Mkuu wa mkoa wa Mwanza mhandisi Evarist Ndikilo anaongoza maandamano mchana wa leo kwa ajili yakuwapokea Vijana wa timu ya Taifa ya watoto wa Mitaani, iliyo twaa kombe la dunia la Mashindano hayo kwa ngazi ya watoto chini ya miaka 16.
KOMBE KUBWA LA DUNIA. |
Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, mabingwa hao watapokelewa katika eneo la Usagara takribani km 10 kutoka katikati ya Jijini Mwanza na Msafara huo Utaongozwa na Mkuu wa Mkoa , Wakuu wa Wilaya za Mwanza, Wakurugenzi Wanachi wakiwa na matarumbeta, Polisi wa usalama barabarani pamoja na wananchi wa mikoa ya Jirani
Mbali na kuyaongoza maandamano hayo hadi eneo la Uwanja mkongwe wa Nyamagana, Shughuli zingine zitakazo tendeka katika hafla hiyo ni pamoja na kutoa zawadi kwa mabingwa hao pamoja na nasaha mbali mbali zitakazo tolewa na wadau wa soka mkoani hapa.
Timu hiyo ya Watoto wa Mitaani iliyo chini ya kituo cha Tanzania Street Children Accademy, imekuwa na mafanikio makubwa katika siku za hivi karibuni, kwani imesha twaa ubigwa wa Mkoa wa Mwanza mara mbili kwa Timu ya wanawake, ili hali timu ya wavulana hivi sasa inashiriki Ligi daraja la tatu Ngazi ya Mkoa.
Mbali na Ushindi huu, Timu hiyo imewahi kushiriki Mashindano mbali mbali Duniani, ambapo Mwaka 2012 ilipokwenda Nchini Ujerumani Timu hiyo ilishiriki Makombe Manne ya Vijana na kutwaa makombe 2 kama mshindi wa kwanza na mashindano mengine mshindi wa pili kombe Moja na kombe moja mshindi wa sita.
Tayari mkoa wa Mwanza umeweka mikakati mbali mbali kuhakikisha timu hiyo inajengewa mazingira mazuri ili iweze kuwa timu ya kutegemewa katika siku za usoni.
Mashindano makubwa ya kombe la Dunia yanategemewa kuanza mwezi wa 6 tarehe 12 mwaka huu wa 2014 huko Nchini Brazil.
Post A Comment: