Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal leo amekutana na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao yake makuu
jijini Tokyo nchini Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na Rais wa Kampuni
hiyo inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Nobuhiro
Endo.
Ujio
wa Kampuni hii nchini Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa makampuni ya
Japan kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa Makamu wa Rais nchini
Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea Makao Makuu
ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.
Katika
mazungumzo na uongozi wa NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wageni wake
nia ya Tanzania kuona inatanua mawasiliano na teknolojia nchini ili kuinua
uchumi na akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC inakaribishwa hapa nchini
ili kusaidia Tanzania kupiga hatua.
Uongozi
wa NEC nao ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC inaushirikiano wa
karibu na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba wanatarajia kukutana na
uongozi wa wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutazama fursa za kusaidia
teknolojia katika ulinzi.
Imetolewa
na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu
Dar es Salaam Septemba 12, 2014
Post A Comment: