HUU NDIO MNARA ULIOZINDULIWA HUKO SENGEREMA MKOANI MWANZA KWA MADHUMUNI
YAKUPINGA NA KUTOKOMEZA KABISA MAUWAJI YA ALBINO HAPA NCHINI.

Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya watu wenye albinism waliouawa.
Kabla ya uzinduzi huo maandamano yalifanyika yakihusisha wageni pamoja na wananchi wa wilaya ya Sengerema walio hamasika na mpango huo ulionuia kutokomeza kabisa mauaji hayo ya kinyama. 
Viongozi wa kada mbalimbali wilayani Sengerema wakiwa na Rais wa Under the Same Sun Bw. Peter Ash wakisoma majina ya watu wenye albinism waliouawa kwa matukio ya ushirikina.
Mnara uliozinduliwa unamwonyesha baba asiye na ulemavu wa ngozi akiwa amembeba mabegani mtoto wake mwenye albinism huku mama ambaye pia hana ulemavu wa ngozi akisaidia kumvika kofia mwanaye. Kumbe sasa hata baba na mama wasio na albinism katika mwonekano wa ngozi ya kawaida wanaweza kuzaa mtotomwenye albinism.
Pia Shirika hilo la Kimataifa la kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngoziduniani kupitia Taasisi yake ya Under the Same Sun limetoa tuzo ya kwanza duniani kwa vyombo vya habari 127 hapa nchini ikiwemo kampuni ya IPP MEDIA ambayo imejinyakulia ushindi mkubwa wa tuzo 5. Pichani Mwakilishi wa ITV Cosmas Makongo akitoka kupokea moja kati ya tuzo.

Ni tuzo ya kwanza duniani kwa vyombo habari na waandishi wake ambao wameibuka washindi kwa kuhamasika kufuatilia kwa ukaribu matukio mbalimbali yaliyojitokeza na kuyawasilisha kwa jamii.





Mwakilishi wa ITV Cosmas Makongo akipata mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Tawala wilaya ya Sengerema Alfred Kapole mara baada ya kupokea Tuzo kwa Kampuni yake ya IPP kupitia ITV kwa kutangaza bure habari na vipindi vilivyokuwa vikihamasisha kupungua kwa mauaji ya kinyama dhidi ya albinism hapa nchini.

Rais wa Under the Same Sun Peter Ash akitoa hotuba yake kwa jamii iliyofurika katika viwanja vya Telecenter mjini Sengerema. Huku akiwa na baadhi ya watu walioathirika  na matukio ya kinyama walio nusurika kuuawa wakipoteza baadhi ya viungo vyao. Kutoka kushoto ni Bi. Mariam ambaye alipoteza mikono yake kwa kukatwa mapanga na watu waliokuwa wakihitaji viungo vya albino kwaajili ya masuala ya ushirikina, mtoto Festo aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na kukatwa kabisa mkono wake wa kushoto huku aking'olewa meno pamoja na Said Abdalah mkulima mkata mkaa aliyekatwa mkono wake wa kushoto kwa imani hizo hizo. Inasikitisha.

Wadau wa Taasisi ya Under the Same Sun Vick Ntetema (L) na Gamariel mboya (R).
Nao wazazi wenye watoto wenye albinism walifika eneo la tukio kupata elimu. Kutoka kushoto ni Daudi Nzila akiwa na mwanae Elikana na Mathayo Felician akiwa amempakata mwanae Faustin.
Mahudhurio yalikuwa makubwa huku huzuni ikitawala.
Wanahabari mstari wa mbele kunasa matukio.
Eneo lilifurika watu kiasi cha wengine kujikita pembezoni mwa barabara.
Mwanadada Mariam aliyekatwa mikono yake yote na wavamizi, aliwatoa machozi wengi kwa simulizi ya mkasa wake.

Mwalimu Peter akisoma risala ya Kikundi cha albinism Sengerema kwa mgeni rasmi.
Wananchi wakigawiwa vipeperushi na majarida ya Taasisi inayopambana na ukatili dhidi ya watu wenye albinism ya Under the Same Sun.
Elimu toka kwa majarida.
Wageni wadau wa Taasisi ya Under the Same Sun, ambapo kulia ni Bi. Maphordens Soto ambaye ni Mfamasia Bingwa wa kutengeneza losheni za kuwakinga albinism dhidi ya miale mikali ya mwanga wa jua inayo athiri ngozi zao.
Blogger G. Sengo.
Mnara huu wa kwanza wa kihistoria dunia umesimikwa katika kipita shoto kikuu kinachounganisha barabara zinazoelekea mkoa wa Geita, Kahama, Bukoba mkoani Kagera na Kamanga mkoani Mwanza, ukiwa umeorodheshwa majina takribani 72 ya watu wenye albinism waliouawa.
Axact

Post A Comment: