.Mgonjwa mmoja agundulika
.Serikali ya Mkoa, yatoa tahadhari kwa wananchi.
.Serikali ya Mkoa, yatoa tahadhari kwa wananchi.
DALILI ZA DENGUE ZINAVYO JITOKEZA. |
Mtu mmoja Mkaazi wa Jijini Mwanza katika maeneo ya kilimahewa mwenye umri wa miaka (62), amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Sekouture akisumbuliwa na ugonjwa wa Dengue mara baada ya Vipimo kuonesha.
Kwa miujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo siku moja tatu zilizopita kwa ajili ya kuchunguza afya yake, lakini mara baada ya vipimo vya kawaida hakugundulika kuwa na ugonjwa wowote ndipo ilipo mlazimu mtaalam wa maabara kumshauri mgonjwa huyo kupima vipimo vya ugonjwa wa dengue na kupatikana akiwa ameambukizwa virusi hivyo vinavyo ambukiza ugojwa wa dengue.
SOMA TAARIFA NZIMA HAPA CHINI.
KUWEPO KWA UGONJWA
WA DENGUE KATIKA MKOA WA MWANZA
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu, Waandishi wa habari, wawakilishi wa
vyombo vya habari na wananchi wote. Napenda kutoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa
wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza. Hadi sasa kuna mgonjwa mmoja katika Hospittali
ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo. Kufuatia taarifa hii napenda wananchi wafahamu machache kuhusu
ugonjwa wa Dengue. Ugonjwa wa Dengue husababishwa na VIRUS vinavyoitwa “Dengue
Virus” na vinaenezwa na mbu aina ya
Aedes.
Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji
yaliyotuama karibu na makazi ya watu au kwenye vyombo vya kuhitadhia maji majumbani.
JINSI
UGONJWA WA HOMA YA DENGUE UNAVYOENEZWA
Binadamu hupata ugonjwa huu baada ya kuumwa
na mbu wa aina ya Aedes aliye na Virusi vya ugonjwa huu. Mbu
hawa hupendelea kuuma wakati wa mchana.
Ugonjwa huu huwapata wetu wa rika zote aidha
watoto wenye umri chini ya miaka mitano na mama wajawazito huathirika zaidi.
Ndugu
wananchi
Dalili
za Ugonjwa wa Homa ya Dengue
Asilimia 90 ya wagonjwa walioambukizwa
ugonjwa huu uonyesha dalili awali kuanzia siku ya 3 hadi 14 baada ya kuumwa na mbu
mwenye virusi vya ugonjwa huu dalili hizi ni kama zifuatazo:
·
Homa
kali ya ghafla
·
Kuumwa
kichwa hususani sehemu za machoni
·
Maumivu
makali ya misuli pamoja na viungo vya mwili
·
Kichefuchefu
au kutapika
·
Kuvimba
tezi
·
Kupatwa
na harara
Asilimia 10 ya wagonjwa hupatwa na dalili
kali kama kutokwa na damu kwenye sehemu za uwazi za mwili mfano mdomoni,
masikioni pamoja na sehemu za kutolea haja ndogo na kubwa.
Ndugu
wananchi,
Njia
za kujikinga na Homa ya Dengue
Ugonjwa wa dengue unazuiliwa kwa njia
zifuatazo:-
·
Kuangamiza
mazalio ya mbu
·
Kufukia
madimbwi ya maji au nyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi
hayo
·
Kuondoa
vitu vyote vinavyoweza kuwa mazalia ya
mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, chupa na magurudumu ya gari ambavyo
vinaweza kufanya maji kutuama karibu na makazi.
·
Kufyeka
nyasi na vichaka vilivyo karibu na makazi.
·
Kuhakikisha
maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
·
Kufunika
mashimo ya maji taka kwa mfuniko
·
Kusafisha
mitaro na gata za paa la nyumba ili
kutoruhusu maji kutuama.
Kuzuia
kuumwa na mbu kwa:-
·
Kutumia
dawa za kufukuza mbu (Repellents)
·
Kuvaa
nguo ndefu
·
Kuweka
wavu wa kuzuia mbu kwenye madirisha na milango
Kwa kufanya hayo, tunaamini tunaweza kuzuia
maambukizi ya ugonjwa huu yasiendelee kutokea.
Naomba kila mmoja atimize wajibu wake.
Asanteni
kwa kunisikiliza,
Baraka M. Konisaga
KAIMU MKUU WA MKOA
MWANZA
Post A Comment: