafunzi wa darasa la 4(jina lake
pamoja na jina la shule anakosoma vinahifadhiwa).
Habari
zilizothibitishwa Jeshi la Polisi pamoja na
mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msumbiji
katika Kata ya Pasiansi Wilayani Ilemela,
Fortunatus Cheneko, zinasema Mhana anadaiwa kutenda
unyama huo Machi 4 mwaka huu.
Hata
hivyo, inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa
Machi 19 mwaka huu na Polisi katika
kituo kikuu cha Wilaya ya Ilemela (Kituo
cha Polisi Kirumba), siku chache baada ya
baba mzazi wa mwanafunzi huyo kutoa taarifa
ingawa pia alipewa dhamana siku hiyo hiyo
kwa madai kuwa ana undugu wa karibu na
maofisa kadhaa wa Jeshi la Polisi.
Kwa
mujibu wa habari, Mhana alifanya
ubakaji huo wakati akiwa na mwanafunzi huyo
katika kituo chake cha masomo ya ziada
kilichoko katika mtaa wa Msumbiji.
Inadaiwa
kwamba Mhana ambaye mara kadhaa
amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya
wananchi wa Mtaa wa Msumbiji kutokana na
tabia yake ya kupenda kurubuni watoto (wa
kike) wadogo kwa nia ya kufanya nao mapenzi, alivuliwa
Uchungaji miaka kadhaa iliyopita kutokana
na kukiuka taratibu pamoja na maadali ya kanisa .
“
Cha kushangaza ni kwamba mtuhumiwa alipewa
dhamana siku hiyo hiyo. Inagwa yeye(mtuhumiwa ) huku
uraiani anatamba kuwa hawezi kufikishwa
mahakamani kwa sababu ana ndugu zake wa
karibu katika jeshi la Polisi ambao ni
wamezaliwa katika mkoa wa Singida” alidai baba
mzazi wa mtoto huyo, Fredrick Mariba, wakati
alipoulizwa na JAMHURI , jana.
Anadai
kuwa alichelewa kubaini kuwa mwanaye
huyo mwenye umri wa miaka 11 amebakwa kwa
sababu baada ya kufanyiwa unyama huyo mtoto
huyo hakuweza taarifa kwa wazazi labda kwa
kuogopa kuadhibiwa , hadi alipohojiwa na mama
yake wa kambo pamoja na bibi yake kutokana
na kulalamika maumivu hasa anapokwenda kujisaidia chooni.
“
Ilibainika siku moja baada yab kwenda
kujisaidia chooni ambapo alisikika
akilia. Na ndipo bibi yake
alipomuuliza na kisha akamkagua sehemu
za siri na kubaini kuwepo kwa
michubuko” alisema na kuongeza kuwa baada ya
kuhojiwa kwa kina mtoto huyo alisema aliyekuwa mwalimu
wake kabla ya kuanza darasa la kwanza, yaani mwalimu
Mhana ndiyo alimlazimisha kufanya mapenzi.
Huku
akibubujikwa na machozi, Mariba
alilalamika kuwa kitendo cha askari Polisi
kuruhusu dhamana kwa mtuhumiwa huyo kabla ya
kufikisha suala hilo mahakamani kinaweza
kuhatarisha maisha ya mtoto wake.
“
Jambo jingine ni kwamba hadi sasa Madaktari
katika Hospitali ya Mkoa( Sekou-Toure) bado
hawajathibitisha chochote kwa maandishi iwapo
mtoto huyu amebakwa kweli ama la. Kila
nikienda ninambiwa mara Daktari Mkuu hayupo
ama yuko bussy, kitendo ambacho kimesababisha
mwanangu ashindwe kwenda shule kwa zaidi ya
majuma mawili sasa” alisema.
Akizungumza
na gazeti hili nyumbani kwake jana( Machi
27), Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msumbiji,
Cheneko alisema kitendo kinachodaiwa kutendwa na
mchungaji huyo kimezua hofu miongoni
mwa wakazi wa mtaa huo.
“
Kwa ujumla taarifa hizi zimeleta hofu,
hasa kwa wazazi wa wanafunzi
wanaosoma katika shule hii kwa sababu inawezekana
kabisa kuwa wengi wameshabakwa halafu wakanyamaza.
Tunaomba wahusika wafanye uchunguzi
zaidi dhidi ya mwalimu huyu kwani anaweza
kusababisha uvunjifu wa amani hapa mtaani
kwetu iwapo mtuhumiwa ataendelea kutamba
kwamba yeye hakamatiki wala hawezi
kufikishwa mahakamani“ alisema Cheneko.
Cheneko
aliendelea kudai kuwa baada ya
kufuatilia amebaini kwamba kituo kinachomilikiwa na
mwalimu huyo hakina usajili wowote.
Alisema
ameshatoa taarifa hizo katika ofisi ya
Mkaguzi wa Elimu wa Manispaa ya
Ilemela ili kubaini iwapo kituo hicho
kimesajiliwa ama la.
Hata
hivyo, jitihada za JAMHURI kumpata
Mhana ili aweze kuzungumzia tuhuma
zinazomkabili bado hazifanikiwa kwa sababu
kituo kimefungwa tangu juzi na hata
simu yake ya mkononi ( 0756 018 147)inaonesha kuwa
haipo hewani.
“
Katika kumbukumbu zetu hatuna kituo
kinachomilikiwa na mwenye jina unalolitaja. Tumeshaambiwa na
ndio tunajiandaa kwenda huko Msumbiji
kufanya ukaguzi katika kituo hicho” alisema
Mkaguzi Mkuu wa Elimu katika Manispaa ya
Ilemela, Leah Athanas, wakati alipoulizwa n JAMHURI .
Kamanda
wa Polisi mkoani hapa, Valentino Mlowola, alikiri
kuwepo kwa taarifa hizo na kwamba ofisi
yake inaendelea na uchunguzi.
Alisema
ni haki ya mtuhumiwa kupata dhamana na
atakamatwa na kufikishwa mahakamani mara
uchunguzi utakapokamilika.
Kumbukumbu
za Polisi(JAMHURI limeziona) zinaonesha kuwa tukio
hilo liliripotiwa katika kituo cha Polisi Kirumba
siku ya Machi 19 mwaka huu majira ya saa 3:10
asubuhi( 09:10 hrs
Post A Comment: