MKUU WA MKOA WA MWANZA KATIKA MOJA YA MAJUKUMU KUHIMIZA MAENDELEO (PICHA ZOTE NA MAKTABA YA BLOG HII). |
WATAALAM WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA WAKIWA ZIARANI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO. |
WATAALAM WA SEKRETARIETI WAKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MWANANCHI WAKATI WA UKAGUZI WA SHIGHULI ZA MAENDELEO. |
Wachapishaji wa magazeti ya Serikali nchini, Tanzania standard Newspaper (TSN), wamejipanga kuimarisha shughuli zao katika kanda ya Ziwa, na mikoa ya Jirani ya Kigoma na Tabora.
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mwakilishi wa shirika hilo katika kanda ya ziwa, Pius Rugonzibwa, amesema lengo lao nikuimarisha shughuli katika kanda hii kwa kuhakikisha mambo mengi ambayo yalikuwa yamekosa kuripotiwa sasa yanapata kuripotiwa kwa upana mkubwa.
"Ni kweli mhe. Mkuu wa Mkoa kuja kwangu huku, ni pamoja na kuanza sasa kuimarisha shughuli zetu kwani hapo awali tulikuwa na waandishi peke yao, lakini kwa kuona umuhimu wa kanda hii ndio maana nimepangiwa kwenye kanda hii, alisema bwana Rugonzibwa na kuongeza kuwa, yapo maboresho ambayo kama shirika yanaendelea kwenye mchakato ambayo yatasaidia kuimarisha shughuli zetu.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Mwanza, mhandisi Evarist Ndikilo amemuahidi mwakilishi huyo ushirikiano wa kutosha na akamtaka kuha kikisha wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kutangaza fursa nyingi zilizopo kwenye kanda hii, " Ndio nafahamu kwamba mna wawakilishi hapa Mwanza, lakini kwa Mkoa mkubwa kama huu, ninaimani yapo mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine hayajatangazwa vyakutosha." alisema na kuongeza "sasa kama kweli mmeamua kujitanua kwa kanda hii ni imani yangu kuwa mtakuwa mstari wa mbele katika kuandika mambo mengi ya kanda hii." Tumekuwa na kongamano la uwekezaji kwa kanda ya ziwa, muitikio ulikuwa mzuri maana wageni wengi walifika na sasa tupo kwenye maandalizi ya tathmini ambayo tunatazamia kuifanya mwezi wa sita."
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha mwakilishi huyo na wenzake kutoka magazeti hayo ya serikali yeye pamoja na wasaidizi wake lakini pia Wataalam wa Sekretarieti kutoa ushirikiano kwa TSN kwa ujumla wake..
TSN, Ni wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Habari Leo, Sunday News pamoja na gazeti la Michezo la Sport Leo.
Post A Comment: