Pichani ni Bibi Sarah Kibonde Msika, aktika Semina iliyofanyika katika chuo cha Fedha TIA tawi la Mwanza kwa ajili ya Semina ya Ufahamu juu ya SSRA. |
JESHI
la POlisi mkoa wa Mwanza wamelalamikia kuhamishwa hamishwa kwenye mifuko ya
hifadhi za jamii na kufanya michango yao mingine kutoonekana katika kuchangia kwenye mifuko ya
hifadhi ya jamii.
Malalamiko
hayo yalitolewa jana na baadhi polisi walioshiriki katik semin ya siku moja
iliyoandaliwa na Mamlaka ya usimamizi na Udhibiti wa Mifuko y Hifadhi za Jamii
(SSRA) iliyohusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii.
Akiongea
kwa jazba katika semina, Martin Nkinga alisema
wamekuwa wakihamishwa kutoka PSPF kwenda NSSF huku michango yao ikikwama njiani
bila kufikishwa kwenye mfuko husika na hivyo kuwasabishia kero ya kufuatilia
kila wakati bila mafanikio.
Wakati
hayo yakijiri, Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa (NSSF) na ule wa Bima ya Afya (NHIF)
umezidi kuonyooshewa vidole na wadau wao mbele ya Mdhibiti na msimamizi wa
mifuko ya hifadhi ya jamii katika semina za wadau zinazoendelea jijini humo
Askari wakifatilia kwa makini Semina hiyo. |
Wakiongea
kwa uchungu askari Polisi hao Mwanza mbele ya Maafisa wa SSRA hapo jana wamesema,”’
‘ NSSF imekuwa kero kubwa kwa wateja wake ikilinganishwa na mifuko mingine ya
hifadhi ya jamii kwani mfuko huo mbali ya kuwa na Vitega uchumi vingi bado
wanachama wao wameendelea kuwa wa hadhi ya chini zaidi”,alisena na kuongeza.
“Inashangaza
kuona mtu umechangia sawa sawa na mwingine katika muda unaolingana kazini
lakini mwisho wa kustaafu unakuta sisi wa NSSF tunapata mafao kiduuuchu sana
ikilinganishwa na mwalimu au mtumishi mwingine aliyekuwa akichangia katika
mifuko mingine” alisema mmoja wa polisi hao.
Huku
Mkaguzi msaidizi wa Polisi Msangi yeye kiliochake aki kipeleka kwenye mfuku wa
bima ya afya, (NHIF), kwamba hivi sasa wamekuwa na masharti magumu kwa wanachama
kana kwamba matibabu wanayo yapata niya bure kumbe wanachangia mishahara yao, “Haiwezekani
mtegemezi mtu amemuandika katika orodha ya wategemezi lakini inapofika wakati
mtu huyo ameugua eti hatambuliki kwakuwa tuu jina lililokuwa kwenye
kitambulisho na lile la muajiriwa havirandani wakati mimi nakatwa mshahara
wangu tena bila yakuulizwa, huu ni unyanyasaji wa hali ya juu sana”.
Kwa
upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa SSRA, bibi Sarah Kibonde Msika
akitoa majibu kwa wadau hao alisema, “ Ni dhahiri kwamba zipo changa moto kadha
wa kadha kwenye mifuko hii na sio rahisi kuzimaliza kwa wakati mmoja lililopo
ni kwenda nazo taratibu na muda utafika, kama sio kuzimaliza basi tutazipunguza
kwa kiwango kitakacho leta tija kwa wanachama.
Awali
akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa watu kujiunga na Mifuko ya hifadhi ya Jamii
kwa watumishi wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Mwanza alisema, kujinga na
mfuko wa hifadhi ya jamii sio kujitabiria mabaya bali kujiweka tayari kwa
wakati wa badae “ Kwa hivi sasa wengi wetu tunajiona tunanguvu nyingi za
kutuwezesha kukimbia huku na huko kwa ajili yakujitafutia riziki ni vema, tukatumia
kama wakati wa kujiwekea akiba ya badae” alisema Kibonde na kuongeza.. “ Mimi
hapa kama mfano wa kuigwa nimejiunga na mifuko miwili mmoja ukiwa ni wa lazima
na mwingine wa hiayari ambayo siku moja itanisaidia hata kusomesha watoto wangu
alisema Bibi Kibonde.
SSRA
walio anzishwa kwa Mujibu wa Sheria namba 8 ya Mwaka 2008hivi sasa wanaendelea
na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya
jamii katika mkoa wa Mwanza ambapo hapo kesho viongozi wa shirikisho la wafanyakazi
katika Mkoa wa Mwanza watapatiwa elimu hiyo kwenye ukumbi wa Walimu uliopo
kirumba.
Kwa mujibu wa SSRA hadi hivi sasa ni watanzania wapatao Mil.1.8 tu ndio walio jiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, wakati nguvu kazi yenye uwezo wa kuzalisha ni mil.22, suala ambalo linawalazimu SSRA kujizatiti na kutoa Elimu kwa umma hivi sasa, ambapo hapo jana walitoa elimu kwa Watumishi wa Serikali ya Mkoa na hivi leo wametoa elimu hiyo kwa Askari Polisi pamoja na wanafunzi wa Chuo usimamizi wa Fedha nchini TIA.
Koplo Kelema akitoa kilio chake mbele ya Maafisa wa SSRA. |
Liberatus Chonya, Afisa Uhusiano wa SSRA akinukuu mambo muhimu katika Semina hiyo. |
Mmoja ya walimu wa TIA Tawi la Mwanza akitoa maelekezo kwa washiriki kabla ya Semina kuanza. |
Maafisa wa Polisiwakisikiliza kwa makini Semina hiyo kutoka SSRA. |
Hapa darasa linaendelea kwa wanasemina kumsikiliza mtoa mada kwa umakini wa hali ya Juu. |
Tungependa kufahamu upi ni Mfuko bora wa Hifadhi ya Jamii kuliko mwingine, Ni baaadhi ya maswali yaliyo ibuka |
Semina hiyo iliwahusisha askari wa Jinsia zote. Pichani ni Msaisizi wa Polisi Msangi mkuu wa kituo cha Polisi akitoa ushauri katika semina hiyo. |
Post A Comment: