MKURUGENZI MTENDAJI WA UMATI , LULU NG'WANAKILALA PICHANI AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA. |
Chama cha uzazi na malezi bora
nchini UMATI, Tanzania kimeazimia
kwenda Bungeni Mjini Dodoma kwa ajili yakuwakilisha mambo mbali mbali yanayo
kikabili chama hicho, ikiwapo kuongea na mlezi wao ambaye ni Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea na vyombo vya habari
Jijini Mwanza mkurugenzi mtendaji wa UMATI Tanzania, Lulu Ng’wanakilala, alisema
kama UMATI wanadhamiria kwenda Bungeni wakati Wizara zinazohusika na masuala ya
uzazi na Malezi zitakapokuwa zikiwasilisha bajeti zao za mwaka 2014/2015 ili
kuweza kuwashawishi wabunge waweze kuziongezea Wizara hizo bajeti yakutosha kwa
ajili yakufikia malengo ya Milenia katika masuala ya uzazi wa mpango, ambapo
lengo ni kufikia asilimia 60% ifikapo 2015. “Tunadhamiria kwenda Bungeni na
kuonana na wawakilishi wa wananchi, tukiwa na lengo la kuimba Serikali
kuziwezesha Wizara ambazo zinahusika na masuala ya Uzazi kwa ujumla ili ziweze
kutengewa fedha za kutosha katika bajeti ijayo ili tuweze kufikia malengo ya
Milenia” alisema na kuongeza “ kwa hivi sasa kiwango cha matumizi ya uzazi wa
mpango ni asilimia 27% na lengo letu nikufikia aslimia 60% jambo ambalo unaona
tunakazi ya ziada sana kufikia hatua hiyo” aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa
wanazungumza nao katika Hoteli ya Ryan's Bay ya Jijini Mwanza.
Katika hatua nyingine,
Ng’wanakilala, alisema katika mataifa Mengine suala la uzazi wa mpango limekuwa
linauwakilishi rasmi jambo ambalo linasaidia kurahisisha shughuli hizo kwenda
vizuri na sekta husika kutengewa mafungu yakutosha.
UMATI ambayo imekuwa
ikijishughulisha na masuala ya uzazi wa mpango, inakabiliwa na changamoto
nyingi katika vita hivyo, ikiwamo mila potofu zilizopo kwenye jamii kama vile
mwanamke kufanywa chombo cha uzazi hivyo muda mwingi kubakia katika suala la
kuzaa na kulea na hivyo kukwamisha hata shughuli za uzalishaji mali.
Katika hatua nyingine UMATI, imesema
Mikoa ya kanda ya ziwa inayounganisha mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita,
Simiyu na Shinyanga ndio yenye Changamoto kubwa zaidi kwani hadi hivi sasa ni
asilimia 13% ya jamii ndiyo inayo zingatia masuala ya uzazi wa mpango
ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa asilimia 27% huku lengo la kitaifa
likiwa ni asilimia 60% ifikapo 2015, hivyo kuifanya UMATI kuelekeza nguvu kubwa
katika kanda hiyo kwa kuanzishwa kwa Mradi mpya wa Water LLo foundation, ambao umekusudia
kufanya kazi katika Mkoa wa Mara.
UMATI ambayo ilianzishwa mwaka 1959,
imekuwa ikijihusisha na masuala ya uzazi wa mpango kwa Jamii ya watanzania
ambao kabla ya Uhuru walikuwa Milioni 9, huku idadi ya sasa ikifikia milioni 45
na zaidi na kukifanya chama hicho kuongeza juhudi katika kuhakikisha Tanzania
inakuwa na uzazi salama ili kuweza kumfanya mama naye aweze kuingia katika
shughuli za uzalishaji mali.
Post A Comment: