KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA RS MWANZA. |
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.
Ameyasema hayo wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na watumishi hao.
Yambeshi amesema kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo na utata kwa watu " kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo tuongoza" alisema na kuongeza. kuwa suala la kuvujisha siri za serikali ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni lazima ajue kutunza siri.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo ya siasa mahali pa kazi" Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Mbali na masuala la siasa na uadilifu katika kazi ,pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo, kusilikiliza kero mbali mbali za watumishi hao ikiwapo suala la kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.
Awali akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala wa serikali na wale wa serikali kuu.
Hata hivyo katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri itakavyowezekana.
Katibu Mkuu Utumishi ndiye mkuu wa masuala ya Utumishi wa umma katika Serikali ya jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
PICHANI ALIYE SIMAMA NI BWANA KIGERE AFISA MANUNUZI WA RS MWANZA |
KATIBU MKUU UTUMISHI AKISIKILZA MAONI NA KERO MBALI MBALI KUTOKA KWA WATUMISHI WA RS MWANZA |
PICHANI HAPA WATUMISHI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI KATIBU MKUU UTUMISHI, HAYUPO PICHANI KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA. |
BWANA DANNY TEMBA, AMBAYE NI KATIBU WA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SEKOUTURE AKINUKUU DONDOO MUHIMU WAKATI WAKIKAO CHA KATIBU MKUU NA WATUMISHI. |
FARIDA MUSHI AFISA UTUMISHI RS MWANZA, AKITOA MOJA YA KERO KUHUSU KUTOKUELEWEKA KWA BAADHI YA MIIUNDO MIPYA YA UTUMISHI KWA BAADHI YA KADA ZA UTUMISHI WA UMMA. |
MJIOLOJIA WA RS MWANZA PICHANI XAVERY HUMBO ALIPOKUWA AKITOA DUKU DUKU LAKE LA MALIPO MBALI MBALI YALIYOKUWA NA UTATA DHIDI YAKE. |
SAIDI KITINGA PICHANI AKIELEZEA KERO KUHUSU MIKOPO YENYE RIBA KUBWA KWA WATUMISHI. |
MCHAMBUZI MKUU WA MIFUMO YA KOMPUTA BIBI FATMA MATOPE, HAKUKOSA CHA KUMSHAURI KATIBU MKUU UTUMISHI JUU YAKUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI. |
Post A Comment: