HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela, jijini
Mwanza inakabiliwa na changamoto ya uzoaji taka ngumu kutokana na kuharibika
kwa magari ya kuzolea taka hizo.
Hayo yalilezwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya
ya Ilemela, Amina Masenza wakati akitoa taarifa ya Januari hadi Machi, mwaka
huu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Alisema katika kipindi hicho uzoaji na utupaji wa
taka ngumu ulikuwa wa matatizo kutokana na kuharibika kwa magari ya kuzoa taka
ya halmashauri.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo
halmashauri ilikodisha magari kutoka makampuni binafsi ambapo jumla ya tani
1,500 za taka ngumu zilizotolewa katika vituo vya Furahisha na Buzuruga.
Alisema kutokana na uharibifu wa mazingira
unaoendelea katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri kwa ajili ya
maendeleo ya kijamii, halmashauri imeandaa mabango kwa ajili ya kusimika yenye
ujumbe wa kuzia uharibifu wa mazingira.
Masenza alisema katika bajeti ya mwaka 2013/14
halmashauri ilitenga Sh. Mil. 320 kwa ajili ya kununua magari mawili mapya ya
kuzolea taka huku halmashauri ikiwa imeweka makubaliano na mradi wa uboreshaji
wa mazingira ya ziwa Victoria.
Aidha kwa upande wa ardhi Masenza alisema katika
kipindi hicho jumla ya migogoro ya 67 ya ardhi imetatuliwa kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Pia alisema viwanja katika maeneo ya Buhilya,
Nyasaka, Bujingwa, Nyamhongholo na Bwiru zimekaguliwa na mipaka yake
kutambuliwa na kwamba katika kudhibiti
ujenzi ujenzi holela kwa kushirikiana na ofisi ya Mhandisi wa Manispaa nyumba
14 zilibomolewa.
Post A Comment: