Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi. |
Ushawishi ukiendelea. |
Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking'ang'ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari. |
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama. |
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama. |
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu. |
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama. |
Mashuhuda. |
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Wananchi waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na hali ya mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa kuufikia mlingoti huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mwanzo, Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA), Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na majengo ya mahakamani hapo na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao kutajwa.
Mahabusu hao sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola, walitajwa kwa majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Watuhumiwa wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013 na walikamatwa tangu mwaka 2011.
Wakiwa katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi, mmoja wa mahabusu hao walisikika wakisema: “Haiwezekani, tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiziwa kesi. “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo kamatwa tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada ya malalamiko yao, ndipo askari mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie na kuwahoji kuhusiana na madai yao, huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze kuingia mahakamani.
“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema Inspekta Henry.
Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ambaye alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.
“Bado hiyo ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu haiwezi kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu ikisha kuwa tayari huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa kuisikiliza,” alisema.
SEMA ULIVYO IPOKEA.
Post A Comment: